Aliyewahi kufika Mbinguni aje amkosoe Mfalme Zumaridi

master of cities

JF-Expert Member
Mar 14, 2015
429
620
Ieleweke kwanza Tanzania haina dini ila watu wake wana dini zao, na kila mmoja ana uhuru wa kuabudu cha msingi asivunje sheria za nchi.

Duniani hapa kuna dini zaidi ya 4000, ikiwemo dini ya Kikristo.

IMG_20230321_230441.jpg

Katika dini ya Kikristo pekee kuna madhehebu zaidi ya 500 hawa hudai kumwabudu Mungu wa mbinguni na mwongozo wao ni kitabu kinachoitwa Biblia na kila dhehebu linatafasri Biblia kivyake na cha kushangaza zaidi madhehebu haya yote hayapatani.

Japo Biblia yenyewe inasema Mungu mmoja na imani moja, sasa imami zaidi ya 500 how comes? Na wote wanafokeana na kusontesheana vidole, na kamwe Mungu hajawahi kushuka na kutangaza hadharani kuwa dhehebu fulani au dini fulani ndio sahihi.

Wote wanajiendea tu na kujitumainisha kwenye vaccum, no body cares sababu masuala ya dini ni masuala yasiyo na udhibitisho wa kisayansi, hvyo ni myth story zinazohusisha imani.

Mfalme Zumaridi yeye pia ana dini yake na wafuasi wake, yupo vizur kimaslahi na wafuasi wake humtii Mfalme huyu, na yeye huitafasri Biblia anavyojua yeye, na kutoa masimulizi anayoyajua yeye na wafuasi wake humtii. Yawe ya uongo au ya ukweli, awe ni kichaa au ana akili timamu still ana haki ya kuamini anachoamini, Mfalme Zumaridi hugawa chakula na pesa na wanazengo humfata Mfalme wao.

Juzi millard ayo kasafiri mpaka Mwanza kwenye jumba la Kifalme la Zumaridi, akamhoji Zumaridi naye akaelezea yaliyo moyoni mwake kulingana na imani yake.

Inashangaza watu wanaotafasiri Biblia kwa mlengo wao wanakuja kumshambulia mtu anayefasiri Biblia kwa mlengo wake, aisee ni upumbavu wa hali ya juu.

Kuna wachungaji walishasema wao wanaweza kufufua wafu, kuna wengine wanauza mafuta sijui ya upako, wengine mitume wanadai wameoteshwa yaani ni story tu za kihuni huni, wengine wana vitambaa yaani ni vurugu tupu, leo kwa Zumaridi imekuwa nongwa?

TCRA na wao wanaacha majukumu yao wananchi wanaibiwa vifurushi, wizi wa kimtandao umetawala wanahangaika na hizi myth story za kufkrika za akina Zumaridi.

Basi aliyewahi kufika mbinguni aje amkosoe Mfalme Zumaridi, aje yeye atuelezee kwa usahihi mbinguni kukoje hasa, vinginevyo tunapotezeana mda tuu!

IMG_20230321_232754.jpg
 
Back
Top Bottom