Meya wa Moshi kuingia darasani kufundisha wanafunzi na kumsifia Rais Samia mbele ya wanafunzi ni sahihi?

Nkerejiwa

Senior Member
Feb 25, 2014
146
214
Moshiblog Updates
flyerdesign_18012022_195441.jpg
MOSHI: MICHANGO YAPIGWA "STOP" MASHULENI, MEYA RAIBU AINGIA DARASANI KUFUNDISHA BIOLOGY

Moshi Kilimanjaro

• Meya Raibu apiga marufuku michango mashuleni, adai walimu wakuu waache watoto wa Rais Samia wasome bila bugudha
• Awaonya wazazi wasiopeleka watoto shule kujiandikisha, adai wasiogope, Rais Samia amekwisha lipa ada yote
• Awapiga msasa wanafunzi wa kidato Cha Kwanza


Mstahiki Meya wa Manispaa Ya Moshi Ndugu Juma Raibu akiwa katika ziara ya kutembelea Madarasa yaliyojengwa Kwa ufadhili wa Fedha za Uviko 19 amezungumza na waalimu na wanafunzi akifafanua faida kedekede za ujenzi wa madarasa hayo.

Meya huyo amedai tayari Kwa asilimia kubwa ujenzi umekamilika na Madarasa hayo yameanza kutumika na yamekuwa msaada mkubwa katika Manispaa hiyo.

Amesisitisa walimu wakuu kuacha mara moja kuwarudisha nyumbani watoto kwa kisingizio Cha michango kwani Rais Samia amekuwa akitoa bilioni 28 Kila mwezi nchini kote kugharamia uendeshaji wa shule za serikali. Namnukuu.

"Ndugu zangu walimu Kwanza niwapongeze Kwa kufanya kazi njema na bora sana ya kuwafundisha watoto wetu, lakini pili niwatake mwongeze bidii ili Manispaa yetu ipae zaidi na zaidi kielimu katika nafasi za kitaifa na tatu niwatake walimu wakuu kuacha mara Moja kuwarudisha mjumbani wanafunzi kisa michango kwani hela hizi zimeshalipwa na Rais Samia Kila mwezi Bilioni 28"

Lakini pia Mstahiki Meya huyo amewataka wazazi wote wa Manispaa hiyo kuwaleta na kuwaandikisha mashuleni watoto wote wanaopaswa kuanza shule za msingi na sekondari, kwasababu ni Elimu bila malipo. Namnukuu

"Watoto Waambie wazazi wote wawalete watoto waliobaki majumbani waje kupata Elimu ili iwe Mkombozi wa maisha yao na taifa Kwa ujumla na hivi sasa Elimu ni bila malipo kwani serikali ya Rais Samia inamaliza yenyewe Kila jambo"

Pia Meya amewataka wanafunzi hao kusoma Kwa bidii ili waje kulisaidia taifa siku za usoni, na Kwa msisitizo zaidi Meya huyo aliwafundisha wanafunzi wa kidato Cha Kwanza Somo la Baiolojia katika mada ya Utangulizi (Introduction of Biology).

MoshiBlog Updates
 
wamuulize kama Samia kalipa ada na michango yote. hii 70 wanayolipa form 1 boarding ni nini?
Wanachangia kidogo ya chakula mkuu.yaani watu wanalipa milioni 70 Ada kwa mwaka jamani kweli wewe unalalamika sabini kwa mwaka na huku usikute unahonga zaidi ya hiyo.haya bana hela za maendeleo zinatuuma Ila za party harusi hatuziulizii
 
Wanachangia kidogo ya chakula mkuu.yaani watu wanalipa milioni 70 Ada kwa mwaka jamani kweli wewe unalalamika sabini kwa mwaka na huku usikute unahonga zaidi ya hiyo.haya bana hela za maendeleo zinatuuma Ila za party harusi hatuziulizii
unapeleka maharage,mahindi,mchele halafu uachangia 70 ya chakula au sio?
 
Wizara ya Elimu popote mlipo , NAOMBA MKEMEE HIKI KITENDO HARAKA SANA KWANI NI KUDHALILISHA TASNIA YA UALIMU. HIVI KWANINI TUNARUHUSU HUU UJINGA UTAMALAKI? WIZARA YA ELIMU TOENI KAULI JUU YA HUU UJINGA.
 
Wizara ya Elimu popote mlipo , NAOMBA MKEMEE HIKI KITENDO HARAKA SANA KWANI NI KUDHALILISHA TASNIA YA UALIMU. HIVI KWANINI TUNARUHUSU HUU UJINGA UTAMALAKI? WIZARA YA ELIMU TOENI KAULI JUU YA HUU UJINGA.
Tulia wewe, wizara ipo chini ya serekali ya ccm, waziri ni wa ccm na meya ni wa ccm
Hata chama cha waalimu pia ni ccm!

Siiiisiem Hoye!
 
Back
Top Bottom