a sinner saved by Christ
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 1,966
- 2,200
- Wote Mrema na Polepole walijiuzulu kutoka nafasi zao za juu ndani ya chama na serikali.
- Wote baada ya kujiuzulu nafasi zao ndani ya chama na serikali wakawa wakosoaji wakuu wa chama na serikali hiyo hiyo waliyokuwa wanafanya kazi awali.
- Wote Mrema na Polepole wakateka hisia za wananchi wanyonge, wakajijengea trust, kuaminiwa, wakaonekana kama wakombozi na tumaini jipya la kutuvusha, kuleta mageuzi na ukombozi wa wananchi wanyonge.
- Wote Mrema na Polepole wakapendwa sana na kuaminiwa sana, na kupelekea kuanza kupewa taarifa za siri kutoka kwa whistleblowers, yani baadhi ya watumishi wa chama na serikali wakaanza kuwaamini na kuwapa siri za serikali kwa kuwaona kama wakombozi wa wanyonge.
- Wote Mrema na Polepole walionyesha kuwa na uchungu na inji hii na kuonyesha nia ya dhati ya kuikomboa kutoka kwenye wizi.
Ambacho wengi hawakukijua kuhusu Mrema
- Mrema alikuwa kazi maalumu. Pamoja na upinzani aliouonyesha na ukosoaji aliouonyesha, lakini ilikuwa ni maigizo kwa kazi maalumu.
- Wafuasi wake walipoteza muda wao, mali zao na hata kuhatarisha maisha yao katika harakati za kampeni usiku na mchana, kwenye jua na mvua, pori kwa pori, milima na mabonde kuhakikisha NCCR Mageuzi na ukombozi unapatikana kutoka kwa mafisadi. Kumbe Mrema mwenyewe anawachora tu.
- Katika siasa za vyama vingi na upinzani inji hii, kipindi hicho waliokuwepo watakumbuka upinzani wa Mrema kupitia NCCR Mageuzi. Mrema alikuwa na sera nzuri sana, ushawishi mkubwa na mvuto mkubwa sana. Alionekana ndiye mkombozi wa wanyonge, na sera pamoja na ushawishi na style aliyokuwa nayo Mrema inafanana sana sana na hii aliyonayo sasa Polepole.