Mfanyabiashara kutoa 2m-3m wanaozika waathirika wa Covid 19

nyumbamungu

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
997
828
Kuna taarifa nimezisikia kuna Mfanyabiashara mwenye asili ya Yemen anataka kutoa Sh 2 Milion hadi 3 Milion kwa wale wanaozika waathirika wa Covid 19.

Aliandika barua kwenda kwenye Baraza la Dhehebu la Dini yake kwamba Baraza liiombe Serikali waumini wa Dhehebu hilo wasizikwe kwa utaratibu waliouweka Serikali, bali Baraza likabidhiwe Mwili wakishafanya taratibu zote za Dini ikiwemo Kumuosha, Kumsitiri na Kumuombe Du'wa ndio wapewe.

Kwa upande wa Kuzika Baraza liteuwe Walimu wa Nne hadi Sita na wapewe mafunzo na Wizara ya Afya jinsi ya kumzika Marehemu aliyefariki kwa ugonjwa wa mlipuko usio na kinga wala tiba, kwaajili ya kuupokea mwili na kuuhifadhi Kaburini, kwa utaratibu unaotakiwa na WHO.

Katika barua yake alisema kama atakubaliwa ataoa posho kwa hao wahusika ambao wanne hadi sita kwa kila marehemu watakaomzika atawapa Sh 500,000. Dhumuni la kufanya hivyo "Kila Marehemu anastahiki kutendewa yaliyomema pindi anapofariki"

ANGALIZO: Huyo Mfanyabiashara ajiridhishe kwa kufanya uchunguzi wake binafsi kufahamu ni wastani wa Wagonjwa wangapi wanaodhaniwa kufariki kwa dalili za Covid 19, asiangalie takwimu inayotolewa na Wizara ya Afya akafikiri ni hao 11 waliotangazwa.
 
Kwenye familia yenu wameshakufa wangapi?fanya kumpa list yenu ili uwe umemsaidia kwenye takwimu


Sent using IPhone X
 
Yemen kwao wanazikaje watu waliofariki au wale waliotangulia mbele za haki kipindi cha machafuko IS?
 
Risky business hiyo
Hapo kwenye kuosha hapo
Wapo volunteers huko India wanazika watu waliopatwa na Corona na Kuna donors wengi wanaowasaidia kwa kuchangia hela na magari
Natumaini atapata kibali hicho maana heshima za aliefariki ni lazima katika jamii yetu


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Yemeni ina matatizo sasa kuliko nchi yoyote Uarabuni na hata Africa sifikiri kama ni suala la kuzika tu hapo kuna kiti kingine kuweni makini. Watu hununua watu...
 
Irani marehemu wanasitiliwa kama watu wengine,wanaoshwa na kufanyiwa yale yote Dini inataka, Niliona hii habari BBC. Ila hawa watu wapewa mafunzo maalum ili wasiambukizwe.
 
Back
Top Bottom