Mfano wa Kodi za Mitandao Amazon

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,603
8,743
Mimi ni diaspora hapa US state ya Texas na kwa hii miaka miwili nina nunua vitu vingi mitandaoni kwa kutumia Amazon. Kwasababu serikali inatafuta njia ya kutoza kodi za mitandao US ni mfano mzuri.

Hapa US kila jimbo lina kodi tofauti hivyo mimi hapa Texas nikinunua majani ya chai kodi yangu ni 8.25% wakati California kodi yake ni 7.25% hivyo nikitumia mtandao nikiwa California na Texas nitalipa kodi tofauti. Hivyo kinachotokea ni kwamba Amazon ina utaratibu na kila jimbo wa kulipa kodi kutokana na anwani yako hivyo Amazon inatuma 8.25% ya kodi kwa jimbo la Texas au California kutokana na mtu anapo ishi.

Hivyo kwa mfano wangu serikali haiwezi kutoza kodi moja kwa moja watu badala yake wanatakiwa waongee na Amazon, Alibaba, .... na mitandao yote ili iwape kodi ambayo wamekubaliana nayo kwa wananchi wa Tanzania. Bila makubaliano hii mitandao ya uuzaji haiwezi kujua kodi ni kiasi gani %X na hivyo hawatozi kodi na serikali haiwezi kwenda kuomba kodi ambayo haijatozwa.

Je, nchi nyingine zimefanyaje mitandao mikubwa ni ya US kuanzia Google, Facebook ambao ni wamiliki wa WhatApp, Apple, Uber.... karibu zote hivyo Jumuiya ya Ulaya iliingiza mikataba na hizi kampuni jinsi gani wananchi wao walipe kodi hivyo ushauri wangu ni kwamba Jumuia ya Africa Mashariki kwenye hili swala iende kwa hizi kampuni kama kitu kimoja hata kama kodi ni tofauti kama walivyofanya jumuia ya Ulaya.

Tanzania ikienda pekee haitakuwa na nguvu mfano Australia ilitaka Facebook waanze kulipa kodi kwenye habari za magazeti ya nchi hiyo na Facebook wakatoa mtandao wao kwa siku chache tu mkuu wa nchi ikabidi arudi kuwapigia magoti Facebook warudishe mtandao. Hivyo tusipokuwa pamoja Tanzania inataka kodi wakati majirani zetu kama Kenya, Uganda.... na wanajumuia wengine hawana shida na kodi hatutakuwa na nguvu ya kujadili hili swala kwa nguvu. Hiyo hili sio swala la wizara ya Fedha bali ni swala la jumuia ya Afrika mashariki na hivi ndivyo vitu jumuia ina manufaa.

Vilevile kuna mitandao ya bure mfano Youtube ya Google wanalipwa na matangazo. Hivyo mimi nikiangalia msanii watangazaji wanamlipa youtube halafu youtube wanalipa wasanii. Sasa hapa kama serikali ikitaka kodi ni kuongea na YouTube wakate kwenye ile pesa ambayo wangemlipa msanii maana ni masanii wa Tanzania lakini serikali hiyo hiyo haiwezi kwenda tena kwa msanii kibinafsi na kuomba kodi kwa pesa ambayo wamelipwa na youtube hii itakuwa ni kulipisha kodi mbili kwa pato moja. Kama kwa utaratibu wa sasa serikali haipati pesa ni rahisi huongea na youtube na kuweka utaratibu wa kulipwa kodi kwa mtu yeyote anaye ishi kwa sasa Tanzania.

Kwa Facebook na kampuni zake za whatapp na instagram ni ngumu serikali kupata kodi maana hii kampuni sio kama youtube au apple ambayo inalipa wasanii facebook hailipi mtu lakini inatoa hizi app zake bure na wenyewe wanapata pesa kwa watangazaji. Hakuna mtu anajua ukiangalia matangazo Facebook wanapata kiasi gani ni ngumu sana na hata hapa US bado ni tatizo na hakuna kodi kwenye Facebook, WhatApp au instagram. Hawa ni vichwa ngumu hawatalipa kirahisi na mfano ni Australia na huwezi kuzitoa hizi app kirahisi.

Hivyo Tanzania tunaweza kupata pesa za youtube na amazon lakini app nyingine ni ngumu sana
 
Tukianza na YouTube tutafika mbali sana kiuchumi.

#SiempreJMT
Tutafika mbali wapi mkuu ilihali hata wenyewe kwa wenyewe hawataki kukosoana?

Gwajima na Slaa ndio mfano tosha na huo mjadara wao ungemalizwa tu kwa wabunge kuchapisha mitandaoni salary slip zao na hata kama ni posho, ni ujinga wa hali ya juu sana wa hiyo posho kutokukatwa kodi.

Kila mtu na alipe kodi kwa fedha anazopewa iwe posho, mshahara au kiinuua mgongo.
 
Tutafika mbali wapi mkuu ilihali hata wenyewe kwa wenyewe hawataki kukosoana? Gwajima na Slaa ndio mfano tosha na huo mjadara wao ungemalizwa tu kwa wabunge kuchapisha mitandaoni salary slip zao na hata kama ni posho, ni ujinga wa hali ya juu sana wa hiyo posho kutokukatwa kodi...kila mtu na alipe kodi kwa fedha anazopewa iwe posho, mshahara au kiinuua mgongo.
Umeshawahi kuajiriwa?

