Mfahamu ndege Tai na tabia zake

Mfahamu ndege Tai na tabia zake

View attachment 433066

UTANGULIZI

Tai ni moja kati ya aina ndege walio maarufu, Umaarufu wake umejikita katika mtindo wake wa maisha ambao ni wa kipekee.
Kuna aina nyingi wa Tai mfano; kuna tai mwenye mkia mweupe, kuna tai mwenye rangi ya dhahabu, kuna tai wa Ufilipino na kadhalika. Inakadiriwa kufikia aina sitini za tai duniani na wengi wao wanaoatikana Afrika, Ulaya na Asia.

Tai ni ndege aliye na sifa za upekee hasa kutokana na ufundi wao wa kuwinda, uwezo wao wa kuona kwa macho ni mzuri kwa sababu anaona Umbali mara saba zaidi ya jinsi anavyoona binadamu.

Tai hukadiriwa kuweza kuishi zaidi ya miaka 60 na pindi afikishapo miska 50 makucha yake huwa yanakuwa yameshachoka, mdomo wake nao huisha makali.

View attachment 433067

TUANGALIE MAISHA YA TAI

Jambo la Kwanza
Tai hupaa juu sana angani wala shomoro na kunguru hawawezi kufika huko. Hakuna ndege yeyote mwenye uwezo wa kupaa juu sana kufikia kimo anachofikia. Mara nyingi huwa tunawaona mwewe wakipita sehemu fulani, shomoro na kunguru huwazomea lakini tai hataki ujinga huo.
FUNZO: Kaa mbali na shomoro na kunguru, Tai huruka na tai wenzie.

Jambo la Pili
Tai wanauwezo wa kuona mbali sana. wanauwezo kuona kitu kilichoko umbali wa kilometa tano. Tai akiona mawindo yake huangalia pale pale na huanza kwenda kukamata mawindo hayo kwa kasi kubwa. Haijalishi kama kuna vipingamizi vyovyote njiani, tai hatabadili kuangalia mawindo yake hadi akamate mawindo.

FUNZO: Unatakiwa kuwa na maono na uyatazame mpake uyapate au uyatimize hiyo ndio siri ya kuelekea mafanikio yako, haijalishi vikwazo unavyokumbana navyo njiani, wewe kaza mwendo bila kurudi nyuma.

Jambo la tatu
Tai hali mzoga, anakula kile tu alichokamata yeye.

FUNZO: Kuwa makini na kile unacholisha macho yako, masikio yako hasa kuangalia filamu na luninga. Usipende kutumia mizoga (mambo machafu) kwa sababu utaiharibu nafsi yako na maisha yako hatakwenda kwa kasi kubwa ya mafanikio.

Jambo la nne

Tai wanapenda mvua kubwa na yenye upepo. Mawingu yakikusanyika tai wanafurahi. Tsi hutumia upepo wa mvua kupaa juu sana hatumii nguvu nyingi kupaa anaweza kutandaza tu mabawa yake halafu anaanza kuelea bila shida akifurahia maisha mazuri. Huku ndege wengine wakati wa mvua kubwa yenye upepo hujificha kwenye mapango.

FUNZO:Tunaweza kutumia mvua kubwa yenye upepo(changamoto) kujinyanyua juu sana watu wote waliofanikiwa wengi wao hufanikiwa wakati wa changamoto kubwa. Wao hutumia mvua ya upepo kupaa juu sana angani tena wakati mwingine juu ya mawingu.

Jambo la tano

Tai hupima kwanza kabla ya kuamini. Tai jike akitaka kukutana na tai dume na wakataka kujamiiana, tai jike hupaa kwa kasi kubwa kwenda chini wakati huo tai dume anafuatia kwa nyuma. Akifika chini huchukua tawi la mti kisha hupaa tena angani na tawi hilo huku tai dume anafuata kwa nyuma. Akifika umbali mrefu angani tai jike huliachia hilo tawi na tai dumr hulikimbilia mpaka alikamate kabla halijadondoka chini na akisha likamata analirudisha tena juu kwa tai jike. Tai jike atalipokea hilo tawi na anapaa nalo juu sans halafu analidondosha tena. Kama kawaida yake tai dume atalifukuzia mpaka alikamate na atalirudisha kwa tai jike tena. Tai jike ataendelea na mchezo huu mpaka ajirizishe kwamba tai dume huyo yuko vizuri na amefuzu majaribio hayo. Hapo ndipo tai jike atakubali kupandwa na tai dume huyo jike.

FUNZO: Katika maisha yako binafsi au katika biashara au katika mapenzi yako, unatakiwa kupima mtu unayetaka kumpenda au kushirikiana naye kama kweli ana dhamira ya dhati au ni muogizaji tu.

Jambo la Sita

Tai akitaka kutaga mayai, tai jike na tai dume hushirikiana kutafuta sehemu iliyo juu sana kwenye mti ambayo sehemu hiyo haina maadui. Kisha tai dune anaenda chini ardhini kuchukua mitu yenye miiba anakuja anaitandaza kwenye sehemu wanayotengeneza kiota. Tai dume tena hurudi ardhini kuchukuwa matawi ya mitu kwa ajili ya kutengeneza kiota kikubwa. Kisha baada ya kuweka miiba na vimatawi vidogo vya mti, tai huyu anaenda tena chini kuchukua majani laini, akimaliza kuweka majani laini anatudi tena kuchukua miiba anakuja anaiweka juu ya kiota ili kuzuia maadui na mwisho akimaliza hayo yote ana nyonyoa baadhi ya manyoya yake ili kuweka sehemu ya mayai. Wanasaidiana na tai dume kuyaatamia kwa zamu, pia kazi ya ulinzi huifanya wote kwa kushirikiana. Vifaranga wakishatotolewa; tai dume na tai jike hushirikiana kuwalea. Baada ya muda kidogo tai jike ataanza kuwatoa vifaranga na kuwaweka kwenye miiba pembeni kidogo ya kiota, halafu vifaranga hurudi ndani ya kiota, atafanya hilo zoezi mara kadhaa baadaye atayaondoa manyoya kwenye kiota. Wale watoto wakirudi kwenye kiota watakutana na miiba itawachomachoma na kuvuja damu. Kisha tai jike atawarusha chini wale vifaranga kabla hawajadondoka tai dume atawadaka ataendelea na zoezi hilo moaka watoto wafahamu kuruka.

FUNZO: Pale tai wanapoandaa kiota wanatufundisha kujuandaa kwa ajili ya mabadiliko. Lakini ushiriki wa mke na mume ni muhimu sana ili kujenga familia yenye mafanikio.

Jambo la saba

Tai anapozeeka, manyoya yake huwa dhaifu na hayatamwezesha kupaa kwa kasi kama hapo zamani. Akiona hivyo huenda kwenye pango mbali na maadui, akifika humo kwenye pango hujinyonyoa manyoya yote hadi anabaki uchi kabisa. Anaendelea kujificha humo mpaka anaota manyoya mengine ndipo anatoka nje.

FUNZO:Wakati mwingine tunatakiwa kuziacha baadhi ya tabia mbaya ambazo zinatukwamisha kufikia mafanikio yetu makubwa.

View attachment 433068View attachment 433167
Jambo lingine analo fanya Tai katika process ya rejuvination ni kunyofoa kucha na kugonga domo lake kwenye mwamba mpaka linaisha lote,wakati huhuo anapojinyonyoa manyoya,kisha hujificha pangoni mpaka domo na kucha viote.
 
pia kwa muda huo hula wadudu wadogo wadogo mpk atakapo recover tena...
 
Kilichonifurahisha ni aina ya" mapenzi " ya hao Tai kupimana kwa tawi la mti lisifike ardhini , hapo nimepapenda,... sijui kama kuna aina nyingine ya viumbe wanajaribiana kwa kiasi cha Tai....
Nyuki, ila ukifaulu ujue ndo kifo chako...
 
Daaah Tai now ndo itakua nembo yangu ya kunitambulisha mimi kama mimi
 
Andiko linatia hamasa, hongera mkuu.
Ila katu hatuwezi kuwa tai ila tunaweza kujifunza filosophy ya maisha ya tai.

Diversity ndio ukweli na Nature ya maisha.

Ukiona mwanadamu anatamani kuwa ndege tai, u must know something must be wrong somewhere?
Kiumbe mwanadamu ndo kiumbe kilichobarikiwa kuliko viumbe vyote

Jaribu kufikiri kiumbe kinachoweza kuvumbua na kuaply technology ya simu ,TV, aeroplane, cars etc

Ufahamu wa mwanadamu ktk kuelewa genetics ya viumbe hai na namna anavyoweza iaply na kuleta ustawi wa afya na huduma zingine.

Ebu piga picha kiumbe aliyebarikiwa, vipaji na uwezo wa kuimba, kucheza, kuzungumza, ubunifu, ujenzi, etc... Jamani utukufu aliovikwa mwanadamu ni mkuu mno na hajabu Sana.

Kama kuna viumbe tunavyoweza kuruhusu kuinspire Maisha yetu basi wawe wanadamu wenzetu waliofanikiwa ktk mambo tunayotamani kuyaishi.
 
Tumependelewa kuliko kiumbe chochote hapa duniani
 
Masahihisho: Tai anakula mizoga pia, rejea maandiko, nimeshuhudia Serengeti mizoga ya wanyama wakubwa ikiliwa na Tai.
Picha uliyomalizia nayo story sio ya Tai, huyo anaitwa African Fish Eagle.
Eagle=Mwewe
Vulture=Tai
 
Imeandikwa ktk Zaburi ya 103:5 ujana wako ukarejezwa kama Tai!
Ahadi ya Bwana hiyo!
 
