Mfanyakazi The Guardian Ltd aaga dunia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfanyakazi The Guardian Ltd aaga dunia

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Feb 4, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,204
  Likes Received: 3,995
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mfanyakazi wa Kampuni ya The Guardian Limited, Michael Salira (70)


  Mfanyakazi wa Kampuni ya The Guardian Limited, Michael Salira (70), pichani, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake Yombo Makangarawe Barabara ya Mwinyi, jijini Dar es Salaam.

  Baba mdogo wa marehemu, Norbert Ikonko, alisema mwanaye aliaga dunia ghafla akiwa amelala nyumbani kwake.

  Ikonko alisema wanatarajia kuusafirisha mwili wa marehemu Salira, kesho Jumapili kwenda katika Kijiji cha Ruaha, Kata ya Mwaya, Tarafa ya Mahenge Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro na kuzikwa siku ya Jumatatu.

  Alisema mwili wa marehemu utaagwa nyumbani kwake Yombo Makangarawe kesho kuanzia saa 7:00 mchana.

  Marehemu alihitimu masomo yake katika Shule ya Sekondari Kwiro mkoani Morogoro mwaka 1959.

  Baada ya kuhitimu elimu ya sekondari, alijiunga na Chuo cha Ualimu Mpwapwa mkoani Dodoma mwaka 1960 hadi mwaka 1961 na kutunukiwa Cheti cha Ualimu Daraja la 1.

  Baadaye, alijiunga na Wizara ya Elimu ambako alifanya kazi hadi alipostaafu mwaka 1995.

  Aliajiriwa rasmi na Kampuni ya The Guardian Ltd Septemba Mosi, 2007 kama Mhakiki Kurasa (Proof Reader), kazi aliyoifanya kwa weledi na uadilifu mkubwa hadi kifo chake.

  Ameacha mjane, watoto wanne ambapo wawili kati yake ni wa kike na idadi kama hiyo wa kiume pamoja na wajukuu wanane.

  Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Salira. Amina.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  Feb 4, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,848
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  RIP kaandae makao ya wengine huko
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,194
  Likes Received: 1,588
  Trophy Points: 280
  Poleni sana.
   
 4. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2012
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,637
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  RIP Mzee...
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,319
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Rip mpiganaji
   
 6. mwenyenchi

  mwenyenchi JF-Expert Member

  #6
  Feb 4, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 653
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Poleni sana
   
Loading...