Mfalme Daudi wa Tanzania

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,619
12,283
Mfalme Daud ni moja ya wafalme wali itawala israel nakutokana na uadilifu wake na mapenz yake kwa Mungu, Mungu alipitia uzao wake kumpata nabii Isa au kwa wakriso wanamuita Yesu.

Mfalme Daud kabla yakuwa mfalme alikuwa mchunga mbuzi na köndoo wa baba yake Yese, pia alikuwa mpiga kinubi mzuri sana.

Mfalme huyu kabla yakuwa mfalme alipita nyakati nzito sana kiasi ukisoma Histor yake unasisimka mwili. Wakati ule palikuwa na watu wali itwa wafilisti na katikati yao alikuwa jemedari wao alie itwa Goliati. Alikuwa pande la mtu jitu kubwa lililo shinda vita moja hadi nyingine.

Kipindi kile taifa hilo chini ya mfalme Saul, Goliati alitaka mtu wakupigana naye na ikiwa atamshinda basi Israel watatawaliwa na wafilist na ikiwa atashindwa bas wafilisti watakuwa watumwa wa Israel. Israel na wafilisti walipiga kambi kwa muda mrefu wakitafuta mtu wakupigana na Goliati.

Siku moja Daud akatumwa kuwapelekea chakula kaka zake vitani na huko ndipo miujiza ilianza. Kufupisha Daud alipokuwa akienda kwenye uwanja wa vita alitaka apewe nafasi kupigana na Goliati. Habari hizi zilimfikia Mfalme pamoja na masimango na vitisho alipewa Daud alidhamiria kupigana na Goliati.

Siku ile Daud alikataa mavaz yakijeshi akachukua kombeo lake kupigana na Goliati. Goliati alipo muona alimdharau sana Daud. Ila Daud akasema atampiga nakumkata kichwa kwa jina La Mungu wake alie watukana majesh ya Israel. Kwa hakika Goliati aliuwawa na kijana mdogo sana na dunia wakati ule ikawa ni story kubwa sana.

Tanzania pia ktk hali ya upendo mkubwa wa Mungu taifa hili tumempata Daud mwenye aina ya maisha na mienendo inayo fanana na DAUD. Mh Dk Magufuli amekuwa na mikakati na misimamo yakupigana na goliati aka mafisadi kwa gharama yeyote na hao magoliati wamekuwa na mtazamo wa goliat yule wa wafilisti eti watamshinda wakisahau yeye ana Mungu na Mungu hajawah shindwa popote pale nia ya huyu Rais ndio nia ya Mungu wetu kwa taifa hili teule kufupisha ni kwamba Daud wetu wa Tz ambaye ndie Rais lazima atawashinda na ufisadi utakuwa histor ktk taifa hili. Tanzania imempata mfalme Daud na sina shaka mfalme wetu atashinda chini ya mkono wa Mungu tunaye muomba kila siku.

Mungu ibariki Tanzania na Rais wetu.
 
Anapaswa kutafuta namna ya kusolve problem ya viwanda vyetu vya sukari kuliko kukimbilia kuanza kamatakamata ya wafanyabiashara,Nitamwona anaandaa nchi kuwa ya viwanda kama ataanza na uboreshaji wa viwanda vya sukari tofauti na hapo hizo sifa muda si mrefu zitapotea.
 
Mfalme Gaudi atapita na serikali yake ila Tanzania itajengwa na watoto wa mfalume Daudi yaani vijana wa leo.kama Sulemani alivyo jenga kanisa la Mungu.
 
Kama mafisadi walishindwa kuingia Ikulu basi watarajie kugeuka mashetani
 
Haujaelezea hadithi yote, ngoja nimalizie kwa kifupi. Daudi alipokuwa anatembeatembea kwenye ghorofa ya nyumba yake akamuona Mwanamke mwenye umbile zuri sana mke wa mtu akiwa anaoga bafuni, akafanya hila mpaka akatembea na huyo mama na kumpa mimba, kilichotokea baada ya hapo ilikuwa ni masikitiko makubwa sana kwa familia ya daud
 
waTZ, sindiyo anaanza hatua moja baada ya ingine.. ni lazima auondoe uchafu na vipingamizi njiani ili aweze kutufikisha huko mbele!!!
TumainiEl ndiyo kiongozi mwenye kufuata nyao za Daud ... God bless JPM!!!
Watasubiri sana Daudi wao ampige goliati haitatokea Daudi huyu amebaki kubweka kama mbwa nje ya nyumba ya Goliati akijua Goliati anafungua mlango lazima aondoke aje na agenda nyingine.
 
ni kweli jpm anaweza kufananishwa na daudi kwani hata upatikanajiwa wake haukutarajiwa hakuna aliyempa nafasi kubwa ya kuwa raisi wa nchi,

kama daudi
kwani hata samweli alipoenda kuwatia mafuta wana wa yese ili apatikane mfalme daudi hakuwepo.

alikuwa kuchunga kondoo wa baba yake.
 
