Mfalme Mgonjwa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mfalme Mgonjwa...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Sep 23, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Sep 23, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  KUNA tunaokumbuka kisa cha mfalme simba na wanyama wenzake. Mfalme simba alipatwa na ugonjwa. Akabaki kibandani asiweze kutembea. Na njaa nayo ikamshika. Wanyama wengi walimtembelea mfalme kumjulia hali. Walikwenda akina pundamilia, twiga, swala na wengineo. Kila aliyeingia kibandani kwa mfalme hakutoka nje.

  Mfalme simba katika kiu yake ya nyama akamtamani sana kobe. Ni kobe katika wanyama wote ambaye hakuonekana katika nyumba ya mfalme simba kumjulia hali. Simba akatuma ujumbe akilalamika; "Enenda ukamwambie kobe, nashangaa katika kuugua kwangu sijamwona kuja kunijulia hali"!

  Ujumbe ukamfikia kobe. Siku moja kobe naye akaenda kumjulia hali mfalme simba. Hakufika mpaka iliko nyumba ya mfalme simba. Alisimama mbali na kutamka: "Ewe mfalme wangu simba, nimekuja kukujulia hali, waendeleaje na afya yako?".

  Mfalme simba akajibu: "Mbona salamu hizo unazitoa ukiwa mbali hivyo?". Kobe akamjibu mfalme wake: " Kuna jambo linanishangaza mfalme wangu, naona nyayo zote za wanyama zimeelekea kwako, lakini hakuna nyayo zinazorudi"!

  Katika jamii yetu sasa kuna akina mfalme simba wagonjwa na wenye njaa ya nyama. Wamewatafuna twiga, swala, pundamilia na wengineo. Sasa wanawatamani akina kobe pia!
  Ndio, katika nchi yetu sasa kuna harakati za kimakundi. Tunaziona ndani ya chama tawala, tunaziona nje ya chama hicho. Kuna wenye kuongoza harakati hizo.

  Na Watanzania tulio wengi tumekuwa ni watu wa kupenda sana kutafuna maneno. Kuna mawili makubwa ambayo ni mapungufu yetu; mosi, hatuna misimamo, pili, tukiwa nayo hatuisimamii.

  Tunapenda sana kuzungumza tusichomaanisha na mara nyingi hatumaanishi tunachozungumza. Na Mtanzania haumizi kichwa kujiuliza; " kwanini nizungumze". Maana suala si unachozungumza, bali ni kwanini unazungumza.

  Na kwanini wananchi wanaonekana kukata tamaa na kukosa imani kwa kinachozungumzwa na viongozi wao. Ndio, kikubwa kinachokosekana hapa ni namna nzuri ya kuwasiliana na wananchi ili kuwafahamisha na labda kuwaelimisha juu ya kilichotokea.

  Watanzania wengi hawana taarifa muhimu kuweza kutafsiri matukio na kinachozungumzwa na viongozi wao. Ni ukweli kuwa Watanzania walio wengi wanaishi vijijini. Ni takribani asilimia 21 tu ya Watanzania wenye fursa ya kupata taarifa muhimu juu ya kinachoendelea katika nchi yao; ni kupitia magazeti, runinga na redio. Waliobaki asilimia sabini na tisa ya Watanzania ndio hao wa Manzese Dar es Salaam, Mwanjelwa Mbeya, Kihesa na Kilolo Iringa na kwingineko.

  Ni hawa wasio na taarifa za kutosha kutafsiri mambo na hata kufanya maamuzi yanayotokana na kuwa na taarifa (informed decisions). Ni asilimia 79 hii ya Wanzania wa Mwanjelwa , Kilolo na kwingineko wenye kuiweka Serikali madarakani kwa wingi wa kura zao.
  Media, kwa maana ya ya wanahabari ndio walipaswa wajitoe kwenye vita vya kimakundi na kuwasaidia Watanzania hawa kupata taarifa zitakazowawezesha kufanya maamuzi sahihi.

  Lakini miongoni mwa wanahabari hawa, kuna walioingia katika foleni ya kwenda kuwajulia hali wafalme wagonjwa. Wamejiingiza kwenye vita ya kimakundi. Wamelisahau jukumu lao, wamelisahau kundi kuu. Ni kundi lile la asilimia 79 ya Watanzania.

  Tunaziona nyayo za baadhi ya wanahabari zikienda kwa wafalme wagonjwa, hatuzioni nyayo zao za kurudia!
  Wanahabari walipaswa kuwa daraja la kupitisha taarifa kutoka chini kwa wananchi kwenda juu kwa viongozi, na kinyume chake.

  Lakini, miongoni mwa wanahabari hao, wameamua kwa makusudi kulivunja daraja hilo. Ni kweli kuwa kila mwanadamu kwa namna moja au nyingine ananunulika, lakini kwa wengine, bei zao ni utu na heshima, basi. Wanasukumwa kufanya yale yenye maslahi mapana kwa taifa.

  Na hilo ni Neno La Leo. ( Limechapwa pia kwenye Mwananchi, leo Jumapili)
  Maggid,
  Iringa
   
 2. mukizahp2

  mukizahp2 JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2012
  Joined: Jul 28, 2012
  Messages: 635
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Mtazamo wangu ...wewe mwenyewe mjengwa umekwenda kumuona mfalme mgojwa na haukurudi,yaani hiyo habari yako ni nzuri sana, na unajiongelea wewe mwenyewe na wanahabari wenzako wachache mlioamua kuasi makubaliano ya wanahabari wenzenu,wanahabari wa iringa waliamua hakuna kuandika habari za polisi ..

  Ila wewe ukaona lazima uandike,najua uliongoza harambee ya mchango kwa marehemu mwangosi lakini ulitakiwa kufuata maamuzi ya wanahabari wenzako...wewe na michuzi ni wasaliti
   
 3. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Divide and rule worked...
   
 4. we gule

  we gule Senior Member

  #4
  Sep 23, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ila naamini kwa kadiri siku zinvyokwenda Watanzania wanaanza kubadilika kidogokidogo ,kwani hiyo asilimia kidogo amabayo inapata hizo taarifa watakuwa nichachu ya kwa hao wengine .

  Ni ukweli haupingiki katika ufukara na umasikini uliopo sio rahisi jamii kuielimisha ,kuihabarisha mabadiliko yanayotokea na kuwafikia kwa wakati muafaka kwani kila siku kukicha watu wapo kwenye mihangaiko ya kutafuta ka ugali kao na wanaowazunguka.

  Leo hii fanya utafiti kidogo tu pale Kariakoo uliza maswali rahisi tu; hivi jana ITV Kulikuwa na taarifa gani muhimu au Gazeti za jana kulikuwa na habari gani kuu au Muulize Mkuu wa mkoa wa Katavi ninani na tumaini huwezi kupata jibu lolote sasa katatika mazingira kama hayo hao wapo mjini, vipi mwanakijiji aliyepo Nyagwijima Kibondo, aliyepo Mambali Nzega, aliyepo Namanyele Rukwa awe na taaarifa ?

  Bado kuna kazi kubwa inahahitajika kwanza kuondoa Umasikini halafu Ujinga na mengine yatafuata.
   
 5. Root

  Root JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,146
  Likes Received: 12,853
  Trophy Points: 280
  wanatafunwa kwa tamaa zao wenyewe au bila kujua
   
 6. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,743
  Likes Received: 6,018
  Trophy Points: 280
  Bora mfalme simba yeye alikuwa anawala jumla tena ni lishe aliyoandikiwa na mola wake!

  Lifalme letu la leo (mfumo) linakamata, linabaka na kujeruhi vibaya, linaua, na hatimaye linaacha maiti porini ikiliwa na kunguru, fisi, na ndege mwitu.

