Mfanyabiashara mwingine wa kihindi atekwa

Kisha Mambosasa wa Tabora (RPC) akakosa usingizi masaa 300 namwisho muhindi akarudishwa hadi dampo wakaacha na gari lao na ndani kukakutwa zana za uvuvi zimetelekezwa
 
Kishori usikute alikuwa anaenda kuwapa elfu 50 tu
 
Kuna uwezekano na mwandishi wa habari hii katekwa wakati anamalizia kuandika hii habari.
 
Unajua haya mambo yalikuwa hayapo bongo.
Sasa hawa wazee wa system wamewaamsha watu waovu wakajua mbinu rahisi ya kupata hela kutoka kwa matajiri.

Sasa inakuwa ni shida aisee.
Ni mwendo wa teka nikuteke.
 
Ni katika kuua soo. Si unakumbuka baada ya Lissu kupigwa risasi, likapangwa tukio la kumpiga sijui mstaafu gani risasi, halafu akakimbizwa kutibiwa South Africa? Lengo ionekane kuna wimbi la wapiga risasi au watekaji, kisha eti watu tuchukulie ni kawaida
 
Unakimbilia wapi? au na wewe unawasiwasi wa kutekwa?
Malizia habari........, Je baada ya kupata ajali?
1: Walikufa au walipona
2: Je huyo aliyetekwa amepatikana au bado
3: Walio mteka walipatikana au walifanikiwa kutoroka

Naomba umalizie hiyo habari vizuri
 
TABORA:
Mfanyabiashara mwingine mwenye asili ya Kihindi aliyefahamika kwa jina la Kishori ametekwa na watu wasiojulikana usiku wa Oktoba 25, 2018 na kisha kuondoka nae sehemu isiyojulikana.

Kwa mujibu wa mashuhuda ambao wameongea na mwandishi wa mtandao wa Dar Mpya mapema leo mjini hapa, wameeleza kuwa, tukio hilo limetokea eneo la katikati ya mji wa Tabora karibu na Golden Eagle hotel eneo ambalo ni jirani na ofisi na makazi yake.

Shuhuda hao wameongeza kuwa, wakati tukio hilo limetokea lilikuwa ni la ghafla na walimchukua na kisha kukimbia na gari na kutokomea huko kusiko julikana.

Hata hivyo imeelezwa kuwa watu hao walimtaka awape fedha ili wamuachie, lakini mfanyabiashara huyo aliwaomba warudi nyumbani ndio wape hizo fedha na watu hao walimkubalia baadae kwenda nae nyumbani kwa lengo la kuzichukua fedha ili wamuachie.

“Wakati usiku wanafika kuchukua hizo fedha alizoahidi angewapa ili wamuachie, tayari jeshi la Polisi walitaarifiwa na walifika baada ya mmoja wa wafanyakazi wa muhindi huyo na wengine kushuhudia tukio hilo. Lakini watu hao walishtukia mchezo huo na kukimbia na mfanyabiashara huyo”.

Habari zaidi zinaeleza kuwa, baada ya watu hao kukimbia na mfanyabiashara huyo walikuja kupata ajali katika barabara ya Ujenzi eneo la hoteli ya Wilca baada ya kugonga mti.
labda yule mangi comedian (RC wa kule mkoani) kahusika baada ya kunyimwa moolah.

who knows....
 
Watu wamekwishaonja utamu wa pesa ya utekaji, hawataaacha. Ni kama "kula nyama ya mtu..."
 
TABORA:
Mfanyabiashara mwingine mwenye asili ya Kihindi aliyefahamika kwa jina la Kishori ametekwa na watu wasiojulikana usiku wa Oktoba 25, 2018 na kisha kuondoka nae sehemu isiyojulikana.

Kwa mujibu wa mashuhuda ambao wameongea na mwandishi wa mtandao wa Dar Mpya mapema leo mjini hapa, wameeleza kuwa, tukio hilo limetokea eneo la katikati ya mji wa Tabora karibu na Golden Eagle hotel eneo ambalo ni jirani na ofisi na makazi yake.

Shuhuda hao wameongeza kuwa, wakati tukio hilo limetokea lilikuwa ni la ghafla na walimchukua na kisha kukimbia na gari na kutokomea huko kusiko julikana.

Hata hivyo imeelezwa kuwa watu hao walimtaka awape fedha ili wamuachie, lakini mfanyabiashara huyo aliwaomba warudi nyumbani ndio wape hizo fedha na watu hao walimkubalia baadae kwenda nae nyumbani kwa lengo la kuzichukua fedha ili wamuachie.

“Wakati usiku wanafika kuchukua hizo fedha alizoahidi angewapa ili wamuachie, tayari jeshi la Polisi walitaarifiwa na walifika baada ya mmoja wa wafanyakazi wa muhindi huyo na wengine kushuhudia tukio hilo. Lakini watu hao walishtukia mchezo huo na kukimbia na mfanyabiashara huyo”.

Habari zaidi zinaeleza kuwa, baada ya watu hao kukimbia na mfanyabiashara huyo walikuja kupata ajali katika barabara ya Ujenzi eneo la hoteli ya Wilca baada ya kugonga mti.
mchongo wa kubalance ya MO , tumestuka !
 
Habari zaidi zinaeleza kuwa, baada ya watu hao kukimbia na mfanyabiashara huyo walikuja kupata ajali katika barabara ya Ujenzi eneo la hoteli ya Wilca baada ya kugonga mti.
Hapa ndio mwisho wa habari yako!?😳
 
Hii habari haijakamilika
 
Baada ya kugonga mti ikawaje ! Rudi kwenye tukio utoe taarifa kamili huku bado wengi hawajakuelewa
 
Back
Top Bottom