Meya Mbeya atangaza vita na CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Meya Mbeya atangaza vita na CHADEMA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mungi, Aug 14, 2011.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Na Thobias Mwanakatwe




  14th August 2011








  Mikutano ya hadhara inayoendelea kufanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Mbeya Mjini jijini hapa, imeanza kuwa mwiba mkali kwa viongozi ambapo Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga ametangaza kuwashitaki viongozi wa Chadema kudai fidia ya Sh. Bilioni 1.2 kutokana na kutumia mikutano yao hiyo kumdhalilisha.
  Kapunga alitangaza uamuzi huo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari na kudai kuwa viongozi wa Chadema wamekuwa wakitoa maneno ya kashfa na kejeli dhidi yake.
  Alisema ameamua kuchukua hatua ya kuwashitaki viongozi wa Chadema kwa sababu kauli za viongozi wa chama hicho ni za udhalilishaji na zimelenga kumuondolea utu wake kama kiongozi wa juu wa Chama cha Mapinduzi (CCM).
  Alisema Chadema katika mikutano yake iliyofanywa katika kata za Nzovwe, Majengo na Mwenge, viongozi wake wamekuwa wakimtukana matusi ya nguoni na hivyo amedhamiria kuwachukulia hatua za kisheria baada ya kuwasiliana na mwanasheria wake.
  ‘’Nitawashitaki viongozi wa Chadema waliotoa maneno ya matusi sikishitaki chama chao, wamedhalilisha utu wangu, wamenidhalilisha kama mjumbe wa kamati ya utendaji ya ALAAT, pia wamenidhalilisha kama Mwenyekiti na Mameya wa majiji yote nchini pamoja na familia yangu,’’ alisema Kapunga.
  Kapunga ambaye pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Mbeya mjini, alisema kuwa katika mikutano ya viongozi wa chama hicho wamekuwa wakidai kuwa yeye ni mpinga maendeleo na kwamba jambo hilo si la kweli kutokana na yeye kuhusika moja kwa moja katika mipango mbalimbali ya uendelezaji wa jiji la Mbeya.
  Aliongeza kuwa mikakati mingi ya maendeleo ya jiji hilo anatumia fikra zake binafsi na kuzipeleka katika kikao cha madiwani na kupitishwa na kutolea mfano ujenzi wa ukumbi wa mikutano ya Mkapa ambao alichukua wazo hilo alipokuwa nchini Cameroun ambako aliuona ukumbi wa kisasa.
  Alisema viongozi wa Chadema ndio wanaopinga maendeleo kwa kuwa wanazuia wananchi kuchangia maendeleo na kutolea mfano kuwa katika kata ya Mwakibete walihamasisha wananchi kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari kwa Sh.3000 kila mmoja ambapo hata hivyo wamekuwa wakitoa risiti ambazo hazitambuliwi na Halmashauri ya Jiji.
  Aidha Meya huyo alikanusha madai ya viongozi wa Chadema kuwa yeye anazuia kutangazwa kwa nafasi zilizoachwa wazi za madiwani ikiwemo Diwani wa kata ya Iyela ambaye alijiuzulu kwa kusema kuwa hadi sasa hajapata barua ya kujiuzulu kwa Diwani wa kata hiyo na kwamba hata hivyo mwenye mamlaka ya kutangaza nafasi hizo ni msimamizi wa uchaguzi.



  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

  Huyu Meya anapoteza muda wake bure. chadema hawakurupuki kutoa tuhuma yoyote dhidi ya mtu yeyote.
   
Loading...