Mfalme Daud ni moja ya wafalme wali itawala israel nakutokana na uadilifu wake na mapenz yake kwa Mungu, Mungu alipitia uzao wake kumpata nabii Isa au kwa wakriso wanamuita Yesu.

Mfalme Daud kabla yakuwa mfalme alikuwa mchunga mbuzi na köndoo wa baba yake Yese, pia alikuwa mpiga kinubi mzuri sana.

Mfalme huyu kabla yakuwa mfalme alipita nyakati nzito sana kiasi ukisoma Histor yake unasisimka mwili. Wakati ule palikuwa na watu wali itwa wafilisti na katikati yao alikuwa jemedari wao alie itwa Goliati. Alikuwa pande la mtu jitu kubwa lililo shinda vita moja hadi nyingine.

Kipindi kile taifa hilo chini ya mfalme Saul, Goliati alitaka mtu wakupigana naye na ikiwa atamshinda basi Israel watatawaliwa na wafilist na ikiwa atashindwa bas wafilisti watakuwa watumwa wa Israel. Israel na wafilisti walipiga kambi kwa muda mrefu wakitafuta mtu wakupigana na Goliati.

Siku moja Daud akatumwa kuwapelekea chakula kaka zake vitani na huko ndipo miujiza ilianza. Kufupisha Daud alipokuwa akienda kwenye uwanja wa vita alitaka apewe nafasi kupigana na Goliati. Habari hizi zilimfikia Mfalme pamoja na masimango na vitisho alipewa Daud alidhamiria kupigana na Goliati.

Siku ile Daud alikataa mavaz yakijeshi akachukua kombeo lake kupigana na Goliati. Goliati alipo muona alimdharau sana Daud. Ila Daud akasema atampiga nakumkata kichwa kwa jina La Mungu wake alie watukana majesh ya Israel. Kwa hakika Goliati aliuwawa na kijana mdogo sana na dunia wakati ule ikawa ni story kubwa sana.

Tanzania pia ktk hali ya upendo mkubwa wa Mungu taifa hili tumempata Daud mwenye aina ya maisha na mienendo inayo fanana na DAUD. Mh Dk Magufuli amekuwa na mikakati na misimamo yakupigana na goliati aka mafisadi kwa gharama yeyote na hao magoliati wamekuwa na mtazamo wa goliat yule wa wafilisti eti watamshinda wakisahau yeye ana Mungu na Mungu hajawah shindwa popote pale nia ya huyu Rais ndio nia ya Mungu wetu kwa taifa hili teule kufupisha ni kwamba Daud wetu wa Tz ambaye ndie Rais lazima atawashinda na ufisadi utakuwa histor ktk taifa hili. Tanzania imempata mfalme Daud na sina shaka mfalme wetu atashinda chini ya mkono wa Mungu tunaye muomba kila siku.

Mungu ibariki Tanzania na Rais wetu.
Nanukuu: nyerere aliwahi kusema katiba ya nchiii hii ukiitumia tofauti unaweza ukajiita mungu kama sijakosea sasa naona mwisho wa siku itakuwa hivo
 
Du!, nimemkumbuka Mfalme Daudi, baba yake na Mfalme Suleiman, ni kweli Daudi alikuwa shujaa, ila pia hakuwa malaika!, alikuwa na udhaifu mmoja mkubwa wa kupenda 'chini' kupindukia!. Siku moja akamuona mke wa jemedari wake Uria, akamtamani, ili ampate, akaamua kumuua mumewe Uria, kwa kumtuma vitani bila kujiandaa ili aangamizwe!, ni kweli Uria aliuawawa vitani na majeshi yake mengi yakateketea kwa ajili ya Mfalme Daudi kupata 'chini' moja tuu!. Baada ya kifo cha Uria, Mfalme Daudi akamtwaa mke wa Uria na kumfanya ndio mkewe, na ndiye aliyemzalia Suleiman!.

Kufuatia Suleiman kuzaliwa kwa tamaa ya 'chini', ugonjwa huo kwa Suleiman ndio alikuwa balaa!, alioa wanawake 800!, na masuriya 200!, na miongoni mwa mabibi zake ni Queen of Sheba ambapo Suleiman alikufa akaoza!, akahamisha dhahabu yote ya Israel na kumhonga huyo mwanamke, Queen of Sheba, ambapo alikwenda kuificha kichawi, chini ya Milima ya Abysinia iliyopo Ethiopia!, cha ajabu baada ya kufa kwa Queen of Sheba, wote waliotafuta ile hazina, waliishia kuchimba tuu mashimo na kubaki patupu kutokana na kibibi kichawi Gagula kuilinda hazina ile mpaka leo!.

Huyo ndio Daudi yule!, vipi huyu Daudi wetu!, unaujua udhaifu wake?!.

Pasco
 
Back
Top Bottom