Mfanano halisi

Abuu Dharr

JF-Expert Member
Dec 28, 2017
2,898
3,006
WAOVU HUFANANA

Tuseme tu ukweli,waovu hufanana mpaka sura zao,harufu zao,rangi zao,tabia zao

Waovu,hujuana/hufahamiana wao kwa wao
Hata kama hawajawahi kukutana

Nyoyo za Binaadamu,zinawasiliana na kutafutana

Muovu humtafuta muovu mwenzake,na hakuna kinyume chake

Hata siku moja,muovu,hamtaki mwema,na wala hawezi kukaa nae,ni nadra sana

Kawaida yao,kupeana maneno mazuri baina yao,na hupendezeshana kila jambo lao

Maisha yao,yanaendeshwa na uongo mwingi na matamanio.

Wazinzi huitana na kuambizana kwa pmj
Walevi kadhalika
na mfanowe

Ndege wa rangi moja,huruka kwa pamoja

Ila ipo siku itafika.

Hayakuwa maisha haya ya Dunia,isipokuwa ni udanganyifu tu.
 
Mkuu unataka kufa?
mbona umeandika kama wosia?
pia binafsi sijaelewa chochote..
 
Back
Top Bottom