Wapandishwa Kizimbani kwa kukata Nyaya za Umeme za Tsh. Bilioni 2.3

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,370
8,107
Mfanyabiashara Amos Lusekelo na mwenzake Mohamed Mbonde wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kuisababishia hasara Shirika la Umeme (Tanesco) ya Sh2.3 bilioni.

Lusekelo ambaye ni mkazi wa Sinza na Mbonde, wamefikishwa mahakamani hapo leo Desemba 16, 2022, na kusomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mary Mrio.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Sylvia Mitanto, amedai washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Akiwasomea mashtaka yao, wakili Mitanto amedai katika shitaka la kwanza, washtakiwa wanadaiwa Novemba 22, 2022 katika barabara ya Mbezi, washtakiwa waliharibu miundombinu ya Tanesco.

Wakiwa eneo hilo, washtakiwa wanadaiwa kukata nyaya zinazosambaza umeme eneo la Chang'ombe na Kiwanda cha ALAF.

Shitaka la pili, siku na eneo hilo, washtakiwa kwa kukata nyaya hizo, waliisababishia Tanesco hasara zaidi ya Sh2.32 bilioni wakati wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Hakimu Mrio amesema washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina

Washitakiwa baada ya kusomewa mashtaka yanayowakabili, Hakimu Mrio aliwaambia kuwa hawatakiwi kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina Mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali Maalumu.

Upande wa mashtaka umedai, upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na hivyo kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mrio ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 29, 2022 itakapotajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande.

MWANANCHI
 
Kibatala atawatetea maana ndiyo kazi yake kutetea magaidi na waovu wa jamii
 
Kama wanahela watatoka baada ya Siku mbili tu lakini kama ni masikini watasubili sana.awamu ya samia pesa inaamua kila kiltu.Rejea tukio la mfanyabiashara wa mwanza kuua watu wawili hadharani na kufungwa maisha lakini kwa kuwa anapesa ameachiwa huru.
 
Naamini Jenerali SABAYA enzi akiwa kwenye kiti cha kunesanesa alikuwa anawachukia MAWAKILI WA KUJITEGEMEA NA KUWAONA TAKATAKA,lakini leo ndio wamekuwa KIMBILIO LAKE WANAOMSAIDIA KUMTETEA kwenye Kesi zake,kama haujawahi kupata Kesi naamini utaona MAWAKILI ni Takataka,lakini siku likija kukufika ndio utajua umuhimu wa hao MAWAKILI ambao leo unawaona takataka
 
Kama wanahela watatoka baada ya Siku mbili tu lakini kama ni masikini watasubili sana.awamu ya samia pesa inaamua kila kiltu.Rejea tukio la mfanyabiashara wa mwanza kuua watu wawili hadharani na kufungwa maisha lakini kwa kuwa anapesa ameachiwa huru.
Hata kwa Magu wenye pesa walitoka, tena mnakaa chini na DPP mnayajenga
 
mmh hapa Kuna namna.
hizo nyaya wakati zinakatwa kulikuwa na umeme?
Walipanda vipi?
Walizibeba vipi.
 
Mfanyabiashara Amos Lusekelo na mwenzake Mohamed Mbonde wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka mawili likiwemo la kuisababishia hasara Shirika la Umeme (Tanesco) ya Sh2.3 bilioni.

Lusekelo ambaye ni mkazi wa Sinza na Mbonde, wamefikishwa mahakamani hapo leo Desemba 16, 2022, na kusomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mary Mrio.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Sylvia Mitanto, amedai washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi.

Akiwasomea mashtaka yao, wakili Mitanto amedai katika shitaka la kwanza, washtakiwa wanadaiwa Novemba 22, 2022 katika barabara ya Mbezi, washtakiwa waliharibu miundombinu ya Tanesco.

Wakiwa eneo hilo, washtakiwa wanadaiwa kukata nyaya zinazosambaza umeme eneo la Chang'ombe na Kiwanda cha ALAF.

Shitaka la pili, siku na eneo hilo, washtakiwa kwa kukata nyaya hizo, waliisababishia Tanesco hasara zaidi ya Sh2.32 bilioni wakati wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Hakimu Mrio amesema washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina

Washitakiwa baada ya kusomewa mashtaka yanayowakabili, Hakimu Mrio aliwaambia kuwa hawatakiwi kujibu chochote kwa kuwa Mahakama hiyo haina Mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali Maalumu.

Upande wa mashtaka umedai, upelelezi wa shauri hilo haujakamilika na hivyo kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mrio ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 29, 2022 itakapotajwa na washtakiwa wamerudishwa rumande.

MWANANCHI
Sasa kama upelelezi haujakamilika mahakamani wanafanya nini hao watu?!
Hivi si kuna sheria mpya inayokataza kumkamata mtu na kumpeleka mahakamani kabla upelelezi haujakamilika au ilikuwa ni siasa tuu?

Kama hiyo sheria ipo basi ifanyiwe marekebisho kiongezwe kipengele kuwa atakayekiuka sheria hiyo yani kumkamata mtu kumpeleka mahakamani kabla ya upelelezi kukamilika awekwe mahabusu na mahakama imhukumu kifungo cha miezi 6 papo hapo kwa kivunja sheria hiyo.
 
Miaka kama 2 nyuma kuna jamaa walienda kuiba nyanya nyuma ya mitambo ya symbion,kuna nyaya nyingi zimepita,aise walichokutana nacho ni balaa maana walipigwa shots moja matata sana jamaa waligeuka kama mkaaa,na mpaka sasa sijui kama wako hai

Ova
 
Back
Top Bottom