Mfano wa Kuigwa CCM & Chadema; Huu Hapa!

Mfano wa Kuigwa CCM & Chadema; Huu Hapa!

William rudi ng'ambo, bongo imeshakuchanganya. Hapo la kuiga ni lipi?

- ha! ha! ha! mkuu more swaggaz, I mean nilipoanzisha tawi la CCM nikiwa ng'ambo si mlisema nimechanganyikiwa, sasa na huku tena vipi? ha! ha! ha! sasa unataka nirudi kule nikachanganyikiwe zaidi? ha! ha1 ha!


William.
 
​
Kamanda James Mwakibinga, kada wa CCM akiwa na watoto wadogo huko Kawe, hii ndio moja ya njia muhimu sana ya kuimarisha chama chochote cha siasa, ni kuanzia kwa watoto wadogo.

- Huu ndio mfano wa kuigwa na chama chochote cha siasa iwe hapa au Duniani popote pale, hope CCM will take a note here, kwamba zamani Mwalimu Nyerere alifanya haya ya kufikisha chama kwa wananchi kwa kuanzia na watoto, tukiwa watoto tulicheza halaiki, tulicheza Chipukizi, tukiwa Sekondari tulicheza halaiki, and then tulienda JKT!

- Siku hizi ni kila mtu na lwake, ujitahidi mwenyewe tu ufike juu hamna matayarisho no wonder tunakuwa na viongozi wasiowakamilifu na itikadi tena wengi sana!



William.
Umeonae. CCM imepoteza dira kama ambavyo Mwalimu na Baba yako walitaka iwe. Ndo maana baba yako siku hizi kimya baada ya kuumizwa kwenye mchakato. Na wewe vile vile ukaumizwa kwenye mchakato wa EALA pamoja na elimu yako nzuri. Ndo maana umepost hii thread. Basi pambana hadi mwisho.
 
​
Kamanda James Mwakibinga, kada wa CCM akiwa na watoto wadogo huko Kawe, hii ndio moja ya njia muhimu sana ya kuimarisha chama chochote cha siasa, ni kuanzia kwa watoto wadogo.

- Huu ndio mfano wa kuigwa na chama chochote cha siasa iwe hapa au Duniani popote pale, hope CCM will take a note here, kwamba zamani Mwalimu Nyerere alifanya haya ya kufikisha chama kwa wananchi kwa kuanzia na watoto, tukiwa watoto tulicheza halaiki, tulicheza Chipukizi, tukiwa Sekondari tulicheza halaiki, and then tulienda JKT!

- Siku hizi ni kila mtu na lwake, ujitahidi mwenyewe tu ufike juu hamna matayarisho no wonder tunakuwa na viongozi wasiowakamilifu na itikadi tena wengi sana!



William.

Ilikuwa saa ngapi? Anaweza shitakiwa huyu, hawa si watoto wa shule? Tena naona kama darasa nyuma yake.
 
Ndio maana kiwango cha elimu kinazidi kuporomoka,shule na siasa wapi na wapi?msiwashirikishe watoto kwenye michezo yenu michafu waacheni wasome.
 
Leo hii let these vyama viweke acivities za uzalendo zaidi....

ukisema vyama vishuke mpaka huko primary kujijenga ......!! usije ukakuta watoto wanauawa! kwa nini?

sasa kama chama ukisema tu unataka kugombea urais unataka kuliwa nyama mtoto gani ataota ndoto za kuwa rais kupitia chama hicho!! usije ukakuta Bavicha wataongea na wakuu wa shule kuwa mtoto akisema tu anataka kuwa rais kwa chama chao atimuliwe shule.....!! sound joking??? no..very serious problem

ukiwa mshabiki wa vyama ujue una mzigo afadhali uwe mshabiki wa Yanga, ukila tano na simba mnamtafuta mwenyekiti yuko wapi!
Mkuu Waberoya, labda mataifa mengine ambayo kila kitu tumekuwa tukikopi toka kwao wamesonga mbele sana. Nimekuwa nikijiuliza, hivi Romney angetangaza nia yake ya kugombea urais wa US kwenye congress ya Democrats, ingekuwa na athari gani kwenye ambitions zake? Angeendelea kuaminiwa na Republicans?
 
Hayo ilikuwa rahisi kufanya kipindi cha chama kimoja, kwa sasa hayo hayawezekani tena. Huwezi kusema Chadema, CCM na CUF waanze kuingia mashuleni kuhamasisha vijana , hapo itakuwa vurugu mechi. Mimi siwezi kumjaza mwanangu itikadi za kichama nataka akue mwenyewe aamue nini ni kizuri kwake.

Ki misngi na kuunga mkono, hayo hayawezi kufanyika sasa hivi kwa maana kuna vyama vingi vya siasa. Lakini ikumbukwe kuna makosa mengi watanzania tunayafanya bila kujua. Naomba nianzie kutoa maana ya elimu kama alivyo wahi kusema mwalimu Nyerere: "Education is the transfer of knowledge and skills from one generation to the other" CCM wamekuwa wakiifanya na ndio kuna malalamiko kwamba waliokuwa wanasiasa huko nyuma watoto wao ndiyo wanzo nafasi za kiasiasa kwa sasa hivi. Unafikia wakati inaletwa dhana ufalme na kurithishana hata madaraka.


Nitamshangaa mwanaCHADEMA ambaye anasubiri mwanae akue ndio aamue kujiunga ya chadema. Tunahitaji kuwashawishi watoto wetu kuwa waadilifu ili wakikua wajiunge na chadema kwa maana uadilifu ndio msingi mmojawapo wa kujiunga na CHADEMA. Tuwashauri watoto wetu wawe na adabu njema mbele ya jamii kwa maana msingi mwingine wa Chadema ni nguvu ya umma. Mtoto ashauriwe kusoma magazeti yanayoonyesha mrengo wa siasa za chadema. Ukimwachia asome udaku ataendelea na udaku hata anapokuwa mtu mzima.


Watoto wetu wanahitaji kuelekezwa na kusaidiwa kujua yaliyo bora ndio tutajenga jamii bora na endelevu.
 
- Kule US Jeshi la Amerika hupeleka matoi ya kijeshi kwenye shule za chekeckea kuwatayrisha na vita mbele ya safari, unafikiri US wanaingia vita kwa bahati mbaya, hapana ni national interest, huwa inaazia kwenye watoto!



William.[/Q

....to be honest mie huwa sikuelewi, nisamehe
 
​
Kamanda James Mwakibinga, kada wa CCM akiwa na watoto wadogo huko Kawe, hii ndio moja ya njia muhimu sana ya kuimarisha chama chochote cha siasa, ni kuanzia kwa watoto wadogo.

- Huu ndio mfano wa kuigwa na chama chochote cha siasa iwe hapa au Duniani popote pale, hope CCM will take a note here, kwamba zamani Mwalimu Nyerere alifanya haya ya kufikisha chama kwa wananchi kwa kuanzia na watoto, tukiwa watoto tulicheza halaiki, tulicheza Chipukizi, tukiwa Sekondari tulicheza halaiki, and then tulienda JKT!

- Siku hizi ni kila mtu na lwake, ujitahidi mwenyewe tu ufike juu hamna matayarisho no wonder tunakuwa na viongozi wasiowakamilifu na itikadi tena wengi sana!



William.

nini chA kuigwa hapo mkuu! hao watoto wanafurahi kupiga picha tuu, hawajui lolote, hata hayo madole gumba waliyoomyesha itakuwa wameambiwa wafanye hivyo....ndio maana wengine wanapungia coz hawajui chochote zaidi ya kupenda kamera a.k.a picha...
 
- Kule US Jeshi la Amerika hupeleka matoi ya kijeshi kwenye shule za chekeckea kuwatayrisha na vita mbele ya safari, unafikiri US wanaingia vita kwa bahati mbaya, hapana ni national interest, huwa inaazia kwenye watoto!

ACHA UJINGA WAKO WE DOGO NA SERA ZAKO ZA MAREKANI, KWAHIYO MAREKANI WAMERUHUSU MASHOGA NA WASAGAJI, NA SISI TURUHUSU? KWANINI USIJE NA REFERENCE ZA TANZANIA, MAANA NAUHAKIKA TULIKUWA KWENYE MSITARI MZURI TUKAJIKWAA SEHEMU. UKITAKA KUJUA ULIVYOCHAFUKA, ANGALIA ULIPO ANGUKA, NA ULIVYO ANGUKA
SHAME ON YOU,
KWELI NAANZA KUFAHAMU KWANINI CCCCM INAKUFA
 
Mfano mbaya wa kuigwa maana watoto walitakiwa kuwa darasani.

Pili why CCM & CHADEMA tu wakati kuna vyama kibao? Ubaguzi wa kisiasa siyo?
 
William,

Ingekuwa vyema kama ungetuwekea na clip zake, ili tusikie kitu anachozungumza. Kwa mawazo yangu, ni ngumu sana kuitetea CCM kutokana na mambo mengi mabovu iliyoyafanya. Nchi imebarikiwa madini ya kila aina, dhahabu, mbuga nzuri za wanyama , ardhi yenye rutuba lakini wananchi wake ni masikini wa kutupwa. Chama hiki ndicho kinachotunga sera za taifa...Inahitaji moyo wa mamba kukitetea hiki chama.
 
