Mfanyabiashara wa Tanzanite Arusha Afanya uwekezaji Mzito

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Baadhi ya wafanyabiashara wa Madini ya Tanzanite Mkoa wa Arusha,wameitikia wito wa serikali kwa kukubali kuwekeza katika sekta hiyo kwa kuanzisha viwanda vya uchenjuaji na usanifu wa Madini lengo ni kuepukana na suala la utoroshaji wa Madini linalofanywa na baadhi yao wasiowaaminifu katika sekta hiyo.


Akiongea ofisini kwake mfanyabiashara wa Madini hayo,Faizal Shaibhal ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Tanzanite forever lapidary limited amesema kuwa lengo la uwekezaji huo ni kuhakikisha Madini ya Tanzanite yanapanda thamani yakiwa hapa hapa nchini na kuunga mkono matakwa ya serikali yanayotaka Madini yote yachenjuliwa hapa nchini .


Alisema kuanzisha kwa kiwanda hicho ni kuunga mkono Sera ya serikali,inayoelekeza uanzishwaji wa viwanda vya uchenjuaji Madini ambapo amesema kuanzisha kwa viwanda vya uchenjuaji wa Madini vitasaidia kupatikana kwa fursa nyingi za Ajira kwa vijana wa kitanzania na kuongeza uchumi wa Taifa.


"Hadi sasa tumeajiri vijana zaidi ya 20 wa kitanzania kutoka chuo cha Ukataji na Ung'arishaji Vito (TGC) cha jijini Arusha na lengo ni kuwa na vijana wengi zaidi na tutajitahidi kuwawezesha kwa kuwapatia mashine ya kukata Madini ili waweze kujiajiri na kuchangia pato la taifa"


"Tunapofanya Biashara ya Madini tunahakikisha Madini hayo yanalinufaisha taifa na watanzania kwa ujumla ,"Alisema Faizal


Ameongeza kuwa uwekezaji alioufanya kwa kuanzisha kiwanda hicho cha kuchenjua na kusanifu madini jijini Arusha ni mkubwa kutokana na mashine za kisasa alizofunga ambazo

zinatumika nchi mbalimbali duniani na kwamba kiwanda hicho kitakuwa bora kwa nchi za ukanda wa Afrika.


Aidha Alisema kuwa pia anampango wa kuweka mashine nyingine kubwa ya uchenjuaji wa Madini katika mgodi wa Mererani ili wafanyabiashara wenzake waweze kuitumia kukata na kusanifu madini yao .


Katika hatua nyingine mfanyabiashara huyo amemshukuru waziri wa Madini aliyemaliza muda wake ,Anjela Kuiruki kwa kuwaunganisha wafanyabiashara wadogo,pia waziri wa madini wa sasa Dotto Bitego kutokana na uzoefu wake katika sekta hiyo itakayosaidia kuongezeka mara dufu kwa pato la taifa linalotokana na madini hayo.




Pia ameshukuru jitihada zinazofanywa na raisi John Magufuli katika kudhibiti utoroshwaji wa madini hapa nchini ikiwemo ujenzi wa ukuta katika eneo la uchimbaji wa madini ya Tanzanite, Mererani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara.

IMG-20190303-WA0019.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanzo huwa mgumu, Lakini azma endelevu itanyoosha mwelekeo na ukuwaji utavutia soko la ndani na nje..!! excellent task...
 
Mfanyabiashara Faizal please chukua kadi ya chama uwe salama hata ukìfanya upigaji itakulinda
 
Back
Top Bottom