Mfahamu malkia wa kuzimu.

Ciprofloxacin.

JF-Expert Member
Apr 15, 2015
1,583
2,697
Dunia inateswa na mambo mengi Sana ambayo wengi wetu huwa tunadhani yanatokana na akili zetu na mawazo yetu ama pengine ni uamuzi wetu binafsi.
La hasha, kila jambo linalotokea huwa limepangwa ktk ulimwengu wa roho tusioweza kuuona Kwa macho ya damu na nyama.
Kiongozi mkuu au mfalme wa maovu na shida zote duniani ni shetani ,kuzimu wanamwita Lucifer.
Huyu ni kiongozi mkubwa Sana ambaye makazi yake ni chini ya maji, bahari na maziwa. (kuzimu)
Lucifer huwa hafanyi kazi yoyote ngumu, yeye hupokea Taarifa na kutoa amri Kwa pepo mkuu Belzebur, ambaye naye huwaagiza mapepo wengine watatu ambao nao ni wakuu.
Kwa Sababu maalumu, nitamtaja pepo mmoja tu Kati ya hao watatu wengine na kazi zake hapa duniani.
Kwa kawaida, Lucifer ana serikali yake kuzimu yenye dola kamili, na waziri mkuu wake ni Belzebur.
Lucifer huwapa kazi za kufanya hawa hao mapepo, kila Siku.
Na wote hukaa angani, kila mmoja akikaa pande moja ya dunia ,yaani mashariki, kaskazini, magharibi na kusini, na kazi yao ni moja tu ni kuzuia Maombi ya watu Wa Mungu, Na wote wanakuwa chini ya Belzebur.
Huzuia Maombi, ndo maana unaweza kuomba Mungu miaka kibao bila majibu, Soma Daniel 10:13.
Malkia wao anaitwa Kilenzi, hili ni pepo hatari la kike ambalo ndo limeshikilia anasa na pesa zote za dunia hii.
Kilenzi linavunja ndoa za watu na kuharibu maisha ya vijana na mabinti.
Ni pepo haribifu la maisha ya watu, wote wanaotafuta Mali kishirikina, kilenzi ndo mgawaji wa hizo mali endapo tu utafuata masharti yao.
Kilenzi ndo waziri wa fedha na uchumi huko kuzimu.
Kati ya mapepo makuu yote, ni yeye tu ndo jike peke yake.
Mtu yoyote, akitaka chochote, iwe utajiri, Urais, Umaarufu, hata Kama hana elimu Lucifer humpatia kupitia kilenzi endapo tu, atatimiza masharti yao ambayo ni magumu mno.
Kila Siku saa 8 usiku ktk majira ya nchi zote duniani, mapepo hawa hushuka kutoka angani na kwenda kuzimu Kwa ajili ya kufanya sherehe na mikutano maalumu ya kuiangamiza dunia.
Inapotimia saa9:55 alfajiri, yanakuwa tayari yamemaliza kazi zao kuzimu na kurudi angani.
Watu wengi hawajui kuwa muda mzuri wa kuomba Mungu ni kuanzia saa 8:00 usiku hadi mwisho saa 9:55 alfajiri.
Maana kilenzi na wenzake wanakuwa kuzimu na hivyo kuliacha anga likiwa safi.
Kilenzi ndo pepo aliyeshikilia hadi serikali nyingi duniani. Soma ,Ufunuo wa Yohana. 17:1-8.

Jamani tukaeni jaribu na Mungu, Kwa leo naishia hapa, Siku nyingine nitafafanua zaidi.

Mmoja Wa mabinti aliye chini ya miliki ya kilenzi, Kama upo Kama huyu haha kwenye picha, basi wewe ni wa kilenzi, Nitafafanua zaidi.
 
We umejuaje haya
Huyu jamaa tapeli kama nini. Ametumia terminology za kwenye Biblia na kunukuu kamstari kamoja ili kuipa nguvu hoja yake mfu ambayo iko kinyume kabisa na Biblia.

Hizi ni hekaya hatari zinazolenga kuwapotosha watu tu! Hamna kitu hapo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom