Mfalme Zumaridi, Kipimo kingine cha imani na mtihani mwingine kwa mamlaka

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,845
Unaweza kuamini kuwa kuna mtu anakamatwa kwa makosa fulani halafu kwa mujibu wa sheria dhamana yake inakuwa wazi lakini anagoma kudhaminiwa kwa sababu zenye kushangaza? Wafuasi wa Mfalme Zumaridi walioko mahabusu kwa makosa waliyokutwa nayo wamegoma kudhaminiwa wanataka wabaki na kiongozi wao mahabusu.. Hiki ni kipimo cha imani

Nahitaji mno kuijua historia ya mwanamama Diana Bundala amaarufu kama Mfalme Zumaridi.. Ni wazi huyu ni kati ya wale watoto wanaozaliwa wakiwa na mambo ambayo si ya kawaida ama alikuja kuyapata baadae ukubwani

Ni mmojawapo wa watu wachache kwa uwingi wao duniani wenye kipaji cha mvuto na ushawishi...wengine wakichanganya na nguvu za giza za kutafuta kwa waganga wa kienyeji na ushirikina

Diana Bundala Zumaridi ni kundi moja na hawa mitume na manabii wetu Tanzania na sehemu zinginezo duniani.. Ni aina ya watu wenye ushawishi wa ajabu na wenye kutia shaka mno kwakuwa huwatia upofu fulani wafuasi wao na kuwaaminisha mambo yasiyowezekana ama kuwaamrisha wafanye watakavyo nao bila maswali wakafanya

Tumeshuhudia ya Kibwetere

Tumeshuhudia ya Gwajima

Tumeshuhudia ya Applewhite wa ufaransa

Na wengine wengi waliowaletea madhara makubwa viumbe wasio na hatia

Hii ni dunia ya mapepo ambao ni sehemu ya viumbe roho lukuki.. Makazi salama ya mapepo ni kwenye miili ya watu..huko kwingine kumejaa mahangaiko na mateso.. Hivyo ili kujihakikishia usalama inabidi yajitengenezee ufalme wao katikati ya wanadamu na wawatumie wapendavyo.. Kama huamini hili hebu angalia mifano hii michache

Inawezekanaje mtu akwambie umeze JIK ili usafishe dhambi ndani ya mwili nawe ukubali? Hii ilipata kutokea Malawi au South nadhani
Inawezekana vipi mtu akwambie ule nyasi kama chakula cha asili nawe ukubali? Hii iliapata kutokea Afrika kusini

Inawezekana vp mtu akwambie mjifunge maputo halafu mpande mitini mjiachie nawe ukubali? Hii ilipata kutokea hapo Kenya
Visanga ni vingi sana hasa vya ngono ili kupata wachumba ama watoto, kulishwa uchafu wa maniii na uchafu wa ukeni kupitia maji yaitwayo ya baraka ni vitu vya kawaida kabisa

Mfalme Zumaridi ni mwanamke si mwanaume.. Tumejaribu kuhoji kidogo hili lakini tukaishia kuambiwa mbona kuna chifu hangaya mwanamke? Huyu mama ni kipimo tenge kwenye utawala huu wa awamu ya sita .. Namna gani unaweza kushughilikia na mambo ya kiimani.... Akili kubwa? Ubobevu wa hekima ujuzi na maarifa ama maguvu na kulazimisha?

Diana Bundala almaarufu Mfalme Zumaridi amadakwa si kwa kuchelewa sana.. Lakini tayari ana wafuasi watiifu wanaomuamini sana ambao wako tayari kufanya lolote atakalowaambia..!

Kwake kuwekwa mahabusu ni milestone credit.. Kwa kukaa kwake lupango anayatumia maandiko vibaya kwamba yeye si nabii mungu wa kwanza kuwekwa gerezani na hatakuwa wa mwisho..!

Kushughulika na swala lake hakuhitaji hawa walinda usalama wetu wazee wa kulazimisha mambo bali watu wenye upeo na elimu ya maswala maswala ya kiroho kisaikolojia .

Vitu vingine ni mauzauza ya kiroho(spiritual hallucinations) na wao haya mazonge yao huyajengea Uhalisia na kuwaaminisha wengine kuwa huo ndio ukweli

Kuna ambao hayo mauzauza huwafanya wajione mioyoni mwao wao ni miungu
Kuna ambao huwafanya wajione wao ni aina fulani ya wanyama katika umbo la binadamu na ndio maana hujapachika nayo majina
Fikra huumba.. Na kugeuza uhalisia kuwa bayana! Lakini ni mpaka hizo fikra zijirudie mara nyingi.. Kwassasa Diana anajiona kabisa yeye ni mungu

Fikra zake hizo zimealika mapepo na kumpa nguvu kubwa...angalia ibada zake angalia cheza yake vaa yake nknk.. Vimejaa mapambo na rangi kali, kelele na sauti kubwa.,!

Mapepo hawapendi utulivu, mapepo hawapendi ukimya.. Na ndio maana makanisa mengi ya manabiii na mitume yamejaa kelele na mihemko mbalimbali tofauti kabisa na watu wanaofanya meditation ama wanaofanya ibada zao kwa ukimya na utulivu
 
Hivi mtani kalumanzila kwani huyo mwanamama amekamatwa kwa sababu ya Imani yake?

Je jicho lako la kitaalamu linasemaje kuhusu Imani ya huyo mama na wafuasi wake?
 
Kweli kukaa lupango ni boost kubwa kwake hta lupango wangempa uhuru angeazisha kanisa huko huko na askari wangekua wafuasi ni basi tu jicho la tatu linamtazama.
 
Nikweli hili swala linafikirisha sana kiasi kwamba unjiuliza maswali mengi yasiyo na majibu mfano aliawaza nini mpaka akaamua kujiita yeye ni mungu wakati anajua wazi amezaliwa na ana wazazi hapa duniani je analizungumziaje jambo hili!?
 
Wamuachie Mungu chini ya Jua Mfalme Zumaridi afanye kazi yake ya kuhubiri dini.
Screenshot_20220309-143355.jpg
 
Linaweza kubadilishwa na kuwa kusanyiko bila kibali japo nalo limejaa makengeza..na kutumikisha watoto pia limewekwa
Kusanyiko bila kibali ndani ya kanisa?

Hii inchi ina watu wa hovyo sn.
Wanamuonea bure dada wa watu.

Kama ni makanisa yapo mengi huko mitaani.
Kama kosa ni kusema yeye Mungu kuna ubaya gn?

Mbn wahindi wanasema ng'ombe Mungu na hawakamatwi?
Sasa ng'ombe na mwanadamu Nani ana ufahamu?
 
Kusanyiko bila kubali ndani ya kanisa?

Hii inchi ina watu wa hovyo sn.
Wanamuonea bure dada wa watu.

Kama ni makanisa yapo mengi huko mitaani.
Kama kosa ni kusema yeye Mungu kuna ubaya gn?

Mbn wahindi wanasema ng'ombe Mungu na hawakamatwi?
Sasa ng'ombe na mwanadamu Nani ana ufahamu?
Umeruka kwenye swala la kutumikisha watoto kinyume na sheria, umerukia kwenye swala la mungu ng'ombe wa wahindi. Au na ww ni mmoja wa wanufaika wa hayo mazingaombwe?
Linaweza kubadilishwa na kuwa kusanyiko bila kibali japo nalo limejaa makengeza..na kutumikisha watoto pia limewekwa
 
Back
Top Bottom