Mfanyabiashara, fundi umeme kizimbani kwa Uhujumu Uchumi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mfanyabiashara Anuary Hamdani na fundi umeme Joseph Oswald wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi kufuatia hatua yao ya kuhujumu miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Yusto Luboroga wakili wa serikali Mwandamizi Maternus Marandu alidai, washitakiwa walitenda kosa hilo Agosti 7 mwaka huu eneo la Magomeni Mikumi, jijini Dar es Salaam.

Ilidaiwa kwamba kwa nia ovu, washitakiwa hao kwapamoja waliingilia miundombinu ya Tanesco kwa kuondoa mita ya umeme ya Tanesco kutoka nyumba ya Ahmed Amdani iliyokuwa na deni

Ilidaiwa kwamba, mita hiyo ilikuwa na deni la Sh. 3,521,587.70 na kuwekwa mita nyingine mpya kwa lengo la kukwepa deni hilo.

Baada ya kusomewa shitaka hilo, washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwakuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya Uhujumu uchumi.

Upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na Kesi imeahirishwa hadi Septemba 10 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom