TANZIA Mfalme Harald V wa Norway afariki akiwa na umri wa miaka 89

TANZIA Mfalme Harald V wa Norway afariki akiwa na umri wa miaka 89

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,171
Reaction score
3,680
Mfalme Harald V wa Norway amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 89, baada ya kulazwa hospitalini wiki iliyopita kwa matibabu ya ugonjwa nadra wa damu.

Ikulu ya Oslo imesema mfalme huyo alifariki kwa amani saa 06:35 kwa saa za eneo (04:35 GMT) siku ya Ijumaa katika Hospitali ya Taifa ya Oslo.

Harald alikuwa mfalme wa kwanza wa Norway kuzaliwa nchini humo tangu karne ya 14. Atarithiwa na mwanawe, Mwanamfalme Haakon.

Baada ya kutawala kwa miaka 35, Harald atakumbukwa kama mfalme aliyependwa na wananchi na aliyefanya mageuzi yaliyosaidia kuibadilisha na kuifanya familia ya kifalme iendane na nyakati za sasa.

Pia alivunja baadhi ya mila za kifalme alipomuoa mwanamke wa kawaida asiye wa familia ya kifalme, na alijulikana kama kiongozi aliyekuwaunganisha wananchi wakati wa nyakati ngumu zaidi za Norway.

Soma pia Mfalme Harald V wa Norway, alazwa Hospitalini akiwa na hali mbaya kiafya

1787900003062.png

King Harald V

===============

Norway's King Harald V has died at the age of 89, after he was taken to hospital last week for treatment for a rare blood condition.

The palace in Oslo said he passed away peacefully at 06:35 local time (04:35GMT) on Friday at the national hospital in Oslo.

In the 24 hours leading up to his death, members of the royal family had visited the king, and crowds had laid flowers at the palace.

Harald was Norway's first king born in Norway since the 14th Century. He will be succeeded by his son Haakon.

After 35 years on the throne, he will be remembered as a popular and reforming figure who modernised the monarchy, broke with tradition by marrying a commoner and served as a unifying figure at Norway's most difficult moments.

Royal observers say he was down-to-earth, respected and beloved, describing him as a "grandfather" of the nation and the "People's king" - a title also used by his father King Olav V.

Source: BBC
 
Kuna watu wengine wanatamani tuwe na utawala kama wa kifalme hivi ambapo eti rais anatawala hadi mauti yanamkuta na kwa mtizamo wao sijui akifa anamuachia nani urais kwa Afrika hii ni ngumu sana kutokana na hulka ya waafrika kwani huyo rais na wapambe wake watakuwa na utajiri wa kufuru huku wananchi wake wakitafuta mabaki ya vyakula kwenye dampo la huyo "rais".
 
Mfalme Harald V wa Norway amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Ijumaa Agosti 28, 2026 akiwa na umri wa miaka 89, baada ya kulitumikia taifa hilo kama mfalme kwa zaidi ya miaka 35.

Kifo cha Mfalme Harald kimefungua ukurasa mpya katika uongozi wa kifalme wa Norway, ambapo mwanawe, Haakon, amechukua nafasi hiyo na kuwa mfalme mpya wa nchi hiyo.

Haakon ametawazwa kwa jina la Mfalme Haakon VIII, akimrithi baba yake aliyekuwa akiongoza ufalme huo tangu mwaka 1991.

Harald V alizaliwa Februari 21, 1937, na alikuwa mfalme wa Norway kwa kipindi cha zaidi ya miongo mitatu, akishuhudia mabadiliko mbalimbali ya kijamii na kisiasa nchini humo.
1787906051268.png
 
Kuna watu wengine wanatamani tuwe na utawala kama wa kifalme hivi ambapo eti rais anatawala hadi mauti yanamkuta na kwa mtizamo wao sijui akifa anamuachia nani urais kwa Afrika hii ni ngumu sana kutokana na hulka ya waafrika kwani huyo rais na wapambe wake watakuwa na utajiri wa kufuru huku wananchi wake wakitafuta mabaki ya vyakula kwenye dampo la huyo "rais".
Ndio mlivyo karirishwa kwani libya ilikua ipo ulaya mashariki ama magharibi???
Dikteta kaondoka ukweli usemwe tu yaani
Hata wafalme wa ulaya na malkia wanajilimbikizia mali na raia wao wanaishi hovyo
Uingereza wanalala mpaka nje na ughali wa maisha
 
Kuna watu wengine wanatamani tuwe na utawala kama wa kifalme hivi ambapo eti rais anatawala hadi mauti yanamkuta na kwa mtizamo wao sijui akifa anamuachia nani urais kwa Afrika hii ni ngumu sana kutokana na hulka ya waafrika kwani huyo rais na wapambe wake watakuwa na utajiri wa kufuru huku wananchi wake wakitafuta mabaki ya vyakula kwenye dampo la huyo "rais".
Ndio heri utawala wa kifalme kuliko democrasia ya ovyooo
 
Ndio heri utawala wa kifalme kuliko democrasia ya ovyooo
Ndio nauliza kwa mazingira ya Tanzania huyo mfalme atapatikanaje?

Kuna vitu vingine unapoviwaza ni kama umebakiwa na akili za kuvukia barabara tu.
 
Back
Top Bottom