Mfahamu Afande Sele

Kamtukana Mungu anakamatwa na polisi, kwani huyo Mungu mwenyewe yuko wapi? Wanambeza mwehu, kumbe na wao ni malofa.
 
Afande Sele ni nani?

Seleman Msindi au Afande Sele (amezaliwa tar. 24 Aprili 1976) ni msanii wa muziki wa hip hop na Bongo Flava kutoka Mkoani Morogoro, Tanzania.

Amewahi kushinda tuzo ya (mkali wa ryhmes) mwaka [2003] kutokana na wimbo yake wa "Darubini Kali" aliyomshirikisha Dogo Ditto kwa sasa Lameck Ditto. Ni muasisi wa makundi ya 'Ghetto Boys' na 'Watu Pori', yaliozaliwa na kufia mjini Morogoro kwa kufuatana na alikuwa msanii wa kwanza kuujaza uwanja wa mpira wa miguu wa JAMUHURI mjini morogoro alipozindua albam yake ya kwanza ya 'MKUKI MOYONI'.

Aliongoza kampeni ya maleria mwanzoni mwamiaka ya 2005 na 2007. Mwanzoni wa mwezi wa 11 mwaka 2012 alitangaza rasmi kufanya kazi kama kundi jipya la watu pori baada ya kufanya kazi na MC KOBA ambaye ni miongoni mwa waliokuwa wakiunda kundi la watu pori miaka ya nyuma.

Ametoa Nyimbo nyingi kali ikiwemo MTAZAMO, Amani na Upendo, SIMBA DUME Na nyingine nyingi.Afande Sele kwa sasa ana video ya wimbo wake Soma Ule ambayo imeongozwa na mtayarishaji Raph Tz (upcoming video director) aliyepewa heshima na msanii huyo kufanya video hiyo ambayo imekidhi maudhui ya wimbo.

Huyo ndiye afande Sele wa Morogoro.

Duuuh sijaona historia yake na sugu hapa.
 
Kwa sababu za kiafande mkuu
Nakumbuka aliwahi simulia kwenye moja ya interview zake jina lilianzia shule ya msingi tatzo mm nae kichwa panzi sikumbuki vzr sijui alikuwa kiranja wa ulinzi sijui alikuwa na cheo gani ndipo wanafunzi wenzie wakampa jina la afande kutokana na harakati zake
 
Nakumbuka aliwahi simulia kwenye moja ya interview zake jina lilianzia shule ya msingi tatzo mm nae kichwa panzi sikumbuki vzr sijui alikuwa kiranja wa ulinzi sijui alikuwa na cheo gani ndipo wanafunzi wenzie wakampa jina la afande kutokana na harakati zake
Dah kumbe afande kweli
 
Hivi Kigulunyembe ni shule ya msingi? Maana jamaa amesoma hapo na kina Prof J.
Secondary, shule ya kanisa kubwa, wamesoma pale, wasanii wengi tu, na marehemu mama tunda alikuwa madarasan ya chini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom