Kinyonyoke
JF-Expert Member
- Oct 4, 2016
- 3,498
- 13,141
HAPO kale palikuwapo na dola kubwa. Mfalme wa dola hiyo, alikuwa na mguu moja na jicho moja. Siku moja mfalme akizungukia makumbusho yaliyomo ndani ya kasri la kifalme, alikutana na michoro ya picha za babu zake. Baada ya kufurahia uzuri wa michoro ile, fikra ikamjia kwamba, miaka mingi ijayo wajukuu zake nao watazulu mahala hapo, lakini hawatokuta mchoro wake.
Mfalme hakupata kuruhusu kuchorwa, kwa sababu hakuwa na hakika kama angelitokea mchoraji mahiri ambaye, angelimchora vizuri licha ya mapungufu yake kimwili. Kutokana na umuhimu wa kumbukumbu, hatimaye mfalme aliwaalika wachoraji mahiri na mashuhuri. Walipofika, akawatangazia hitaji lake la kuchorwa picha nzuri kwa ajili ya kuihifadhi kwenye makumbusho - na kwamba, mchoraji atakayebeba dhima hiyo, atalipwa kwa kadri ya kazi yake.
Minong'ono ikazizima baina ya wachoraji - hofu ikitamalaki nyoyoni mwao. Kila mmoja aliihofia nakama itakayomkumba endapo ataitwaa fursa hiyo. Kumchora mfalme akiwa na mguu na jicho moja, japo ndiyo uhalisia wake, ni sawa na kumdhalilisha. Vivyo hivyo, kumchora akiwa na miguu miwili na macho mawili ilhali sivyo alivyo, ni kama kumdhihaki na kumsanifu - kitu ambacho kitatishia uhai wa atakayechora. Kwa hivi, mchoraji mmoja baada ya mwingine alitoa udhuru.
Katika hali ya kushangaza, mchoraji mmoja alinyoosha kidole na kukubali jukumu la kumchora mfalme. Mfalme alifurahi ilhali wachoraji wengine wakistaajabia maamuzi ya mwenzao. Basi, baada ya ruhusa rasmi, mchoraji alianza kazi yake kwa umahiri na ustadi mkubwa. Hatimaye akaimaliza kwa wakati.
Wachoraji, watumishi wa mfalme, wageni waalikwa, nk. walijawa shauku ya kutaka kuona maamuzi atakayochukua mfalme dhidi ya mchoraji mara baada ya mchoro kufunuliwa. Muda ulipofika, mchoro ukafunuliwa. Kila mmoja alipigwa butwaa - akistaajabia alichokiona.
Mfalme alichorwa akiwa amepanda farasi - huku upande ule wenye mguu moja ndio wenye kuonekana ilhali ule mwingine akifichwa upande wa pili wa farasi. Mkononi mfalme alishika upinde huku lile jicho bovu, akilifumba kama anayetafuta shabaha ya kurusha mshale uliopachikwa kwenye upinde.
Watu wote walishangilia. Mfalme alifurahi sana kwa namna mchoraji alivyotumia sanaa pamoja na hekima kubwa kuficha mapungufu yake. Akamzawadia mchoraji tuzo yenye thamani na heshima kubwa. Mchoraji alichowazidi wenziye si umahiri wa uchoraji, bali kuliona jambo bora - na kulitumia kuuficha udhaifu.JIFUNZE.