Mfanyabiashara wa madini, Mathias Manga apigwa risasi

Huyo sio bilionea acheni uongo, huwezi kuwa bilionea wakati hujapiga picha na ZE KING OF ALL SOCIAL MEDIA! :A S wink:
 
We Chalii Umenivunja Mbavu'aje Yani Mtu Apigwe Moto Jana Leo Yuko Fiti Kisaikolojia Kuendelea Na Kampein Aliemshuti Katumia Risasi Ya Kuwindia Ndege Nadhani

Ushangae sasa. Manga hajapigwa risasi ni kujitafutia Umaarufu tyuu.
Huwezi ukapigwa risasi tatu kisha ukaenda kia kumpokea fisadi Lowassa.
 
Arusha imekuwa kama Soweto wakati wowote unaweza kutolewa uhai wako.
Nadhani umaskini tulionao watanzania ni zaidi ya Soweto maana kila dakika 6 kuna mtu anakufa kwa malaria, au magonjwa kama kipindupindu achilia mbali HIV/AIDS. Tufanye jitihada tujiepushe na umaskini kwa kutafuta wanasiasa wanaoongoza watu kufanya shughuli zinazoweza kuwafanya wawe na maisha mazuri kuliko wachumia matumbo yao wasiojali kama mtanzania anayo haki ya kuwa na huduma bora za jamii badala yake wanakamua hata hiyo pesa ya kodi kwa manufaa yao tu......!!!!!!! Inaskitisha
 

nikweli mkuu hawa jamaa wa madini ni mabilionea; kama anamgodi na unatoa mawe vizuri; kuuza madini ya dola laki nane kwa mwaka si ajabu kwa rate ya sasa hiyo ni bilioni na zaidi. mtu anakua na cash milioni 200 kwenye safe ofisini huoni kua ni tajiri kibongo bongo??
 
 

Manga ni bilionea tena wa kiwango cha juu kma anajenga hotel ya 17bn hiyo ni hesabu mpka ikamilike nw iko kwenye finishing.....2011 ametoa madini karibia mwaka mzima kwanini asiitwe bilionea
 
sina hakika na matumizi ya neno ""BILLIONEA"" kwa Arusha....mwenye uwezo wa kuwa na gari zuri, bia kila siku, anafanya shughuli zake mbuguni, basi ni ""BILLIONEA"".

mbona kama unapadiss mbuguni sana jombii...walikufanyaga nini uko??
 
sina hakika na matumizi ya neno ""BILLIONEA"" kwa Arusha....mwenye uwezo wa kuwa na gari zuri, bia kila siku, anafanya shughuli zake mbuguni, basi ni ""BILLIONEA"".

Jamaa anazo na anaweza stahili kuitwa hivyo mkuu. Ana jengo moja kubwa sana pale mbele ya seven up. Hilo jengo lenyewe ni B zaidi ya 50 mpaka likamilike.
 
Kwa nini iwe siasa na isiwe kudhulumiana kwenye biashara zake?
Freeland hapa umeonge neno la maana.
Maana akili zetu tumevyo zi set,kila kitu Siasa tuu,hata mtu akichepuka utasikia siasa tuuu.

Issue za matajiri hawa ni za ndani na wao wenyewe wanajua,na ndio maana wamemzuia asionane na watu.

Na ukitaka post ichangiwe zaidi humu basi ikae kieneo fulani ndio utajua kwamba watu Siasa zimeingiza mafunza vichwani mwetu.
 
sina hakika na matumizi ya neno ""BILLIONEA"" kwa Arusha....mwenye uwezo wa kuwa na gari zuri, bia kila siku, anafanya shughuli zake mbuguni, basi ni ""BILLIONEA"".

Mtu ambae anamiliki migodi mikubwa miwili ya kisasa ya tanzanite, ana magari zaidi ya kumi ya kifahari, anamiliki hotel ya nyota 4 mwanza, na ana apartment kama 20 arusha, na ana malizia ujenzi wa ghorofa 6 ya hotel ya kitalii, achilia mbali vitega uchumi vidogo vidogo kibao, huko kijijini kwenu anaitwaje?
 
Reactions: amu
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…