  Maumivi, fedheha, udhalilishaji, na kila aina ya aibu.
   
 7. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Pia hii hadith inamfaa na 6, kapiga kelele ya mwakyembe, ya ufisadi, na wengine ila yeye yupo mbio sana, kaja CDM amani haijamjia, afadhali hata kobe kuliko 6.
   
 8. m

  majebere JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  hizi hadithi za simba na sungura ndio zililaza akili ya wantanzania.
   
 9. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,586
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Mambo haya si katika habari bali hata fani zingine pia. Angalia madaktari,kugoma,kuomba msamaha na wengine kupinga msamaha.Hapo mfalme Simba anajichukulia ki ulaini.
   
 10. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #10
  Sep 23, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Usaliti Usalitini.........
   
 11. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  naona umeanza kupuliza
   
 12. Chum Chang

  Chum Chang JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,001
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  kuna hoja imewekwa kuh unafiki wa waandishi.maggid kaka unachoandika sicho unachomanisha

  kwanza toa boliti kwenye jicho lako ndipo uwaangalie watanzania jamani maggid si aliwahi kuweka tangazo la kuomba kazi na akaweka historia yake moja ya mambo yanayonishangaza ni lile tangazo ya kuwa yeye ni mswidi.....

  Sasa sijui kama ni mtz au muiringa na la mwisho amemsaliti mwangosi japo anachangisha pesa kwa yule mjane hali anawalamba miguu maafande kwa kuwapamba kwenye blog yake
   
 13. peri

  peri JF-Expert Member

  #13
  Sep 23, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  maggid umetoa ujumbe mzuri sana ila ni watu wachache sana ambao wanakuelewa/watakuelewa ulichoandika.
  Wengi ni wagonjwa tayari, makundi yanawatafuna mpaka wanashindwa kutumia akili zao kutafsiri mambo wanataka watafsiriwe na watu wanaowaamini na kuwapenda.
  Wanaogopa kutofautiana nao ndiomana hawataki kufikiri kwa akili zao bali wanataka wasaidiwe kufikiri.
   
 14. m

  maggid Verified User

  #14
  Sep 23, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Chung Chang,

  Unachosema hapa ni uongo mtupu ulioutunga bila aibu. Sijawahi kuweka mahali popote tangazo la mimi kuomba kazi na kuwa mimi ni Mswidi. Mara nyingi uongo kama huu ukiachwa kuna watakaodhani ni ukweli. Na kama ni muungwana unapaswa kuniomba radhi kwa kunitungia uongo bila aibu.

  Maggid
   
 15. Chum Chang

  Chum Chang JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,001
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Uongo wa nini na post uliweka wewe mwenyewe
   
 16. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #16
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,520
  Likes Received: 10,438
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii rangi inaumiza macho,wengine hatuna miwani maalumu.!
   
 17. a

  afwe JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Maggid, well written!
   
 18. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ni kweli ameandika vizuri hadi kuainisha cha kufanyika.

  1. Mkakati una mapungufu kwa sababu watekelezaji ni hao hao wanaokwenda kumjulia hali mfalme bia kurejea.

  2. Kwenye zama hizi si kweli 79% hawahabarishwi na vyombo vya habari; kuna watu wanaowafikia wananchi vijijini kuwaelimisha and they make a difference eg M4C.

  3. Sikuipata vizuri role(nafasi) yako ya kujikwamua na mfalme simba, natumaini kuna mkakati

  Ila nashauri tujumuishwe wote kwenye kumpa sumu ale afe.
   
 19. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #19
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,552
  Likes Received: 1,898
  Trophy Points: 280
  Wewe kwani ulienda kwa simba ndo ukarudi na michango ya msiba badala ya kupigania haki ya waliyoliwa na simba?
   
 20. Aggrey86

  Aggrey86 JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 856
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hii rangi mkuu wengine tumeshindwa kusoma inaumiza sana!
   
Loading...