Wiliam, uchokozi unauanzishwa mwenyewe, watakunanga ile mbaya! Wewe una mwili mkubwa na bichwa kumbe ubongo wako sawa na wa sisimizi. Huelewi serekali yako ya magamba imepiga marufuku siasa mashuleni? Au kwa vile nawe Vasco dagama, hujui kinachoendelea? Hukumbuki kuwa kuna mtoto alibeba bango lililoandikwa kikwete kama nchi imekushinda niachie mimi hapa Ruanda Nzovwe mbeya. Magamba mlipiga kelele nchi nzima, wewe uliku umelala? Kijana shauri yako.
 
- Kule US Jeshi la Amerika hupeleka matoi ya kijeshi kwenye shule za chekeckea kuwatayrisha na vita mbele ya safari, unafikiri US wanaingia vita kwa bahati mbaya, hapana ni national interest, huwa inaazia kwenye watoto!


uwiiii umeanza mambo yako ya transamerica sijui international exposure mara sijui intercontinental nini yale yaleeeee ya bungeni siku ile...hivi huwezi kutoa mifano ya mvumi au chakwale mpaka uanze kule US....mwe hebu ngoja ni sisi tuje kuenda siku moja maana mnatuonea kweli...mweeee chonde chonde ndugu yangu chegweyemisi
 
hao watoto waliambiwa kua wanapiga picha na GAMBA? usifananishe enzi za nyerere na sasa hivi....nyerere hakua fisadi
 
Siungi mkono hoja that is it. Subiri wafike chuo
 
Hivi huyu William ndio angekuwa mbunge wetu EAC?! E bwana tungeliwa vibaya, ana upeo kiduchu sana maana mipost yake huwa ovyo.
 
By the time hao watoto wanafika umri wa kupiga kura CCM will dead and buried longtime!!
 
Malecela pale ninapoona sioni cha kujivunia nchi yangu hii ya mama yangu, narudi those days....naanza kuimba wimbo mmoja baada ya mwingine, nakumbuka marafiki zangu wa kipindi hicho, dunia isiyo na huruma imetutupa huko na huko!

Longing for the past (nostalgia) is always my desire!

My all time fav. song is,

Tazama ramani utaona nchi nzuri, yenye mito na mabonde mengi ya nafaka
Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri, nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzania
Majira yetu haya yangekuwaje sasa? Utumwa wa nchi Nyerere ameukomesha
.

Chemchem ya furaha ama nipe tumaini, kila mara kwako niwe nikiburudika.
Nakupenda hasa hata nikakufasiri, nitalalamika kukuacha Tanzania.
Majira yetu haya yangekuwaje sasa? Utumwa wa nchi Nyerere ameukomesha.


Nchi yenye azimio lenye tumaini, ndiwe peke yako mwanga wa Watanzania
Ninakuthamini hadharani na moyoni, unilinde nami nikulinde hata kufa.
Majira yetu haya yangekuwaje sasa? Utumwa wa nchi Nyerere ameukomesha
.


xxxxxxxx

du........!
 
​
Kamanda James Mwakibinga, kada wa CCM akiwa na watoto wadogo huko Kawe, hii ndio moja ya njia muhimu sana ya kuimarisha chama chochote cha siasa, ni kuanzia kwa watoto wadogo.

- Huu ndio mfano wa kuigwa na chama chochote cha siasa iwe hapa au Duniani popote pale, hope CCM will take a note here, kwamba zamani Mwalimu Nyerere alifanya haya ya kufikisha chama kwa wananchi kwa kuanzia na watoto, tukiwa watoto tulicheza halaiki, tulicheza Chipukizi, tukiwa Sekondari tulicheza halaiki, and then tulienda JKT!

- Siku hizi ni kila mtu na lwake, ujitahidi mwenyewe tu ufike juu hamna matayarisho no wonder tunakuwa na viongozi wasiowakamilifu na itikadi tena wengi sana!



William.

Weye kweli umechoka au ndo kiwewe cha kushindwa ubunge A.Mashariki! kijana badilika,kama unawapenda watoto waandalie mazingira bora ya elimu sio hayo maigizo.
 
​
Kamanda James Mwakibinga, kada wa CCM akiwa na watoto wadogo huko Kawe, hii ndio moja ya njia muhimu sana ya kuimarisha chama chochote cha siasa, ni kuanzia kwa watoto wadogo.

- Huu ndio mfano wa kuigwa na chama chochote cha siasa iwe hapa au Duniani popote pale, hope CCM will take a note here, kwamba zamani Mwalimu Nyerere alifanya haya ya kufikisha chama kwa wananchi kwa kuanzia na watoto, tukiwa watoto tulicheza halaiki, tulicheza Chipukizi, tukiwa Sekondari tulicheza halaiki, and then tulienda JKT!

- Siku hizi ni kila mtu na lwake, ujitahidi mwenyewe tu ufike juu hamna matayarisho no wonder tunakuwa na viongozi wasiowakamilifu na itikadi tena wengi sana!



William.

Cha kuiga hapa ni nini mkuu, ni kupiga picha na watoto ama? Sijakusoma vizuri.
 
Back
Top Bottom