Mfumo ndiyo daraja la kukupeleka katika mji wa uhuru wa kipato (financial freedom)

Mpulusi

Member
Apr 15, 2016
35
31
Kwa kuwa kila mwanadamu anataka maendeleo, basi ni dhahiri kwamba huu mchezo unasheria zake, ambazo wachumi hawataki kuwafundisha raia wengi wa dunia, they call it money game.
Moja ya sheria mhimu ambayo itatufaa leo hapa jukwani ni hii sheria ya ubuni au ubunifu wenzetu huita creativity.
Ubunifu wa aina yoyote hutengeneza mfumo mpya katika kukidhi mahitaji ya viumbe hai hapa duniani, they call it system.
Ukiweza kuwa na mfumo wako, utakaoeleweka na jamii basi hela zitaufuata huo mfumo, maana yake hela zitakuja zenyewe katika mfumo wako ambao mara nyingi hujengwa na akili hiz hiz za kibinadamu, lakini siyo za kawaida, yaani lazima uwe wa tofauti sana ndiyo utaweza kujenga system imara.
Makampuni yote duniani makubwa katika idara zote, ukichunguza kwa akili ya kawaida, unaweza usiamini kama zilitumika akili za binadamu, kama malaika alishuka huv, kumbe la ni binadamu walioamua kuwaza tofauti.
Tunasema mfumo ni daraja la kukupeleka katika mji wa uhuru wa kipato, ambako akili za watu wengine na nguvu zao zitatumika kustawisha mfumo wako, na utalipa kiasi chochote kununua akili zao maana hela zinaufuata mfumo.
Ok ok ndugu zangu, tuzidishe kuwaza tofauti, ili tuwe wa tofauti na hatimaye tutafanya vitu tofauti as great thinkers keep doing everyday, kama watanzania pia tunaweza.
Sheria zipo nyingi ila ADUI WA UBUNIFU NI UBINAFSI. and this going to kill our lovely continent Africa. Mgongano wa mawazo ni afya ya akili...... Karibu
 
Back
Top Bottom