Mfanyabiashara usijali pesa jali mteja

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
30,202
69,279
Kikubwa nachotaka kieleweke ni huu msemo "jali mteja na sio pesa"

kama tujuavyo kila mfanyabiashara lengo lake ni kuuza kwa wingi bidhaa zake, ili uuze sana lazima uwe na wateja wakutosha,ili uwe na wateja wa kutosha lazima uwe na bidhaa zenye ubora n.k
Nimelisema hili kwasababu kuna wafanya biashara baadhi hawawajali wateja wao hivyo kupelekea biashara zao kushuka ama kudorora... Na kuanza kulaumu ama kumshuku mfanyabiashara mwenzake kuwa anatumia kizizi...!!

Kuna wafanyabiashara mpaka kero kwanza anamajibu ya ovyo,matusi na dhamira yake dhahiri anaonyesha anatamaa na pesa
Inatakiwa ifike kipindi wenye tabia hizi mjirekebishe mnafukuza wateja.

Kwanini ujali wateja..?
Ili upate pesa yake ambayo kwako wewe ndio tageti yako.
Ili upate pesa ya kuendeleza mtaji wako.
Ili mteja aendelee kuja kununua bidhaa zako.
Ili upate wateja wengi kwa wateja wachache ulio nao.

Huo ni mtazamo wangu juu ya swala hilo,nawakaribisha wadau mtaoe na nyie mitazamo yenu... Asanteni.
 
Back
Top Bottom