Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,313
- 148,954
Kupitia Mtandao wa X, Askofu Mwamakula amesema Kuna taarifa kuwa aliyekuwa Meya wa Ubungo, Boniface Jacob amenyakuliwa na defenda akiwa kikaoni Sinza, Dar es Salaam na haijulikani kapelekwa wapi. Sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito kama ni Polisi wamemchukua waseme maana huyo ni kiongozi wa jamii hawezi kunyakuliwa kama mwizi.
Soma Pia: Meya wa Manispaa ya Ubungo, Ndg. Boniface Jacob akamatwa na Polisi kwa mahojiano
UPDATES
Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikisema kada wake aliyekuwa meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob 'Boni Yai' amekamatwa na Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa Kinondoni, Mtatiro Kitwinkwi amesema hana taarifa.
Akizungumza na Mwananchi kamanda Kitwinkwi kuhusu sakata hilo amesema: “Hapana, sina taarifa.”
Taarifa za Jacob kukamatwa, zimeanza kusambaa mitandaoni dakika chache zilizopita leo Jumatano, Septemba 18, 2024 na kwamba amekamatiwa Sinza, jijini Dar es Salaam.
Mwananchi limemtafuta, Wakili wa Chadema, Hekima Mwasipu ambaye amesema yupo njiani kuelekea Kituo cha Polisi cha Osterbay.
“Ni kweli amekamatwa na polisi waliovalia sare na wengine wamevalia kiraia maeneo ya Sinza. Walikuwa na defender na tuna taarifa kuwa amepelekwa Osterbay polisi na mimi niko njiani nakwenda.”
===
Kwa mjibu wa Wakili Hekima Mwasipu, nikwamba Mhe. Bon Yai amekanatwa na Polisi na yuko Ostabei ofisi ya RCO, kwasasa simu zake zinachukuliwa kisheria kisha ataanza kuandikwa maelezo yake! Mliokaribu fikeni Obei fasta na barua za dhamana mkononi ili mahojiano yakiisha iwe rahisi kumwekea dhamana! Makosa anayotuhumiwa ni kusambaza taarifa za Uongo.
Boniface Jacob amekamatwa eneo la hotel ya Golden Fork, Sinza majira ya saa 11.09 jioni ambapo polisi 2 wenye uniform na 3 waliokuwa hawana uniform wenye silaha walifika hotelini hapo na kumkamata Kwa nguvu na kumpakia kwenye gari Yao aina ya defender
Katika kurupushani hiyo amechaniwa nguo na sasa OC CID wa Osyterbay amewataka Mawakili wetu kumpelekea nguo kituoni hapo! Tunaendelea kufuatilia taarifa za kina kuhusu tukio hili.
Polisi wa Osyterbay wanaelekea nyumbani Kwa Boni Yai muda huu kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake !
Hawajasema wanachoenda kukipekua.
Mawakili wetu wapo na wataambatana naye kuelekea kwenye upekuzi huo!
Soma: Jeshi la Polisi: Tumemkamata Boniface Jacob kwa makosa ya Jinai anayotuhumiwa nayo
Soma Pia: Meya wa Manispaa ya Ubungo, Ndg. Boniface Jacob akamatwa na Polisi kwa mahojiano
UPDATES
Akizungumza na Mwananchi kamanda Kitwinkwi kuhusu sakata hilo amesema: “Hapana, sina taarifa.”
Taarifa za Jacob kukamatwa, zimeanza kusambaa mitandaoni dakika chache zilizopita leo Jumatano, Septemba 18, 2024 na kwamba amekamatiwa Sinza, jijini Dar es Salaam.
Mwananchi limemtafuta, Wakili wa Chadema, Hekima Mwasipu ambaye amesema yupo njiani kuelekea Kituo cha Polisi cha Osterbay.
“Ni kweli amekamatwa na polisi waliovalia sare na wengine wamevalia kiraia maeneo ya Sinza. Walikuwa na defender na tuna taarifa kuwa amepelekwa Osterbay polisi na mimi niko njiani nakwenda.”
===
Saa 12:07 Jioni: Ameandika Yericko Nyerere
Kwa mjibu wa Wakili Hekima Mwasipu, nikwamba Mhe. Bon Yai amekanatwa na Polisi na yuko Ostabei ofisi ya RCO, kwasasa simu zake zinachukuliwa kisheria kisha ataanza kuandikwa maelezo yake! Mliokaribu fikeni Obei fasta na barua za dhamana mkononi ili mahojiano yakiisha iwe rahisi kumwekea dhamana! Makosa anayotuhumiwa ni kusambaza taarifa za Uongo.
Saa 12: 15 Jioni: Ameandika John Mrema
Boniface Jacob amekamatwa eneo la hotel ya Golden Fork, Sinza majira ya saa 11.09 jioni ambapo polisi 2 wenye uniform na 3 waliokuwa hawana uniform wenye silaha walifika hotelini hapo na kumkamata Kwa nguvu na kumpakia kwenye gari Yao aina ya defender
Katika kurupushani hiyo amechaniwa nguo na sasa OC CID wa Osyterbay amewataka Mawakili wetu kumpelekea nguo kituoni hapo! Tunaendelea kufuatilia taarifa za kina kuhusu tukio hili.
Saa 12: 30 Jioni: Ameandika John Mrema
Polisi wa Osyterbay wanaelekea nyumbani Kwa Boni Yai muda huu kwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake !
Hawajasema wanachoenda kukipekua.
Mawakili wetu wapo na wataambatana naye kuelekea kwenye upekuzi huo!
Saa 12: 40: Ufafanuzi wa Polisi
Jeshi la Polisi limekiri kumshikilia Boniface Jacob kutokana na tuhuma za Makosa ya Jinai zinazomkabiliSoma: Jeshi la Polisi: Tumemkamata Boniface Jacob kwa makosa ya Jinai anayotuhumiwa nayo