Mfahamu vizuri Vladimir Putin, Rais wa Urusi

Rais wa Urusi, Vladimir Putin amepata mkanda mweusi wa nane katika karate. Putin mwenye miaka 63, ni mwanafunzi wa Kyokushin, aina ya karate ambayo wachezaji hawavai vifaa maalum kichwani. Putin pia ni mahiri kwenye martial arts ambapo alipewa mkanda mweusi wa tisa kwenye taekwondo mwaka 2013. Pia ni mchezaji mzuri wa judo
 
RAIS wa Urusi, Vladimir Putin ametajwa tena kuwa mtu mmoja mwenye nguvu kubwa ya ushawishi kwa mara ya tatu mfululizo. Kiongozi huyo mwenye miaka 63, ameendelea kushikilia nafasi hiyo katika orodha inayotolewa kila mwaka na jarida mashuhuri la Forbes.

Kwa mujibu wa jarida hilo, uamuzi wa kumteua na kumweka mtu katika orodha hiyo, umetokana na kiwango cha fedha anachomiliki au kuongoza; idadi ya watu wanaoathirika na uamuzi wake na uwezo wake wa jumla wa ushawishi. Pia wanaangalia namna gani ameonekana akitumia uwezo na nguvu zake za ushawishi, ambapo Putin ameonekana ndiye anayeongoza moja ya nchi kubwa duniani na hatua ambazo amekuwa akichukua Ukraine na Syria, zimekuwa zikiripotiwa karibu kila siku.

Aliyeshika namba mbili katika orodha hiyo, ni Kansela wa Ujerumani Angela Merkel; ambaye amekuwa mmoja kati ya wanawake tisa tu walio katika orodha hiyo ya watu 73 na amepanda kutoka namba tano aliyokuwa mwaka jana. Uongozi wake katika Jumuiya ya Ulaya, hasa majadiliano yake na Ugiriki na namna alivyokabiliana na changamoto za suala la wahamiaji, vimemfanya aonekane kuwa mtu aliyetumia uwezo wake wa ushawishi.

Aliyeshika namba tatu ni Rais wa Marekani, Barack Obama, ambaye anatarajiwa kuachia ngazi mwaka huu baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Novemba. Amekuwa Rais wa kwanza wa Marekani aliye madarakani, kutokuwa katika nafasi mbili za juu kutokana na hatua zake za kuepusha nchi hiyo kujihusisha na vita katika nchi za nje na mazingira aliyonayo ya Rais anayemaliza muda wake.

Papa Francis ametajwa kushika nafasi ya nne katika orodha hiyo, kutokana na ziara alizofanya katika miezi 12 iliyopita, ambapo pamoja na umri wake wa miaka 78, amevuta watu wengi katika ziara hizo na kufanya ishara za kushangaza. Ziara zake Marekani na Cuba pamoja na kauli zake kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, sakata la uhamiaji katika nchi za Ulaya na mauaji yanayoendelea Mashariki ya Kati, vimesababisha atengeneze ajenda mbalimbali zilizovutia vyombo vingi vya habari.

Orodha hiyo imemtaja Rais wa China Xi Jinping, mwenye umri wa miaka 62, kuwa kiongozi mwenye ushawishi mkubwa kuwahi kutokea katika taifa hilo, baada ya Mao Tse-Tung. Misimamo yake kuhusu suala la Bahari ya Kusini mwa China, hotuba zake chache katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa na namna anavyokubalika kimataifa, vimesababisha mara kwa mara atoe habari kubwa katika vyombo mbalimbali vya habari.

Mwaka jana kulitokea dalili za kuibuka kwa vita baridi kati ya Magharibi na Mashariki baada ya Rais Putin kuamua kuingilia mgogoro wa ndani wa Ukraine, kuhusu Jimbo la Crimea lililoko Kusini mwa nchi hiyo, likipakana na Urusi, upande wa Magharibi. Utafiti wa mitandao kadhaa ya kijamii, ilimtaja Putin kuwa mtu mwenye nguvu zaidi duniani, si kwa maana ya misuli, bali kwa mamlaka yake katika nchi anayoiongoza, nafasi ya nchi hiyo ya Urusi katika siasa za kimataifa na hatua alizochukua katika miezi ya hivi karibuni, dhidi ya misimamo na matakwa ya nchi za Magharibi zinazoongozwa na Marekani.

Mtandao wa Fobes, ulipiga kura kumpata mtu mwenye nguvu kubwa duniani, ambapo kwa vigezo vya kuwa Mkuu wa nchi iliyokuwa na uwezo mkubwa wa kivita duniani, ambayo sasa ni nchi inayotambulika kuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za kimataifa, Rais Putin alitajwa kuwa ndiye mtu mwenye nguvu zaidi duniani, akifuatiwa na Rais Obama na Rais Xi Jinping. Historia ya Putin Rais Putin anaishi katika Mji Mkuu wa nchi hiyo wa Moscow.

Ni msomi mwenye Shahada ya Uzamivu katika Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Peter cha Urusi. Alizaliwa Oktoba 7, 1952 katika mji wa Saint Peter, katika famila ya Vladimir Spiridonovich Putin na Maria Ivanovna Putin. Mama yake alikuwa mfanyakazi wa viwandani na baba yake alikuwa katika Jeshi la Wanamaji la Urusi, ambako aliwahi kufanya kazi katika nyambizi katika miaka ya mwanzo ya 1930.

Babu yake Putin, Spiridon Ivanovich Putin, alikuwa mpishi wa wanamapinduzi wa Urusi, Vladimir Lenin, na Joseph Stalin ambao wamewahi kuongoza nchi hiyo. Mama yake aliuawa na majeshi ya Ujerumani wakati yalipovamia Urusi mwaka 1941, na mjomba wake hakujulikana alipofia wakati wa vita hiyo. Septemba mosi 1960, alianza shule na alipotimiza miaka 12 alianza kushiriki katika michezo ya kujihami, ikiwemo Judo.

Katika ujana wake, Putin alipenda tabia ya waigizaji wa filamu za mambo ya usalama, akiwemo Vyacheslav Tikhonov na Georgiy Zhzhonov. Alihitimu masomo yake katika sheria za kimataifa mwaka 1975, ambapo aliandika thesisi yake ya mwisho yenye kichwa cha habari cha “Kanuni za Biashara za Kimataifa Zinazotoa Upendeleo katika Sheria za Kimataifa.” Akiwa Chuo Kikuu, alijiunga na Chama cha Kikomunisti cha Urusi na kubakia mwanachama mpaka chama hicho kilipovunjwa mwaka 1991.

Agosti 1999, Putin aliteuliwa kuwa mmoja kati ya naibu watatu wa Waziri Mkuu, na siku hiyo hiyo aliteuliwa kuwa Kaimu Waziri Mkuu, wa Serikali ya Urusi chini ya Rais Boris Yeltsin. Yeltsin pia alitamka kuwa angependa kuona Putin akirithi nafasi hiyo ya Mkuu wa Nchi na muda mfupi baadaye ilikubaliwa kuwa Putin agombee Urais. Aidha, mwezi huo huo Bunge la Urusi, lilikubali kuwa Putin awe Waziri Mkuu baada ya kupata kura 233, huku kura 84 zikipinga na kumfanya kuwa Waziri Mkuu wa Tano wa Urusi.

Wakati akiteuliwa kushika nafasi hiyo, Putin hakuwa akijulikana kwa wananchi na mara kwa mara alikuwa akitambuliwa kuwa mtu wa karibu wa Rais Yeltsin na kama ilivyotarajiwa, Putin hakujichagulia mawaziri peke yake, badala yake alikabidhi Ofisi ya Rais kufanya kazi hiyo. Wakati Rais Yeltsin alipoanza kuwa mgonjwa, wapinzani wake walianza kampeni ya kumrithi kutokana na kuugua kwake, ambapo sehemu ya kampeni hiyo ilikuwa kuzuia Putin asionekane kuwa mmoja wa watu wanaofaa kumrithi Rais Yeltsin.

Ingawa mwanzoni haikujulikana ni chama gani alikuwa akikiunga mkono, baadaye alionekana wazi wazi akiunga mkono chama kipya cha Unity Party, ambacho kilipata kura nyingi katika Uchaguzi wa wabunge, na baadaye chama hicho kilimuunga mkono. Vitisho vyake Vladimir Putin mwaka jana alitishia nchi za Mashariki kuwa jaribio la kuhujumu Urusi, ikiwemo kuiwekea vikwazo kutokana na uamuzi wake wa kuingilia mgogoro wa Ukraine, kutasababisha kutokuelewana baina ya mataifa yenye nguvu za kivita na hata kuweka amani na utulivu wa dunia katika mashaka.

“Washirika wetu wanapaswa kufahamu kuwa shinikizo lolote kwa Urusi, iwe la taifa moja au kundi la mataifa ikiwemo kuweka vikwazo kwa Urusi, haitasaidia kudumisha amani, zaidi itazidisha mjadala,” alikaririwa Putin katika mazungumzo yake na jarida la Respublika. “Tutazungumziaje ukuaji na maendeleo ya Ukraine, wakati kuna uamuzi unachukuliwa mara kwa mara kuweka vikwazo vipya huku wakitaka makubaliano ya amani, kama lengo lao ni kuitenga nchi yetu, wanajidanganya,” alikaririwa akisema.

Kiongozi huyo wa Urusi aliendelea: “Tunatarajia kuwa washirika wetu watatuelewa, kuna athari ya malengo yao ya kutaka kuihujumu Urusi …nadhani wanafahamu wazi nini kitatokea, ikiwa kutatokea kutoelewana kati ya nchi zenye uwezo mkubwa wa kivita kwa amani ya dunia.” Mwishoni mwa Agosti, Putin aliwaambia vijana wa nchi hiyo kuwa “Sitarajii kujitokeza kwa taifa au kundi la mataifa litakalotuchezea.

Nashukuru Mungu hakuna hata mmoja wetu anayefikiria kuanzisha mgogoro mkubwa na Urusi. Nataka kuwakumbusha kuwa Urusi ni moja ya mataifa yenye nguvu za kivita.” Mpaka sasa Putin ameacha alama katika siasa za kimataifa, hasa kuhusu hatua mbalimbali za kiuchumi na kauli zake kuhusu amani ya dunia, ingawa haijajulikana lengo lake kubwa ni nini.

Wataalamu wa siasa za kimataifa, wamekuwa wakijadili kama Putin anaweza kwenda mbali ya kutishia mataifa ya Magharibi au kusababisha vita ya dunia, au ni sehemu ya haiba ya uongozi wake. Hata hivyo, mmoja wa wasaidizi wa karibu wa Putin, Sergei Pugachev, amewahi kusema kuwa Putin hana mpango wa kuharibu amani ya dunia, ila kauli zake na mikakati ni matokeo ya siasa za kimataifa za sasa.

Pugachev anayetajwa kuwa rafiki wa karibu wa Putin, ambaye amekuwa akitumia muda mrefu kuzungumza naye, urafiki wao ni wa siku nyingi tangu Putin alipokuwa Meya wa mji wa St. Petersburg’s, ambapo Pugachev alikuwa mshauri wake.

Anasema haamini kama kuna kitu kama hicho cha Putin kutaka kuharibu amani ya dunia, kwa kuwa kwanza hakupanga kuwa Rais wa Urusi, bali aligombea katika nafasi hiyo, kwa kuwa hakukuwa na mbadala. “Hakuwa na mpango huo, hakutaka kuwa Rais wala hakufikiria kuwa Rais na pia hakufikiria kufanya kazi na Serikali kwa muda mrefu,” anasema Pugachev.
 
Magufuli kwenye kampeni alipiga pushups tu, ukawa wanalia mpaka leo....yote haya angeyafanya yeye, wangelia to the end of the world.
Kwani umemuona Putin anakunywa kikombe cha babu hapo?acha masihara basi
 
Rais wa Urusi, Vladimir Putin amepata mkanda mweusi wa nane katika karate. Putin mwenye miaka 63, ni mwanafunzi wa Kyokushin, aina ya karate ambayo wachezaji hawavai vifaa maalum kichwani. Putin pia ni mahiri kwenye martial arts ambapo alipewa mkanda mweusi wa tisa kwenye taekwondo mwaka 2013. Pia ni mchezaji mzuri wa judo
Sisi tuna mikanda mingi sana myeusi ya suruali
 
Akitoka Putin atakuja Dmitry Medvedev.

Yaani wamekuwa wakibadilishana uraisi kwa waziri mkuu.
 
Back
Top Bottom