Meya Ilala azuia wamachinga kuondolewa katikati ya jiji

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
14,228
Reaction score
40,715
meya+charles.jpg

Meya wa Ilala, Charles Kuyeko amesema wamachinga waendelee kufanya biashara mjini na wasibughudhiwe na mtu yoyote.

Kauli ya Kuyeko imekuja baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene kuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwaondoa machinga maeneo ya katikati ya jiji.

Hivi karibuni alipokuwa Mwanza, Rais John Magufuli aliruhusu wafanyabiashara hao waendelee kufanya kazi kati kati ya mji hivyo hata wa jijini hapa wanaguswa na kauli hiyo.
 
View attachment 389224

Ni jambo baya sana kuwatumia machinga katika siasa. Wamachinga waandaliwe maeneo ya kufanyia kazi na waondolewe katikati y jiji ili kufanya shughuli zingine za kiuchumi na kijamii kuendelea badala ya kuwatumia kujipatia umaarufu wa kisiasa.
 
Hawa vijana wanazungushwa leo huyu karuhusu kesho yule kawakataza kazi kweli kweli
 
Meya kaingia mkenge, labda kama bandiko halijamtendea haki ya alichokisema
...hili la machinga, ukipiga hata kura ya maoni kwa wakazi wa Dar, utajua, ni kiasi gani meya yuko mbali na watu wake!
 
Matatizo ya wamachinga yanasababishwa na mamlaka zisizo husika kuingilia mambo ya wamachinga....jiji lilipaswa kushughulikia suala hili.
 
Kwani tamko la rais kule mwanza juu ya machinga kuachwa mijini na wasisumbuliwe linaishia mwanza au linavuka mipaka mpaka dar arusha mbeya na kwingineko n dani ya Tanzania? Naomba kujua ukomo wa tamko hilo la mkulu....or else meya anatii agizo la presdaa
 
Ni jambo baya sana kuwatumia machinga katika siasa. Wamachinga waandaliwe maeneo ya kufanyia kazi na waondolewe katikati y jiji ili kufanya shughuli zingine za kiuchumi na kijamii kuendelea badala ya kuwatumia kujipatia umaarufu wa kisiasa.

Rais haja sema hivi, wewe Ni Nani sasa?
 
ili swala ni vyema uongozi wa majiji husika wakae watatue hili swala kwa muda mrefu na walitungie sheria zake vizuri ili liepuke matamko mana kila mwanasiasa analitumia ajuavyo yeye na kuacha wamachinga wasijue wamfuate nani
 
Raisi keshatoa ruhusa Machinga wasibughudhiwe, Meya yuko sahihi!

Halafu kila nchi duniani kuna machingas.

Hivi hawa wamachinga mnaowafukuza mmewaandalia mahali pa kufanyia shughuli zao?, sehemu ya kuwatosha?

Mbona Mwanza mnawaacha, au kwa Sababu dar iliwakataa CCM kwa hiyo serikali inataka kuwaadhibu machinga wa DSM?
 
Kwani kauli inayosimama ni ipi? Meya upo sahihi
 
Hawa vijana wanazungushwa leo huyu karuhusu kesho yule kawakataza kazi kweli kweli

Lile wazo la kufunga barabara chache kwa muda kuanzia saa 9 alasiri mpaka saa 2 usiku ili wapange bidhaa zao hapo liliishia wapi?
 
View attachment 389224
Meya wa Ilala, Charles Kuyeko amesema wamachinga waendelee kufanya biashara mjini na wasibughudhiwe na mtu yoyote.

Kauli ya Kuyeko imekuja baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene kuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwaondoa machinga maeneo ya katikati ya jiji.

Hivi karibuni alipokuwa Mwanza, Rais John Magufuli aliruhusu wafanyabiashara hao waendelee kufanya kazi kati kati ya mji hivyo hata wa jijini hapa wanaguswa na kauli hiyo.

hiyo hapo juu VS hii hapa Simbachawene: Watendaji jiji Dar ondoa machinga katikati ya jiji, Rais aliruhusu machinga wa Mwanza

ngoja nishike vizuri hapa furushi langu la visheti maana hii movie ni kama steringi anataka kuuawa vile...
 
Kutaka watu wafuate utaratibu nako kunahitaji kushirikiana na mameya? Rais alisema machinga wasibughudhiwe lakini hiyo haimaanishi wafanye vyovyote watakavyo bali pale wanapo fuata utaratibu wasibughudhiwe
sawa lakini hili liko chini ya jiji. rais na waziri wake wanapaswa kusaidiana na jiji na sio kujiamulia tu atakavyo....
 
Meya yuko sahihi! Haiwezekani iwe halali kwa machinga Mwanza kubaki katikati ya jiji ilihali wa Dar iwe haramu! Haiwezekani hata siku moja, hayo maagizo Simbachawene akatoe hayo maagizo huko Mwanza hapo ndo tutamwelewa. Isije ikawa kwa vile Dar iko chini ya UKAWA ndo wananchi wasumbuliwe na Mwanza kwa vile iko ccm ibakishe machinga katikati ya jiji!! Waanzie kwanza huko alikotolea maagizo mzee wa maagizo!!
 
Safi sana Meya Mh.Rais ndivyo alivyoagiza kwanini huyo Waziri anampinga Rais?
 
Back
Top Bottom