Posho zako zilikuwa zinakatwa KODI ya P.A.Y.E?
 
Umeshawahi kuajiriwa?

Posho zako zilikuwa zinakatwa KODI ya P.A.Y.E?
Niko kazini hata sasa mkuu. Kila ninacholipa kodi hukatwa na hiyo PAYE inatumika ku- calculate ni posho gani nipewe...hakuna ninacho pewa cha bure bure hivi kwa majina tofauti tofauti, Mara posho, seating allowance, kiinua mgongo, yote hiyo ni mianya ya rushwa inayofaa kuzibwa kusheria na kufuatiliwa kwa ukaribu na TRA.
 
Niko kazini hata sasa mkuu... kila ninacholipa kodi hukatwa na hiyo PAYE inatumika ku- calculate ni posho gani nipewe, hakuna ninacho pewa cha bure bure hivi kwa majina tofauti tofauti... Mara posho, seating allowance, kiinua mgongo, yote hiyo ni mianya ya rushwa inayofaa kuzibwa kusheria na kufuatiliwa kwa ukaribu na TRA.
Hujanijibu mkuu wangu.

Je, posho zako zinakatwa kodi ya PAYE?

Kwa hiyo mbunge ambaye naye ameshapangiwa kiwango Cha posho kutokana na hizo "scales" unataka akatwe PAYE?
 
Hujanijibu mkuu wangu.

Je posho zako zinakatwa kodi ya PAYE?

Kwa hiyo mbunge ambaye naye ameshapangiwa kiwango Cha posho kutokana na hizo "scales" unataka akatwe PAYE?!!!
Majibu kwa maswali yote mawili ndugu Jumbe Brown ni Ndio.

rejea maana halisi ya PAYE... labda kama huijui ndio maswali yako yatakuwa na la ziada.

Chochote kinachoingia mfukoni kama fedha kwa njia yeyote ile lazima kiwe kimelipiwa kodi hata kabla ya muhusika kukipata, labda tuambiwe au tupewe sababu hasa za ku- justy hizo posho kutolipa ili hali muendesha bodaboda analipa
 
Pamoja na maelezo mengi, lakini si kweli Youtube, Facebook, na mashiriki mengine hayalipi kodi. YouTube, Instagram, WhatsApp, Facebook zinalipa kodi (corporate tax). Hizi zinalipa kodui kutokana na fedha.

Amazon na Ebay, Alibaba pia hulipa corporate taxes. Wanunuzi wa bidhaa kupitia mitandao nao hulipa kodi ambazo kama ulivyosema hukusanywa na wauzaji wa mitandao na kuziwasilisha kunakohusika. Kwa maana nyingine Tanzania au nchi nyingine zina haki kudai mitandao kama Facebook, Jamiiforums kama corporate tax.
 
Tueleze mf. wa nchi moja ya Afrika inayolipwa kodi na Instagram au Facebook na hiyo Kodi inalipwa kw mfumo gani.
Pamoja na maelezo mengi, lakini si kweli Youtube, Facebook, na mashiriki mengine hayalipi kodi. YouTube, Instagram, WhatsApp, Facebook zinalipa kodi (corporate tax). Hizi zinalipa kodui kutokana na fedha . Amazon na Ebay, Alibaba pia hulipa corporate taxes. Wanunuzi wa bidhaa kupitia mitandao nao hulipa kodi ambazo kama ulivyosema hukusanywa na wauzaji wa mitandao na kuziwasilisha kunakohusika. Kwa maana nyingine Tanzania au nchi nyingine zina haki kudai mitandao kama Facebook, Jamiiforums kama corporate tax.
 
Tutafika mbali wapi mkuu ilihali hata wenyewe kwa wenyewe hawataki kukosoana?

Gwajima na Slaa ndio mfano tosha na huo mjadara wao ungemalizwa tu kwa wabunge kuchapisha mitandaoni salary slip zao na hata kama ni posho, ni ujinga wa hali ya juu sana wa hiyo posho kutokukatwa kodi.

Kila mtu na alipe kodi kwa fedha anazopewa iwe posho, mshahara au kiinuua mgongo.
Tuweke utamaduni wa kulalamika. Huu ni wito maana ukilalamika kila wakati hata utamaduni wako wa binafsi unabadilika. Kwenye maisha haya unatakiwa kuwa positive sana. Ukiwa mlalamishi bila kujua wewe ni tatizo vilevile huu ni ushauri tu
 
Tutafika mbali wapi mkuu ilihali hata wenyewe kwa wenyewe hawataki kukosoana?

Gwajima na Slaa ndio mfano tosha na huo mjadara wao ungemalizwa tu kwa wabunge kuchapisha mitandaoni salary slip zao na hata kama ni posho, ni ujinga wa hali ya juu sana wa hiyo posho kutokukatwa kodi.

Kila mtu na alipe kodi kwa fedha anazopewa iwe posho, mshahara au kiinuua mgongo.
Slaa yupo Sawa ila hakujipanga. Alisahau kuwaeleza kuwa posho zao hazikatwi kodi wakati wafanyakazi katika private sector posho zao zinajumuishwa katika mishahara na kukatwa PAYE. Wao wanakatwa PAYE ya mishahara tu. Aidha per diem zao zinatakiwa kukatwa 10% iwapo hawatarejesha receipt za matumizi yake.
 
Back
Top Bottom