Mfumo mpya unachelewesha mishahara. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfumo mpya unachelewesha mishahara.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kurzweil, Aug 6, 2012.

 1. Kurzweil

  Kurzweil JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2012
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 4,868
  Likes Received: 4,712
  Trophy Points: 280
  MKURUGENZI wa Manispaa ya
  Kinondoni, Fotnatus Fwema,
  amesema kuwa ucheleweshaji
  wa mishahara ya watumishi
  wake umesababishwa na
  mfumo mpya wa serikali
  katika ulipaji.
  Fwema alisema hayo baada
  ya watumishi wa halmashauri
  hiyo kulalamika kuwa
  hawalipwi mishahara yao kwa
  wakati.
  Alisema tatizo hilo
  halijawakumba wao tu, bali
  limeikumba nchi nzima baada
  ya serikali kuweka mkakati
  huo wa kuweka mfumo mpya
  wa ulipaji.
  Akizungumzia suala la
  walimu, Fwema alisema
  ametoa barua yenye
  Kumbukumbu namba KMC/ED/
  PF/ iliyokuwa na kusudio la
  kuwachukulia hatua za
  kinidhamu kwa kushiriki
  mgomo kwa kutofika katika
  kituo cha kazi.
  “Nakiri kutoa onyo kwa
  walimu kupitia barua hiyo,
  nilitoa siku saba tangu
  mwanzoni mwa mwezi huu,
  lakini sitoweza tena
  kuwachukulia hatua kutokana
  na mgomo huo kumalizika
  kwa amani,” alisema.
  Awali watendaji wa
  halmashauri hiyo walisema
  kuwa kitendo cha
  ucheleweshwaji wa
  mishahara katika manispaa
  hiyo ni cha kawaida, tokea
  mwanzoni mwa mwaka huu
  hali inayozorotesha utendaji
  wao wa kazi.
  Pia walisema kuwa hawapewi
  fedha kwa ajili ya saa za
  ziada wanazokuwa kazini,
  ama wanapokuwa nje ya
  kituo kikazi hali
  inayowafanya wajigharamie
  wenyewe.
   
Loading...