Mfahamu Bibi. Titi Mohamed na issue ya kutaka kuipindua serikali

proxy.jpeg
 
Wanaume wote wenye hekima dunia hii ni wakware!Anza na king David,Solomon,Bill Clinton,Bob Marley, diamond platnumz(kidding). na wengine uwajuao...Huwezi kuongoza vizuri kama unajidai mgumu utaishia kuwa gaidi tu!'Kazi na dawa!'
🙏🙏🙏 Kweli mkuu kazi na dawa
 
Bibi Titi Mohammed alizaliwa mnamo 1926 jijini Dar es saalam na alipoteza maisha tarehe 5 Novemba 2000 alikuwa mmoja wa wanawake wa kwanza mzalendo kushika nafasi za ubunge na uwaziri nchini Tanzania. Pia alikuwa kati ya wanawake wa kwanza kujiunga na harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mwaka 1969 Bibi Titi Mohammed alikamatwa na mwaka uliofuata alifikishwa mahakamani kwa kosa la kula njama ya kutaka kupindua serikali. Katika kesi hiyo, Bibi Titi alikuwa ni mwanamke pekee katika washtakiwa 7. Baada ya kesi hiyo kusikilizwa alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha. Hata hivyo, mwaka 1972 alisamehewa na rais Julius Nyerere.

Juu ya kutolewa kwake, Mohammed aliongoza maisha yake akiwa mpweke. Mume wake alimtelekeza wakati wa kesi, ushirika wake wa kisiasa ukanyang'anywa, na marafiki zake wengi wakamlaani.

Mnamo mwaka wa 1991, wakati Tanzania ikisherekea miaka 30 ya uhuru, Bibi Titi ameonekana kwenye maandishi ya chama tawala kama "Shujaa wa Kike Aliyepigania Uhuru".

Tarehe 5 Novemba 2000 Mohammed alifariki kwenye hospitali ya Net Care Hospital mjini Johannesburg ambapo alikuwa akitibiwa.

Moja kati ya mabarabara makubwa ya jijini Dar es Salaam limepewa jina la Mohammed kwa heshima ya mafaniko makubwa aliyoyafanya wakati wa mbio za kutafuta uhuru wa Mtanzania.
Asante.
Lakini umekosa kapicha?
Basi tumia hizi...

Nyerere akimwapisha Karuma kama Makamu wa Kwanza wa Rais.JPG


Nyerere ktk Kongamano la Kikatiba 1961.JPG


Nyerere na Baraza la Kwanza la Uhuru.JPG


Nyerere na Kwame Mkrumah.JPG


Nyerere, Sophia, Bibi Titi na Maria Nyerere.JPG
 
Ahaaa nimeamua kuweka avatar ya banned ili wafurahi zaidi wamenipiga ban mbili ndani ya mwezi mmoja
Ndy maana nilishanga kitu kimoja Kuna Uzi mmoja ulichangia alafu Mimi nilikuwa active muda huo..nikasema huyu jamaa mbn naona kapigwa ban lkn anareply km kawaida? Nikakosa majibu
 
Back
Top Bottom