Salahan
JF-Expert Member
- Sep 10, 2014
- 2,963
- 3,675
1. Mark Zukerberg ndiye mmiliki wa mitandao ya Facebook, Whatsapp na Instagram,
2. Ana umri wa miaka 31, alivumbua mtandao wa facebook akiwa na miaka 20 tu. Baadae akaamua kuununua mtandao wa Whatsapp na kuanzisha mtandao wa Instagram.
3. Mark Zuckberg anaeshikilia rekodi ya dunia ya kuwa bilionea mdogo zaidi aliyoiweka akiwa na miaka 23 tu!..
4. Mark haamini kabisa kuwa kuna Mungu.
5. Mark hajawahi kumiliki TV! Maisha yake amekuwa akitumia computer tu.
6. Mara kadhaa amepigiwa upatu kuwa mtu maarufu anaevaa vibaya zaidi duniani! Mara nyingi upendelea kuvaa t-shirt na jeans au kaptura na sandals.
Hata alipoalikwa ikulu ya White house kukutana na Rais Obama alivaa t-shirt na jeans. Wengi huona kama vile hajijali.
7. Unaweza kumblock mtu yeyote facebook kasoro yeye tu! Ukiingia kwenye ukurasa wake option ya kumblock ipo lakini haifanyi kazi. Ukiclick "block" inakuambia error. Kwa kifupi huwezi kumblock. Ingia hapa Mark Zuckerberg | Facebook na ujaribu uone!.
8. Mwaka 2009 Mark alivaa tai kwa mwaka mzima kuonyesha ni jinsi gani mwaka huo ulikuwa serious. Baada ya hapo Mark hakuvaa tai tena unless kuwe na matukio maalumu.
9. Akiwa na miaka 13 tu Mark alitengeneza mtandao wa familia uliokuwa ukiziwezesha kompyuta kutumiana meseji ndani ya nyumba yao!
10. Licha ya Twitter kuwa Mshindani namba moja wa facebook, lakini Mark ni mtumiaji wa mtandao huo pia! Ana akaunti twitter akiwa na wafuasi zaidi ya milioni 1.
11. Mwaka 2011 aliamua kutokula nyama yeyote mpaka awe amechinja mwenyewe!
12. Alimuoa mkewe "Priscilla" 19/05/2012 siku ambayo mkewe alikua anahitimu shahada yake ya udaktari (MD) kutoka Chuo Kikuu cha Carlifonia. Kwahiyo sherehe ya harusi ilienda sambamba na sherehe ya graduation kwa mkewe.
13. Mark Aliacha shule akiwa na miaka 20 chuo kikuu cha Havard. Inadaiwa alikua akibishana na waalimu wake "maprofesa" ambao walimlazimisha kujibu kadri alivyofundishwa. Alipojibu kwa kadri ya uelewa wake alikosa japo anaamini alikua sahihi kujibu vile alivyojua sio vile alivyokariri.
14. Alimuoa Priscilla Chan mwaka 2012 baada ya kukaa naye kwenye mahusiano kwa miaka 10. Walikutana mwaka 2003 wote wawili wakiwa wanafunzi chuo kikuu cha Havard.
15. Kwa mujibu wa mtandao wa Boston.com - Local breaking news, sports, and culture jumla ya utajiri wao ni dola Bil.35 (takriban shilingi Trilioni 80). Lakini pato lao kwa mwaka limekua likiongezeka mara dufu.
Mwaka jana 2015 jumla ya pato lao (annual income) ilikua dola bilioni 12 (yani shilingi trilioni 25). Kiasi hiki kikubwa kuliko bajeti ya nchi kama Tanzania ambayo ni Trilioni 22 kwa mwaka. Yani pato la mtu mmoja linzaidi pato la nchi.!
JIFUNZE
Si kila mvumilivu huishia kula mbivu, wapo walio vumilia sana na bado wakaishia kupata maumivu.
Na si kila subira huvuta heli, subira nyingi kuizidisha shali.
Tena kubwa jingine wale waliosema mwendapole hajikwai Hii si kwawote, kuna walio jaribu kwenda pole pole lakini matokeo yake hakuishia kujikwaa tu bali na kupoteza kucha na vidole vya miguu. Hapo utatambua Kuwa maisha hayana kanuni"Formula".