*MAAJABU YA NDEGE TAI!!!*
Tai ni ndege pekee mwenye uwezo wa kuishi miaka 70. Lakini kabla ya kufika umri huo lazima afanye maamuzi magumu,
yanayomuumiza na kumchukua muda mrefu. Akifikia umri wa miaka 40, makucha yake magumu na makali yanakosa uwezo wa kunyakua chakula, mdomo wake uliochongoka unapinda, mabawa yake yanakuwa mazito na kunata kwenye kifua chake hivyo kumfanya kuwa mzito kuruka na kuwa mwenye kasi ndogo.
Katika hali hiyo ndege huyo hubakiwa na maamuzi mawili; aidha akubali kufa au afanye mabadiliko katika mwili wake ili aendelee kuishi miaka 30 iliyobakia. Akichagua kufanya mabadiliko kwenye mwili wake humchukua siku 150 sawa na miezi 5, hivyo huenda katika kilele cha mlima mrefu na kujificha katika pango ambapo watu na wanyama wengine wanaoweza kumzuru hawafiki. Ndipo huanza kujivua kucha, midomo na mbawa zake zilizozeeka huku akisikilizia maumivu makali, baada ya mabadiliko hayo hurudi katika hali yake ya mwanzo ya kuweza kuruka kwa kasi na kupata chakula chake kizuri (fresh meat).
Bado siku 25 sasa ili tumalize mwaka, hivyo lazima ufanye mabadiliko makubwa sana katika maisha yako, ujivue baadhi ya tabia ambazo zimeleta Ukakasi katika maendeleo yako ya 2018 japo zingine ni ngumu kuziacha na pengine zitakusababishia Maumivu lakini "no pain no gain" lazima ujivue baadhi ya Marafiki wasiolekea unakoelekea, jivue Uvivu, jivue Uongo, jivue Mahusiano yasiyo na Amani, jivue Ulevi, jivue kulala sana, jivue Uasherati, jivue kuahirisha ahirisha Mipango yako, na mengine yanayofanana na hayo.
Ikiwa Tai anafanya maamuzi ya kubadilika akiwa na miaka 40, hata wewe bado hujachelewa...Fanya mabadiliko sasa, ingia Mwaka 2019 ukiwa na Tabia mpya na Mtazamo Mpya kwa ajili ya kuanza safari yako mpya ya maisha. MUNGU Akubariki Sana katika Maamuzi yaliyo sahihi
 
Wewe toa ushauri wako wooote lakini ukigusa Pombe hapo unatutafuta wanywaji, sasa kama husikii wewe endelea utakiona cha mtema kuni
 
nimesoma kote ila nilipofika kwenye ulevi jivue
nikaangalia glasi yangu nikaona hupendi vitu vizuri
nikagundua hata mkeo ulichagua kwa kigezo cha tabia
 
*MAAJABU YA NDEGE TAI!!!*
Tai ni ndege pekee mwenye uwezo wa kuishi miaka 70. Lakini kabla ya kufika umri huo lazima afanye maamuzi magumu,
yanayomuumiza na kumchukua muda mrefu. Akifikia umri wa miaka 40, makucha yake magumu na makali yanakosa uwezo wa kunyakua chakula, mdomo wake uliochongoka unapinda, mabawa yake yanakuwa mazito na kunata kwenye kifua chake hivyo kumfanya kuwa mzito kuruka na kuwa mwenye kasi ndogo.
Katika hali hiyo ndege huyo hubakiwa na maamuzi mawili; aidha akubali kufa au afanye mabadiliko katika mwili wake ili aendelee kuishi miaka 30 iliyobakia. Akichagua kufanya mabadiliko kwenye mwili wake humchukua siku 150 sawa na miezi 5, hivyo huenda katika kilele cha mlima mrefu na kujificha katika pango ambapo watu na wanyama wengine wanaoweza kumzuru hawafiki. Ndipo huanza kujivua kucha, midomo na mbawa zake zilizozeeka huku akisikilizia maumivu makali, baada ya mabadiliko hayo hurudi katika hali yake ya mwanzo ya kuweza kuruka kwa kasi na kupata chakula chake kizuri (fresh meat).
Bado siku 25 sasa ili tumalize mwaka, hivyo lazima ufanye mabadiliko makubwa sana katika maisha yako, ujivue baadhi ya tabia ambazo zimeleta Ukakasi katika maendeleo yako ya 2018 japo zingine ni ngumu kuziacha na pengine zitakusababishia Maumivu lakini "no pain no gain" lazima ujivue baadhi ya Marafiki wasiolekea unakoelekea, jivue Uvivu, jivue Uongo, jivue Mahusiano yasiyo na Amani, jivue Ulevi, jivue kulala sana, jivue Uasherati, jivue kuahirisha ahirisha Mipango yako, na mengine yanayofanana na hayo.
Ikiwa Tai anafanya maamuzi ya kubadilika akiwa na miaka 40, hata wewe bado hujachelewa...Fanya mabadiliko sasa, ingia Mwaka 2019 ukiwa na Tabia mpya na Mtazamo Mpya kwa ajili ya kuanza safari yako mpya ya maisha. MUNGU Akubariki Sana katika Maamuzi yaliyo sahihi
Barikiwa sans.message nzuri
 
Insha Allah

Back
Top Bottom