Meya Jacob alivyomuokoa Marin Hassan (RIP) viwanja vya Jangwani

chuuma

JF-Expert Member
May 19, 2015
363
557
Nakumbuka ilikuwa Siku ya Uzinduzi wa Kampeni za Urais za CHADEMA katika Viwanja Vya Jangwani siku ya Jumamosi ya Tarehe 28 August Mwaka 2010.

katikati ya Hotuba Nzito sana na za Kusisimua za Viongozi Wa Chadema,Ilipofika zamu ya Tundu Antipas Lissu kusimama na Kuanza kuhutubia,hali ya hewa na Utulivu viliondoka Uwanjani hapo ambapo Kundi la Wafuasi na Wananchi waliokuwa wanafuatilia hotuba hizo walipanga kupiga kelele za "WAMEKATA"

Kwa Bahati Mbaya Viongozi Jukwaa Kuu hawakujua Maana ya "WAMEKATA" Kumbe Wananchi walikuwa Wanamaanisha kuwa TBC1 Wamekatisha Matangazo ya Moja Kwa Moja yaliyokuwa yanarushwa Kutokea Viwanja vya Jangwani.

Basi haikupita Muda wa dakika 5,Wananchi wale na Wafuasi wa Chadema wakawa Wanakimbilia lile gari ya Matangazo ya Moja kwa moja pale Uwanjani,ambapo gari hiyo aina ya "VAN" ilikuwa Upande wa Kulia Mwa Jukwaa Kuu na Kaskazini Mashariki Mwa uwanja.

Basi sisi tuliokuwa na Jukumu la Ulinzi tulikimbilia kuelekea upande uleule waliokuwa wanaenda Wananchii.

Nakukumbuka tulikuwa Matukio mawili,Moja ni Wananchi waliokuwa wanaisukuma ile gari ya Matangazo ya Moja kwa Moja ya TBC 1 kuipindua na tukio la Pili lilikuwa ni Wananchi Wanamkimbiza na kumgombani Marehemu Marin Hassan Marin,

Mimi binafsi nichagua kwenda Kumuokoa Marehemu,Matin Hassan Marin,Kwa Sababu kadhaa kwanza niliamini wale wa gari uharibifu wao usingekuwa na Madhara Makubwa kuliko hawa ambao waliamua kwenda kumgombania Marehemu ambaye yeye hakuwa na kosa kwa kuwa kwake Uwanjani na siyo kwenye Mitambo studio,Pili mimi na Marehemu tulifahamiana Kama Majirani wakati huo tukiwa tuanishi wote Ubungo Kibangu.

Pamoja nakufanikiwa kumuondoa na Kumkinga na hadha hiyo,Polisi waiokuwa Uwanjani walikuja kuongeza Nguvu kwangu pia na siyo kwenye gari ingawa hata sisi pia tuliguswaguswa kidogo lakini tulimtoa Salama Mikononi Mwa wananchi.

Nenda Buriani Marin Hassan Marin

Na Boniface Jacob
IMG-20200401-WA0182.jpg
IMG-20200401-WA0183.jpg
IMG-20200401-WA0184.jpg
IMG-20200401-WA0180.jpg
IMG-20200401-WA0179.jpg
 
Sijaelewa,...!!
Au huu ni Uzi wa kabla ya saa 4 asubuhi kusherehekea Fools Day?
Ina maana huyu nguli wa TBC Bwana Marin Hassan Marin keshatutoka?
Kama ni kweli, is't the deadly Virus or what?
 
Kwahiyo ulisubiri na pengine labda ulikuwa unaombea Afe kama si Afariki ili uje ' ujimwambafai ' hivi? Kwahiyo kwa ' kujimwambafai ' Kwako huku / hivi ndiyo Kura zako katika Chaguzi zijazo ambazo utazigombea zitaongezeka? Waswahili tuna taabu sana hakyanani!
 
Kwahiyo ulisubiri na pengine labda ulikuwa unaombea Afe kama si Afariki ili uje ' ujimwambafai ' hivi? Kwahiyo kwa ' kujimwambafai ' Kwako huku / hivi ndiyo Kura zako katika Chaguzi zijazo ambazo utazigombea zitaongezeka? Waswahili tuna taabu sana hakyanani!

Bora umejijua waswahili mlivyo sasa ww hii story imekuuma nini???kama siyo uswahili tu,mtu kuelezea alivyomsaidia mwenzie ndo inakuwa nongwa???


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom