Mfalme Mgonjwa...

Maggid, Well written. Hata kama wengi hatutapenda kushambuliwa ukweli unabaki palepale!
 
Natumai siku nyingine maggid utaandika kwa kina kwa nini "hao wanyama wanaendelea kumjulia hali mgonjwa'".Kwa hilo huenda tukapata njia ya kupata suluhisho
 
Last edited by a moderator:
Maggid,

Mwandishi wa hii article hapa chini ni mmoja kati ya wale walioliwa na yule simba anayejulika kwa jina la CCM. Na dhahma hii ilitokea kipindi kile cha uchaguzi mwaka 2010.

"Mti Mmoja Mrefu Haufanyi Msitu!

“ One tall tree does not make a jungle”- Nelson Mandela.
Hakika, na mimi naamini, kuwa Chama cha kisiasa chenye nguvu kinatokana na kazi ya timu iliyoandaliwa vema. Na si mtu mmoja.

Tujiulize; Je, chama cha siasa ni nini? Katika harakati za kisiasa kuna aina mbili za vyama; Chama cha Ukombozi na Chama cha Uongozi. TANU, FRELIMO, ANC ni mifano ya vyama vya ukombozi vilivyokuja kugeuka kuwa vyama vya uongozi. CCM, CUF, CHADEMA ni mifano michache ya vyama vya uongozi.

Chama imara cha ukombozi kinatakiwa kijenge uwezo wa kuwa chama cha uongozi mara ile kitapotwaa madaraka. Hufanya hivyo kwa kuweka mkazo juu ya mafunzo kwa makada wake. TANU, FRELIMO na ANC viliweza kujenga uwezo huo. Kielelezo cha nguvu na umakini wa chama cha kisiasa ni uwingi na ubora wa makada wake. Chama ni makada kwa vile chama ni itikadi, malengo na shabaha na wala si nasaba na umaarufu wa mtu mmoja mmoja ndani ya chama.

Chama chenye makada wengi wenye kuielewa itikadi, malengo na shabaha ya chama, huwa hakimtegemei mtu mmoja katika kuwepo kwake. Hakimtegemei mtu mmoja katika kufanikisha ushindi wa chama. Hakimtegemei mtu mmoja katika kuhamasisha wanachama au umma. Chama hicho hujiamini. Edward Mondlane, kiongozi wa kwanza wa Frelimo alipouawa kwa bomu la barua, Frelimo walijua watafanya nini, walijua mchakato gani utumike katika kumpata mrithi wake. Na hata Samora Machel, alipotoweka ghafla kwa ajali ya ndege, FRELIMO walijua watafanya nini.

Na kama Nyerere angekufa wakati wa TANU, bila shaka, TANU walikuwa wamejindaa vema na cha kufanya. TANU haikuwa na ukame wa jeshi la makada. Nguvu ya Frelimo kama ilivyokuwa kwa TANU zilikuwa ni makada wake. Na ieleweke, kuwa makada ni roho ya chama. Chama kikianza kupungukiwa na idadi ya makada wake wakereketwa, basi, chama hicho hakina mustakabali ulio salama, kitayumba, kitaangukia kaburini.

Kuna mfano wa chama kisichokuwa na nguvu ya makada. Wakati John Garang wa SPLM alipouawa kwa ajali ya ndege, hakuna ndani ya SPLM aliyekuwa na hakika ya nini kifanyike. Kwamba ni mke na mtoto wa John Garang waliosimama mbele ya kamera za waandishi wa kimataifa kujaribu kuelekeza nini John Garang angependa kifanyike kilidhihirisha udhaifu wa SPLM. Kwamba SPLM ni John Garang na kinyume chake. SPLM ilikuwa ni chama mtu. Na hilo ni Neno La Leo.


Maggid,
Msamvu, Morogoro "
 
Usimsifie huyu si mfalme, bali mwuaji. Damu ya Mwangosi itamteketeza yeye, familia yake yote hadi kizazi chake. Huwezi kuuwa raia wasio na hatia kiasi hicho halafu unawachekea eti wewe ni mtawala wao. Usimwambie kwa mafumbo, kwani hana akili ya kupambanua mafumbo. Mwambie tu ukweli watanzania wameshamchoka kama nguo ya ndani!
 
Back
Top Bottom