Meza ya futari

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,810
MEZA YA FUTARI


Maghrib ilipofika, meza ya kufuturu ikajaa wapambe.
SAMBUSA alivyo mzuri, akatongozwa na BW MKATE WA TAMBI.

Kina MATOBOSHA wakamzoma "woooo umemkosaaa!! !"
"BW.KEBAB ashamposaaa! !!" Akaanza kulia kusikia kuwa ashachukuliwa.

VIAZI VYA MADONGE akamwambia, "na harusi itafanywa kwa khalle BHAJIA, siku
ya IDD mungu akitujaalia. "

Habari zikamfikia MKATE WA SINIA.Akamhurumia, akamwambia "Swahib!! acha
kulia."Penye nia hapakosi njia."Kama ni wazuri, kila mahali wameenea"!!
"kama wataka, nitazungumza na hababa KIBIBI, akuozeshe jirani yake aitwae
JELEBI."

Hababa KIBIBI akaruka..."LA! Muhindi yule atamtesa, kweli ni mzuri, lakini
apenda pesa. "Kwanini tusimuozeshe jamaa yetu KAIMATI?"Maskini mpaka sasa
hajapata bahati."Na ikiwa atakubali, mimi nitampelekea posa, kwa shangazi
yake Bi.KILOSA."

BW.MKATE WA TAMBI akaoona, yanini adhabu? yanini hii aibu?
"nimeamua nitamuowa cousin yangu TAMBI ZA ZABIBU."

TAMBI ZA PAPAYU akafurahishwa na hio choice, habari akazieeneza mezani
upesi. akajisifu .."mimi ndiye nitakaye isimamia hio harusi".Tutangoja ya
kina SAMBUSA ikipita, yetu tutaifanya baada ya sita."


Mjomba wa bw.harusi aitwae SPAGHETTI akasema "musijali mimi nitajitolea
Italian SUITE, BISCOTTI na CAKE ZA CHOCOLATIE."

KITUMBUA alipojua akasema.."Poleni, sitoiwahi hio harusi vile mimi ni mja
mzito, lakini nawaahidi keshani nitajitolea MAJI YA VIMTO."

"Ikiwa hio harusi mutaipanga kwa mpango."Akaruka nyanya TANGO. Mimi siku ya
lunch nitajitolea juice ya MANGO."

MSETO akasema kwa majuto. "Natamani na mimi usiku wa kesha nijitolee WALI
WA POJO, lakini watu washazowea MAHAMRI na VIAZI VYA ROJO."

Akaanza kujisifu tajiri mmoja aitwae MBOGA ZA KIBANIANI. "musitie
wasiwasi.... Mimi kutatoaa sufuria 10 za BIRIYANI.

Mchuzi wa KAMBA akajitolea hall la kupamba.
SPRINGROLL akasema "mimi najitolea kumpaka mkeo henna , na design
nitayomchora ni ya kichina.

Huku na huku, story zikamfikia councillor KUKU. "Ikiwa
watanialika, nitawaletea CHICKEN TIKKA. Kina sambusa watashikwa na homa,
wakisikia nawapelekea mapaja ya kuchoma."

Jamaa wakawa wana hamu akodishwe NDIZI ZA TAMU. Mwimbaji mzuri atokae huko
Lamu. "Ikiwa atakosekana. .mkodisheni VIAZI YA TAMU!!akatoa
wasia ICE-CREAMU.

LASAGNIA akasema "wala harusi yetu musivaeeni vitambara vya border, FALUDA
atawauzia sare rangi ya Powder.

CUTLESSI alivyo sabasi, akaanza kusengenya na MIKIA YA NGISI.
"Hmmm...si ajabu CHAPATI akavaa buibui, maana kila harus arepeat kanzu yake
ya chuichui."

HA! HA! akacheka SAMAKI WA KUPAKA. Kweli yule kanzu zake utafkiri zina
viraka.Kama ni mimi mutanichoka! Nguo zangu zatoka America.

"Kweeenda zakoooo!! Akamsutaaa.. .. MKATE WA UFUTA!!"Naskia wewe MBAAZI na
VIAZI VYA NAZI fundi wenu ni TUI la NAZI.

Wazee wa mji kina KAHAWA wakasema "Mupende musipende". Kadhi tutakao
waletea ni sheikh TENDE." Maana HALUWA amefanywa BALOZI! Na tangu
aongezwe mshahara wa LOZI, siku hizi atutilia pozi."

"Wacheni upuuzi!!!." Akawakemea NYAMA YA MBUZI."

Tena nyamazeni!!! Mwajitia madhambini!"
"Hamjui kua leo ni RAMADHANI?" "Hamuusikiii huo mwadhini?"
"Twendeni msikitini tukaswalini, tusitokeni taraweheni."
"Kwani hamuoniii? mpaka kesho jionii...sote tutakufa tuishie matumboni?





Nawatakia Ramadhani Njema

XP
 
tih tih teeeh, aaaah.
ila mkuu umentamanisha sana, dah.
keki za chokoleti, samaki wa kupaka Lol.
 
Back
Top Bottom