Ikiwa kama "maamuzi magumu" ya Waziri Mkuu wa zamani, ndugu Lowassa, yalipangwa na ‘kitengo' au la, mimi kwa kweli nimevutiwa na matokeo yake. Hili, kwangu mimi, ni tikisiko la kihistoria katika mienendo ya siasa zetu toka tupate uhuru; kwasababu ya tikisiko hili, kitu chochote kinaweza kutokea sasa hivi. Tofauti na hapo zamani, wigo wa siasa zetu umepanuka sasa hivi, na siasa zetu zimebadilika! Binafsi, nimevutiwa na vuguvugu hili ambalo, kwa maoni yangu, limesababishwa na mfumo tatanishi. Mtikisiko huu umenivutia kwa sababu moja kuu: kuna uwezekano mkubwa sana kwamba matokeo ya mtikisiko huu yatakuwa ni kufumuliwa kabisa kwa mfumo uliopo na kusukwa upya! Jambo ambalo siku zote nimekuwa nikitamani litokee nchini Tanzania.
Lakini kabla sijaendelea, ili sote twende sambamba nafikiri ni vizuri nifafanue, japo kwa ufupi tu, maana hasa ya neno hili ‘mfumo'. Katika mazingira ya kawaida, mfumo ni mkusanyiko wa vitengo (units) mbalimbali vinavyofanya kazi pamoja kama sehemu ya utaratibu au mtandao wa mitandao, kama vile ubadilishanaji wa taarifa. Aidha, tukiingia zaidi katika maudhui ya kisiasa, neno ‘mfumo' huweza kumaanisha mkusanyiko wa kanuni na taratibu anuai za kiitifaki ambazo kwayo maamuzi hufanyika. Aghalabu utumiaji wa neno ‘mfumo' hutegemea muktadha wa jambo linaloongelewa.
Kwa wale ambao, kama mimi, mliwahi kupata nafasi ya kusomea fani ya uhandisi, hasa katika somo la Ubunifu wa Mifumo au Systems Design, mtakubaliana na mimi kwamba mfumo wa vitu au watu unaweza ukaundwa kwa njia mbili: unaweza ukaundwa kama mfumo mmoja unaojitegemea au unaweza ukaundwa kwa kujumuisha mifumo mingine midogo-midogo inayojikita ndani ya mfumo huo. Kimsingi, siku hizi mfumo wetu wa siasa chini ya CCM umechukua mtiririko wa aina hii ya pili kimfumo. Aidha, kwa muda mrefu sasa, Tanzania tumekuwa tukitumia mfumo ule ule wa siasa tulioanza nao toka tulipojipatia uhuru, mfumo uliosukwa na waanzilishi wa taifa hili, hususan Mwalimu Nyerere. Mfumo huu sasa umezeeka, umepitwa na wakati, na umejisokota sana na kuzaa ‘mifumo-butu' inayosababisha ufisadi – unahitaji kuzongolewa au kunasuliwa – umekuwa ‘mfumo tatanishi'.
Hapo mwanzo, mfumo huu ulifanya kazi yake vizuri sana na ukawa na nguvu kuliko hata ulivyokusudiwa na mbunifu wake, Nyerere. Hii ndiyo sababu tuliweza kuepuka matatizo ya vita vya kikabila na balaa nyingine zilizopitiwa na karibu nchi zote zinazotuzunguka barani Afrika. Mfumo wa Mwalimu ulikuwa madhubuti. Hata hivyo, kadri Mwalimu alivyoanza kuchoka, ndivyo mfumo wake nao ulivyodhoofika. Mpaka wakati mauti yanampata, mfumo wake ulikuwa umenyong'onyea, itifaki zake nyingi kama zile za Azimio la Arusha zikiwa zimenyofolewa, huku makundi ndani ya chama chake yakimea. Hali hii ilisababisha ombwe (void) katika mfumo wake alioutengeneza, jambo ambalo lilizaa ‘vimifumo' vingine zaidi ndani ya mfumo, vilivyotumiwa kwa ubinafsi na makundi yaliyoibuka katika mfumo wenyewe. Ule uzalendo wote wa ile miaka ya sabini, enzi za TANU na CCM mpya, ulitoweka! Leo hii, matokeo ya dhima hili yamekuwa ni kukinzana kwa ‘mifumo ndani ya mfumo' kunakoambatana na migogoro isiyoisha, inayosababishwa na makundi ndani ya chama. Jambo ambalo limekuwa jinamizi kuu kwa CCM, ambalo kama lisiporekebishwa, litasababisha kifo chake hivi karibuni, kama ilivyotokea kwa chama cha KANU katika nchi jirani ya Kenya.
Sasa basi, nionavyo mimi, uamuzi wa ndugu Edward Lowassa umekuja katika wakati muafaka kwa sababu sisi sote lengo letu la msingi ni kuuondoa mfumo huu mbovu unaochelewesha maendeleo yetu. Mfumo uliojaa, ubadhirifu, ukiritimba, ubwanyeye na, kibaya zaidi, rushwa katika ngazi zake zote – toka chini hadi juu! Katika hali yoyote ile, kama tunataka demokrasia ya kweli, ni lazima tuuondoe utawala wa kurithishana wa ki-CCM uliosababisha ‘ukiritimba wa kisiasa' nchini mwetu, ili matakwa ya watu wetu yaweze kuheshimiwa. Kimsingi, ndiyo maana ninampongeza Waziri Mkuu wa zamani, ndugu Lowassa, na viongozi wa UKAWA kwa mkakati wao katika sakata lote hili.
Hata hivyo, ningependa kutoa angalizo moja dogo tu hapa. Ninajua kwamba sisi sote nia yetu ni moja: kujikwamua kutoka katika mfumo mbovu wa kiutawala kama nilivyofafanua hapo juu. Lakini pamoja na msisimko huu wa kisiasa, ukweli wa mambo ni kwamba, ndugu Lowassa kama mwanasiasa ni 'wild card.' Katika mifumo ya kitaalamu ya data ijulikanayo kama SQL Database Systems, sisi wataalamu wa mifumo hii hutumia wild cards zilizo kwenye baobonya (keyboard) la tarakilishi, kama vile alama ya asilimia "%", kinyota "*" na alama iitwayo kareti "^", kuweza kuudhibiti na kuuendesha mfumo wa data hata katika hali isiyo ya kawaida, yaani hali ngumu ya mambo. Sasa basi, katika mfumo wa data, wild cards kama hizi zinaweza kuwa nzuri sana katika kufanikisha majukumu ya kimfumo. Hufanya kazi haraka na kwa ufanisi wa hali ya juu. Lakini tatizo lake ni kwamba, kitabia, zina NGUVU KUBWA sana katika mfumo kiasi kwamba usipokuwa mwangalifu na kuzibatilisha ipasavyo, unaweza ukajikuta unauharibu mfumo mzima mara moja! Mfumo uliotumia kipindi cha mwaka mzima kuimarishwa, kwa mfano, wild cards hizi zinaweza zikauharibu kwa muda wa sekunde moja tu! Nikiwa kama mhandisi, ninamfananisha Lowassa na wild cards hizi, and for the love of God, UKAWA inabidi watafute mbinu imara sana ya kimfumo na kiitifaki ya kumweka kwenye mstari ulio wima - Lowassa must be ‘tamed'!
Hata hivyo, ni dhahiri kwamba gharama ya ‘kumbatilisha' Lowassa (the cost of ‘taming') ni ndogo kuliko gharama za UKAWA kupoteza uchaguzi dhidi ya CCM. UKAWA inahitaji kupambana na huu ‘mfumo tatanishi' mkongwe tulio nao kwa njia yoyote ile, hakuna ubaya katika hili kama sheria za nchi hazivunjwi. Lengo kuu ni kuung'oa utawala wa CCM na kuufumua mfumo wote tulionao, kisha kuusuka tena upya tukianza na KATIBA mpya ya taifa! Mfumo uliopo sasa na Katiba yake umeharibiwa sana na haufai tena kuwahudumia watu wetu. Haupo pale kwa ajili ya maslahi ya wananchi bali kwa ajili ya maslahi ya wachache, hasa vibopa wa CCM. CCM imeuharibu kabisa kiasi kwamba imebweteka na inaona kama vile madaraka na fursa ya kutawala ni haki yao ya kuzaliwa (birthright) – hata kama wakiiba pesa ya umma kama walivyofanya katika ile kashfa ya #escrow. Wao bado wanafikiri kwamba wao tu ndio walio na haki ya kutawala nchi! Hizi zote ni kasoro mbovu za kimfumo na tutaweza kuzirekebisha pale tu CCM itakapopumzika ikawa chama cha upinzani japo kwa muongo hata mmoja.
Na kwa sababu hii, ninawapongeza tena UKAWA kwa mikakati yao, na Lowassa kwa ujasiri wake. Kama Lowassa alilazimika kuyachukua maamuzi haya kwa sababu ya ‘vimifumo vidogo-vidogo' vilivyokithiri ndani ya ‘mfumo tatanishi' hilo halijalishi sasa hivi; lililo la muhimu sasa ni kuuona MWISHO wa ‘mzunguko wa ukiritimba wa kisiasa usioisha' – the looping political monopoly - ulioota mizizi ndani ya mfumo wa siasa zetu. CCM sasa basi – imetoshaa!!
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.