Meya atembea amejificha ndani ya gari Bukoba

Meya atembea amejificha ndani ya gari Bukoba

Nam...

Member
Joined
Nov 11, 2011
Posts
51
Reaction score
16
Siku chache baada ya taarifa kuhusu meya manispaa ya Bukoba kusema kuwa anakesha ofisini akibadili nyalaka, na hatimaye yeye mwenyewe kusikika akiongea kwenye chombo kimoja cha habari kwa njia ya simu kuwa yuko nje ya mji, amebainika leo kwenye gari akiendeshwa huku ameinamisha kichwa chini akiofia kuonekana kwani ameshasema yuko kwenye vikao, Dodoma, Shinyanga na Dar es salaam.

ameonekana leo kwenye gari ambayo namba zimewekwa siri akiendeshwa na kijana wake wa kazi huku akionesha wasiwasi ndani ya gari hiyo MITSUBISH rangi ya kijani, ambapo nimemgundua baada ya kufika kwenye BUMP moja katika barabara za manispaa na gari kunguza mwendo.

Najiuliza mengi hapa kwamba kudanganya umma hakuna mwisho? lakini ngoja tutazame kama kuna sintofahamu sasa itafahamika.
 
kwa nini haujamuuliza kama anaogopa kurudishwa kwa kuonewa kama wengine kule alikotoka? acha akamilshe shughuli za kiofisi maana nshomile wana majungu mengi ndiyo maana huo mji wa bkb ni kama umelogwa tu. nshomile ni watu wa ajabu tu! sifa wanataka lkn fitina kama nini! mtabakia kujenga dar es salaam wakati hata wengine hamna kibanda kijijini!
 
Tabu zote za nini si ajiuzuru tu, kwani atakufa...!
 
Wahaya kwa majungu hamjambo, sasa kwa uelewa wako ni nyaraka zipi anazoshindia ofisini akizibadilisha, umeya ni taasisi wala si mtu mmoja acha kutumika vibaya mkuu, yote njaa tu lakini!!
 
Mji wa bukoba autoendelea sababu ya majungu na wivu wa kijinga.
Watu mmezidi majungu na mnatumika.acheni meya apige kazi
 
Tabu zote za nini si ajiuzuru tu, kwani atakufa...!
Mleta Uzi ni wale wale wa mwendelezo wa Fitina chuki na uzushi, Meya alifika juzi mjini hapa kuhudhuria mahafali ya shule zake , mgeni rasmi alikuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Bw. Stanislaus Mabula, alishusha nondo kwenye Hotuba yake na kushangiliwa Sana hasa pale aliposema Kuwa wana KAGERA tuachane na tabia ya ubinafsi ,Fitina chuki na uzushi kwa mstakaballi wa MAENDELEO ya wana KAGERA na Tanzania kwa ujumla, vinginevyo historian itatuhukumu. Mleta Uzi Wenzio wako kwenye MAENDELEO wewe uko kwenye Fitina !!!!!! Kachukue buku 20 kwa jamaa , njaa mbaya Sana, kweli Adui mwombee NCAA
 
Back
Top Bottom