Mfano wa Picha ya Mto Msimbazi ulivyokuwa

Kim Jong Jr

JF-Expert Member
Mar 15, 2014
10,986
20,401
Mfano wa Picha ya mto msimbazi kabla ya kuvamiwa na wananchi walioanzisha makazi yao maeneo mbalimbali unapopita mto huo 1451908720777.jpg Huu ni muonekano kwa sasa eneo la mto lilivyo mara baada ya uvamizi wa wananchi na kuanzisha makazi yao kinyume na sheria



Kesho Tarehe 5.1.2015 zoezi la ubomoaji litaendelea lakini hivi watendaji wetu wenye mamlaka ya kusimamia sheria ya mazingira walikuwa wapi mpaka kufikia uharibifu wa namna hii????.... Hivi ni hasara kiasi gani wamewaingizia wananchi ambao walikuwa wamejitutumua kujenga hivyo vibanda walau wapate kujistiri wao na familia zao...

Simaanishi kuwa wananchi hawana makosa.Wana makosa kwa mujibu wa sheria. Na either kujua ama kutokujua sheria za mazingira si sababu ya kuwekwa au kutokuwekwa hatiani.. Rai yangu msumeno ule ule unawaondoa ndugu zetu maeneo haya uhifadhiwe ili utumike kuwashughulikia watumishi wooote waliohisika na ustaw wa maeneo haya kinyume na sheria
 

Attachments

  • 1451908615044.jpg
    1451908615044.jpg
    14.3 KB · Views: 129
  • 1451908825152.jpg
    1451908825152.jpg
    27.1 KB · Views: 93
Last edited:
Mfano wa Picha ya uliokuwa mto msimbazi kabla ya kuvamiwa na wananchi walioanzisha makazi yao maeneo mbalimbali unapopita mto huo View attachment 314825 Huu ni muonekano kwa sasa enep la mto lilivyo mara baada ya uvamizi wa wananchi na kuanzisha makazi yao kinyume na sheria
Duh!
Hatari sana, wahamishwe tu, huo ni uharibifu wa maIngira.
 
Mfano wa Picha ya uliokuwa mto msimbazi kabla ya kuvamiwa na wananchi walioanzisha makazi yao maeneo mbalimbali unapopita mto huo View attachment 314825 Huu ni muonekano kwa sasa enep la mto lilivyo mara baada ya uvamizi wa wananchi na kuanzisha makazi yao kinyume na sheria

Yaani ni Kinyaa! Hadi mtu unaona aibu kuitwa msomi wa Kitanzania...je hao waliokuwa kwenye uongozi?
 
Mfano wa Picha ya mto msimbazi kabla ya kuvamiwa na wananchi walioanzisha makazi yao maeneo mbalimbali unapopita mto huo View attachment 314825 Huu ni muonekano kwa sasa eneo la mto lilivyo mara baada ya uvamizi wa wananchi na kuanzisha makazi yao kinyume na sheria



Kesho Tarehe 5.1.2015 zoezi la ubomoaji litaendelea lakini hivi watendaji wetu wenye mamlaka ya kusimamia sheria ya mazingira walikuwa wapi mpaka kufikia uharibifu wa namna hii????.. Rai yangu msumeno ule ule unawaondoa ndugu zetu maeneo haya uhifadhiwe ili utumike kuwashughulikia watumishi wooote waliohisika na ustaw wa maeneo haya kinyume na sheria
Mkuu hapo umenena.Washtakiwe kwa akosa ya uzembe wa kutowajibika na wizi kwa kupokea mishahara pasipo kutimiza wajibu.Huo ni utapeli kulipwa kwa kazi ambayo hujaifanya.Na sasa hivi wananchi tumechoka na hatutaki kusikia hii habari kuwa serikali haiwezi kuwashughulikia maofisa hao eti makosa hayo yalifanyika awamu zilizopita .
 
ekari za viwanja wanapewa wawekezaji huku mwananchi anabomolewa bila kupatiwa eneo la kujisitiri wakati kuna mapori kibao dar es salaam hadi yanatumika kwenye uhalifu
 
inatakiwa wavunjiwe wote, mto usafishwe na pembeni mwa mto zitengenezwe garden bora za kijaniiii, ili wanaofunga ndoa waende wakapigie picha kule na waweke na public benches ili watu tuwe tunaenda kupumzika na wake zetu kutafakari maisha mida ya jioni. safisha kabisa bonde lote hilo. hata uwanja wa timu yangu ya yanga futilia mbali kule.
 
Hela yangu kuliko kujenga maenea kama hayo ni bora nikaitumbue yoote iishe
 
Back
Top Bottom