Hawa wadada wa nyumbani hawathaminiwi kabisa wanapewa hela kiduchu and yet they are expected kuangalia mtoto/watoto kwa umakini wa hali ya juu. Full disclosure: Mfanyakazi wangu Nampa kima cha mshahara kilichoidhinishwa na serikali (na gharama za matibabu na other costs is on me-including likizo nyumbani kwao mara moja kila mwaka ambayo nalipa gharama mimi)
Mimi nashauri kwetu sote tunaojielewa we should try and professionalize this sector. Kama kima cha chini ni laki moja basi huyu mtu mlipe ujira wake sahihi na wewe u-demand professional delivery kwenye majukumu yake.
Otherwise hizi kesi za kudhuru watoto hazitaisha.
Wewe mtu katoka Iringa or Mwanza (with light touch folks), anakuja mjini unataka kumlipa 40K? Really? Hiyo hela itamsaidia vipi na yeye kutoka kimaisha? Kumlisha si hoja! Unataka awapikie wanao halafu yeye akale wapi?
Cha mwisho, tujitahidi kuwajua vizuri kabla ya kuwaajiri. I mean, tusichukulie kirahisi rahisi tuu. Know her/his background. Jua nyumbani kwao na details muhimu. Imagine leo amefia kwako (God forbid) where do you go? mtu ambaye umempata kwa PM ya Jamii Forum?
In all hawa watu ni wa muhimu sana. Lakini Jamii imewasahau. Ndo maana hata ukienda kwenye sherehe utakuta hata kama mama mwenye mji/mualikwa amependeza namna gani..anaendesha usafiri wa maana......lazima house girl utamjua tuu! (either kavaa nguo ambazo hazimtoshi vizuri-za kupewa mara nyingi, muoga muoga nk). Wakati tajiri yake anang'aa!).
My point is tuwajengee confidence na wajione part of our families. Maana mtu anayeshinda na wanao ni wa kuheshimu sana.