Meya Mstaafu Arusha ashuhudia jiji kusaini Mikataba ya Ujenzi wa Barabara

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Halmashauri ya jiji la Arusha, imesaini mikataba miwili yenye thamani ya shilingi bilioni 5.35 kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami zenye urefu wa kilometa 3.9.

Mikataba hiyo imesainiwa na mkurugenzi wa jiji la Arusha Dkt,Maulidi Madeni ,Meya wa jiji hilo,Paulo Matthysen pamoja na Mkandarasi wa kampuni ya kichina ya Sinohydro anayejenga barabara hizo katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia sasa.

Akiongea Mara baada ya kusaini mikataba hiyo iliyoshuhudiwa pia na aliyekuwa meya wa jiji hilo ,Kalist Lazaro, dkt Maulid Madeni amesema kuwa ujenzi wa miradi hiyo ni pamoja na barabara ya Kisongo Bypass yenye urefu wa kilometa 1.7 inayojengwa kupisha eneo la uwanja wa ndege wa Arusha kupanuliwa.

Amesema mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.25 fedha ambazo zimetolewa na serikali chini ya Rais John Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo ili kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa Arusha.

Akiongelea mradi mwingine wa barabara yenye urefu wa kilometa 4.4 kutoka Murieti hadi Baypass ,Meya wa jiji hilo, Paulo Matthysen amesema kuwa mradi huo utagharimu kiasi cha sh,bilioni 4.1 na kwamba kukamilika kwake kutaondoa changamoto ya muda mrefu kwa wakazi wa eneo hilo.

Kwa upande wake Meya Mstaafu, Kalist Lazaro ambaye ni mwasisi wa miradi hiyo alisema kuwa anafurahi kuona miradi hiyo ikijengwa ,kwani kabla ya kuondoka katika nafasi ya uongozi, alishiriki upembuzi akinifu na sasa anajisikia faraja kuona miradi hiyo ikijengwa kwa kasi kubwa.

"Nashukuru kwa heshima niliopewa na uongozi wa jiji kuona miradi niliyoshiriki kuiasisi ikianza kujengwa kwa kasi chini ya usimamizi wa jiji la Arusha" Amesema Lazaro.

Mkandarasi wa mradi wa barabara hizo,kutoka kampuni ya china ya SnohydroLang Shang alisema kuwa kampuni yake inatarajia kukamilisha mradi huo kwa wakati ila kwa sasa wanakwamishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.

Amesema mvua zinazonyesha kwa sasa zinawafanya washindwe kuendelea kwa kasi kubwa hivyo wanatarajiwa iwapo mvua zitasimama wanaweza kukamikisha mradi huo kwa wakati.

Naye Meneja wa uwanja mdogo wa ndege wa Arusha(Arusha Airport) Mhandisi Elipid Tesha amesema mamlaka ya ndege nchini imetoa eneo la uwanja wa ndege ili kujengwa barabara ya kisongo Bypass yenye urefu wa kilometa 1.7 .

Amesema upanuzi wa uwanja huo utawezesha kuruhusu ndege kubwa zikiwemo za ATCL kutua na kuruka katika uwanja huo.

Ends








IMG-20200204-WA0043.jpeg
IMG-20200204-WA0046.jpeg
IMG-20200204-WA0042.jpeg
IMG-20200204-WA0045.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom