Meya wa Jiji la Mwanza (CHADEMA) asimamishwa kwa ufisadi

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765
Meya wa Jiji la Mwanza Josephat Manyerere wa CHADEMA amefukuzwa ktk nafasi yake leo na madiwani akituhumiwa kukiuka kanuni za uongozi kwa kushindwa kuiendesha vema Halmashauri yake.

Zimepigwa kura 20 za kumkataa na kura 8 tu ndizo zilizomtetea.

Siku kama 4 zilizopita alitakiwa na madiwani wa chama chake (CHADEMA) ajiuzulu kulinda heshima ya chama lakini akakataa.

Gazeti la Mtanzania la Julai 23 lilitoa taarifa ya Meya huyu kupewa siku 4 aachie ngazi

Habari kwa kirefu itafuatia
 
Kama hayo ni yakweli, kuna umuhimu wa kum-hoji Dr pia ili kujua ukweli na kama itadhihirika ni kweli itabidi nae awajibike!! Kwa upande mwingine, haiingii akilini kwa M/kiti wa CDM kuchukua hela ya serikali na kuipeleka kwenye chama wakati ma-signatory ni mkurugenzi na Mweka hazina wa wilaya ambao wote sio wana-CDM
 
cdm kumbe nao wachumia tumbo,ukomboz wa kwl utatoka wapi sasa?cdm inaanza kupoteza dira,watu wenu wameanza mapema je mkipewa nchi?wananchi waende wapi sasa?
 
Kama alikuwa fisadi wamefanya jambo la maana kwa nini ameshindwa kusimamia maendeleo?
 
Kama mji kuendesha kazi haya majitu nchi sindo wataiua kabisa nyambaf yaani haya majitu nimeyachukia kwa sababu ya mambo yao ya udini hasa humu ndani.
Mkuu hebu Funguka Majitu ni watu wenye vitambi vikubwa mafisadi ambao huwezi kuwa wajibisha ambao wengi wamejaa kwenye kile chama cha Mafisadi (CCM) sasa mbona ndio wmeshikilia nchi unataka kuwapa mara ya pili tena?
 
Kama kweli amefanya ufisadi na sasa ametemwa, basi hilo ni jambo zuri sana na kuigwa kwa nguvu zote. Kiini cha malalamiko ya wananchi ni tamia au mfumo wa kukaa kimya hata pale inapodhihirika kuwa mtu amefanya ufisadi.

Hatuongozwi na malaika lakini hii haiminishi kufumbua macho ubadhirifu wa mali ya umma. Lazima kila chama kiwe na ujasiri wanatakiwa wa kumchukulia mtu anayekwenda kinyume na utawala bora.
 
Chadema kinapinga na kupigana na ufisadi wa aina yoyote utakaofanywa na yeyote.

Ni kweli Manyerere ameharibu na madiwani wenzake wamemwajibisha, asilimia kubwa ya madiwani ni CDM,hivyo kusema CCM wamempiga chini si kweli.

By da way cash haishikwi na meya kiasi kwamba yeye apeleke makao makuu ya CDM.
 
Inawezekana ni kweli leo kulikuwa na kikao cha madiwani wa Jiji la Mwanza kuhusu kupiga kura kutokuwa na imani na Meya.
 
Tuondolee uongo asiyemfahamu nani? kashifa zake nyingi ni kuzidiwa kete na mabwepande kitu ambacho kililete malalamiko mengi kutoka kwa wananch ikiwemo hasa wakakti wa maandamano ya kupinga ongezeko la bei ya umeme ambapo wananchi walimwambia Dr. Slaa kwamba hawana imani naye, kashifa nyingine ni kuwasaliti wamachinga
 
Ni kweli meya wa jiji la mwanza mhe.Josephat Manyerere ameenguliwa leo kwa kupigiwa kura yakutokua na Imani nae..mimi mwenyewe nilikua maeneo ya jiji leo.

Mhe. Manyerere alikua na shutuma 11 ambazo madiwani wenzake both ccm nd cdm walitaka awe amejiuzulu ndani ya siku 4,ambazo ziliisha toka juma3 bt hakufanya hivyo, so wakaamua kupiga kura yakutokua na imani na meya,na column ikatimia
 
kama kweli amesimamishwa basi sheria ichukue mkondo hatuwezi kutetea ujinga na ufisadi hata kama yuko CDM hayuko juu ya sheria anatakiwa kuajibika kwa mjibu wa sheria za utumishi
 
Credit kwa CHADEMA. Madiwani wa CHADEMA ndio wengi na ndio walioamua kumwondoa Meya madarakani. Huu ndio utawala wa kidemokrasia na uwajibishwaji. Kinachotakiwa sasa ni mamlaka zinahusika kumchukulia hatua mara moja ikiwapo kumchunguza na kumfungulia mashtaka kwa kasi. Hongereni madiwani wa CHADEMA kwa kuonesha uongozi - hakuna kulindana hapa.
 
safi sana....

big up madiwani wa mwanza kwa kuonesha kwa vitendo namna ya kupambana na ufisadi

awe CDM au popote pale kama anatekeleza kinyume na matarajio ya wananchi then hakuna mbadala zaidi ya kumuwajibisha mtu.

Once again nawapongeza sana CDM........hii ndio demokrasia ya kweli
 
kumbe na huko pia wapo? Kazi tunayo mwaka huu

Chama
Gongo la mboto DSM
 
hawa nao ma..... tu,anayeila halmashauri ya mwanza ni wilson kabwe jamaa habanduliwi pale sijui kuna siri gani asee!!
 
Back
Top Bottom