Mfanyabiashara bilionea Dar es Salaam, adai kutishiwa maisha, akimbia kwa pikipiki kutoroka asiuawe hadi Arusha

Huyo mfanya biashara ni mpumbavu tu.
Yaani anaharibu maisha yake kwasababu ya 125 milioni, alafu anajiita milionea..🤔
Mkuu hujamuelewa mhusika ungesoma vizuri kuna kipengele cha kuvunja oda kwa mchina kaambiwa atalipa faini ya dola 18000 plus na hiyo millioni 129 arudishe je, huo mkataba uliosainiwa na wakakubaliana una maana gani sasa au kwasababu yeye ni kigogo serikalini. Kuna vitu vingine mtu anafosi kwasababu yupo kwenye cheo fulani na ndo maana hatuwezi kwenda popote pale kwan huo mkataba si ulisainiwa na mtu kaweka oda je unasitisha oda na ulipe faini pamoja na kurudisha hela uliyowekewa au maisha yako yaende na maji na pia uangalie hustling ulizopiga mapaka umekuwa level za kuitwa millionea ila kama huo umillionea uliupata kwa mseleleko baridi, utalipa faini pamoja na kurudisha pesa.
 
Mwanaume kukubali mambo kirahisi rahisi ni dalili mbaya sana
Ndo maana tunataifa lenye mambo ya hovyo sababu hatuna wanaume wakupigania haki zao kama wewe mtu anaweza akaja akakupiga makofi mbele ya famila yako ukamwacha sababu ana nguvu

Nauhakika wewe sio mfanyabiashara ndo maana unaongea kirahis
 
Hiyo ndo nia yao kutakatisha fedha kwa hiyo hata huo mpango ni wa uongo
 
Ndo maana nikamwambia yeye sio mfanyabiashara na kama ni mwanaume ni hasara kubwa sana kwa familia yake

Mkataba una-taratibu za kuuvunja hauvunjwi kihuni huni alafu kwenye a real man hutakiwi kukubali mambo kirahisi rahis mtu anaweza akaja akakupiga makofi mbele ya famila yako ukamwacha sababu ana nguvu

Huyo kigogo angetakiwa ampange huyo muuza magari mapema kwamba nakupa hela ila baadae utanrudishia na tunasign mkataba kila kitu
Tatizo vigogo wanatumia nguvu na akili kidogo
 
Umeniongezea kitu, kila siku ni kujifunza..

Madhara yake ni yapi?
Madhara yake wanaweza kuchukua zote zilizomo kwenye akaunti. Kwa mfano, unashika simu yako ile tu umeweka password unaanza kutuma unapigwa na kitako cha bunduki kichwani unazimia, halafu wao wanaendelea na mchakato. Ukizinduka wanakurudisha nyumbani kiroho safi au hata kuuawa. Wakikuacha mzima kucheki salio limepungua au limeisha kabisa. Kama una ujasiri ndio utaanza kulalamika na kumuomba rais aingilie kati.
 
Ingia mkataba na taasisi ya umma say kujenga daraja, halafu usijenge simply tu umepata kazi nyingine. Halafu uone nini kitakukuta kwa mujibu wa mkataba na Procurement Act. Huwezi kuamka tu asubuhi, umeshauriana na mkeo usiku unasema nimeghairi. Wanaomuona Shami mpuuzi ni ignorants.
 
Kwa picha ilivyo, mfanyabiashara akivunja mkataba kienyeji na kuwapa pesa hao watu kienyeji, ipo siku atadaiwa malori na kampuni kwa sababu nyaraka za kampuni zinaonesha wameoda magari kwa huyo mfanyabiashara.
 
Hana maelezo kwamba alitishiwa atauwawa.
Ila matendo yake amekua na hofu atauwawa.
Shamy kacheza faulo. Yeye anajinadi kila siku ana uwezo wa kuagiza malori. Watu wamemuamini. Ila anawapiga watu kalenda. Magari anayoyauza. Ukiona mtu kaagiza ujue ana tenda muhimu sana. Naa malipo sio ya kutakatisha. Watu wanatoa hela mfukoni. Wanafanya transaction according tu kipato hizo gari ni gharama. Huwezi toa tu bilioni kijinga.
Transaction iliyotakiwa ni kudeposit kwa wachina. Hela ampewa. Ila analeta ujanja anataka full payment. Huu ujanja huyo mzee anataka kuondoka na hela za watu. Watamlawiti. Si issue sijui mtu mkubwa serikalini. Hata kijana tu wa mtaani akupe hiyo hela umzingue anakulawiti wallahi
 
Umeeleweka mkuu kabisa sio mtu kwasababu ni mkubwa serikalini ndo afanye anachotaka hapana afuate vipengele vya mkataba vinasemaje.
 
Kwa picha ilivyo, mfanyabiashara akivunja mkataba kienyeji na kuwapa pesa hao watu kienyeji, ipo siku atadaiwa malori na kampuni kwa sababu nyaraka za kampuni zinaonesha wameoda magari kwa huyo mfanyabiashara.
Hio ndo point yangu na kuna jamaa nimemwambia hapo juu
Kuna siku atakuja tena atakuambia tuliingia mkataba wa million 900 wa kuleta malori na hukuleta na unatakiwa ulipe

Mambo ya mikataba hayaendi kienyeji enyeji watu wengi hawaeleweli pale hakuna ubinaadamu ni mkataba unasemaje
 
Jamani jamani jamani. Hakuna aliye salama kwenye utawala huu. Uwe tajiri uwe fukara mambo ni yale yale. Ni suala la muda tu. Suluhisho pekee ni kuungana pamoja na kudai katiba mpya ambayo itawatoa CCM na vibaka kama kina Muliro. Mwenye kusikia na asikie.
 
Umeeleweka mkuu kabisa sio mtu kwasababu ni mkubwa serikalini ndo afanye anachotaka hapana afuate vipengele vya mkataba vinasemaje.
Hata kama Huna kitu au huna mamlaka usikubali kuwa zoba kwenye maisha

Unaweza ukatumia ubinadamu kumbe watu wanaroho mbaya kinoma
Na unaweza vunja mkataba kienyeji sababu hao watu ni wahuni
Kuna siku atakuja tena atakuambia tuliingia mkataba wa million 900 wa kuleta malori na hukuleta na unatakiwa ulipe

Mambo ya mikataba hayaendi kienyeji enyeji watu wengi hawaeleweli pale hakuna ubinaadamu ni mkataba unasemaje na maslai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…