Meya Raibu awarejesha darasani Waandishi wa Habari

Feb 7, 2019
41
45
WAANDISHI KILIMANJARO WARUDISHWA DARASANI

Ofisi ya Mstahiki Meya wa manispaa ya moshi Mhe Juma Raibu imeandaa semina ya kuwaongezea na kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa mkoa wa Kilimanjaro ili wawe bora katika tasnia hiyo.

Akiongea kwenye maadhimisho ya siku ya wanahabari yaliyofanyika mkoani hapa, ametoa wito kwa wanahabari kuzingatia maadili, kanuni na nidhamu ya taaluma hiyo ili kuepusha migongano isiyokuwa ya lazima, akiwahasa wanahabari hao kufuata misingi yote ya kiuandishi kabla ya kuwasilisha habari yoyote kwa maana tasnia hiyo ni kiungo muhimu kwenye jamii.

''Wapo waandishi wazuri sana lakini baadhi wako wengine wanaibaka tasnia hiyo Kwa aidha Kutokujua Au Sababu Ya Elimu Natoa Ofa Kwa Waandishi Wa Mkoa Kilimanjaro Kupigwa Brush na Malecturer wa Tasnia Yenu Ili Kuwajengea Uwezo"

Semina hiyo itaendeshwa na wakufunzi wa elimu kutoka vyuo vikuu hapa nchini ambao wamealikwa na Ofisi ya Meya huyo.

IMG-20210504-WA0035.jpg
 
Back
Top Bottom