Mfugaji amuacha hoi mwandishi wa habari

Mfugaji amuacha hoi mwandishi wa habari

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,627
MWANDISHI:Habari yako mzee, kwani Ng'ombe wako huwa unawalisha nini?

MZEE:Ng'ombe yupi unamuulizia,? Mweupe au mweusi?

MWANDISHI:Mweupe.

MZEE:Huyo namlisha majani.

MWANDISHI:Na mweusi!!!?

MZEE:Namlisha majani pia.

MWANDISHI:Umeanza kufuga lini hawa Ng'ombe wako?

MZEE:Ng'ombe yupi unamuulizia? Mweupe au mweusi?

MWANDISHI: Mweupe.

MZEE:Huyo nimeanza mwaka jana.

MWANDISHI:Na Mweusi!!!?

MZEE:Mwakajana pia.

MWANDISHI:Hivi Ng'ombe wako huwa wanalala wapi?

MZEE:Ng'ombe yupi mweupe au mweusi?

MWANDISHI:Mweupe.

MZEE:Analala hapo kwenye boma.

MWANDISHI:Na mweusi analala wapi!!?

MZEE:Analala kwenye boma pia.

MWANDISHI:Kwanini nikikuuliza kuhusu Ng'ombe wako naww unaniuliza mweupe au mweusi alafu unatoa majibu sawa????

MZEE:Kwasababu Ng'ombe mweupe ndo wakwangu.

MWANDISHI:Enhe! Na huyo mweusi ni wanani??

MZEE:Ni wangu pia.
 
huu uzi ulistahili upelekwe jukwaa la utani
hata hivyo wacha nicheke kabisa kabla haujahamishiwa huko
😀😀😀
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom