Inasemekana huyu meya ana jazba na ni mtu anayependa sifa na ana uchu wa madaraka kweli. nilimsikia redioni nilipokuwa huko mwezi wa nne akiwaambia watu kuwa atavunja soko kuu la Bukoba na kulijega upya; sasa watu wakawa wanalalamika sana.Pale SENATE (KIJIWE KIMOJA CHA KAHAWA PALE SOKONI) kukawa na baadhi ya hoja zifuatazo;
1.Kwa nini hatukushirikishwa kama wadau kuanzia mwanzoni mwa mpango mzima mpaka inasubiriwa dakika ya mwisho ambapo tumekopeshwa na mabenki, tumelipa kodi tra tayari
2.Meya aliwaambia wananchi kwamba soko litajengwa la kisasa na kwamba litawekewa mnara,ili kuwavutia watalii, na kwamba hiyo ramani kaitoa nchi moja ya ulaya sasa swali je ni mzungu ataacha mnara kwao aje kuushangaa Bukoba?
3.Ilisemekana kwamba soko lina wafanyabiashara zaidi ya 1200 ambapo kila mmoja anategemewa na watu wasiopungua 4, sasa ukilibomoa maisha ya watu karibu elfu tano yatakuwa rehani.
4.Wanaunga mkono mipango ya maendeleo na soko lijengwe, lakini itafutwe sehemu nyingine mbadala kama stendi ilivyoamishiwa Kyakailabwa likajengwe soko hilo, isaidie kupanua mji na kuongeza ajira lakini ili libakie kuwahudumia watu wachini, kwani hata soko la kisasa likikamilika bado watu hawatamudu gharama mpya za pango i.e watakuwa wamekufa kabisa kibiashara na kimaisha
5. Kwa sasa Halmasauri inauza viwanja 5000 kwa wananchi, je imeshindwa kutenga eneo la kujenga soko la kisasa?
6.Uendelezaji wa mji wa kisasa si lazima kuharibu kilichopo kwa hoja kwamba
a.ofisi ya mkuu wa mkoa ya kisasa inajengwa nje ya mji kule kahororo na ile ya regional block imeachwa
b.nssf wameacha jengo lao la old airport road na kujenga jengo jipya la kisasa pale jirani na polisi
c. hata soko kuu la Mwanza halikuvunjwa badala yake limetafutwa eneo jingine kubwa maeneo ya Ghana
d. hata uwanja wa taifa haukuvunjwa badala yake ulijengwa mwingine pembeni
7. hoja yao kuu ni kwamba soko lifanyiwe ukarabati mkubwa ikibidi hata kwa awamu lakini isiathiri hali ya maisha ya wananchi ambazo tayari ni duni,
hayo niliyaacha mwezi wa nne sielewi hadi leo imefika wapi lakini inawezekana haya mambo pamoja na mambo mengine ya kisiasa maana kuna uhasama kati ya meya wa sasa na aliyekuwepo kabla kila mtu akitaka ashinde kwa upande wake ndani na nje ya vikao
8. vile vile meya anatuhumiwa binafsi kwamba alifanya utapeli wanafunzi wa form 4 mwaka jana waliokuwa kwenye sule yake ya sekondari ya peace aliwapeleka kwao karagwe wakafanye mtihani ili shule yake isionekane haikufaulisha vizuri, kwa bahati mbaya necta ikastukia deal na kuwafutia matokeo zaidi ya wanafunzi 80 (sina hakika nayo sana lakini nayo pia nliisikia) wazazi wanaangaika sasa.
KWA KWELI KUNA MALALAMIKO MENGI SANA.
NILIACHA WANAPANGA KWENDA MAHAKAMANI SIELEWI ILIPOFIKIA.
HIYO NDIYO BUKOBA NA UKIWEPO UNAWEZA KUSHANGAA,NI MENGI, NI ZAIDI YA UIJUAVYO.