Message ya kugomea sensa


Mimi ni mkristo na ninawaunga mkono hawa wanaogoma kuhesabiwa kwa sababu niano ushahidi kuwa tayaro matokeo ya sensa yameashachakachuliwa kwa faidi ya CCM katika uchaguzi ujao 2015 kama yalivyochakachuliwa kwa faidi ya CCM katika chagzui zilizopita ikiwemo ule wa 2010. Binafsi mimi sensa iliyopita sikuhesabiwa licha ya kukesa nyumbani kwa wiki nzima nikiwangoja haoa wanaohesabu. Maokeo idadi ya watu waliotangazwa kuwepo DSM ilikuwa kichekesho kitupu
 
Embu waachen wenzenu, eh vipengere vya dini wameomba waeekewe wamepingwa. Sasa wanahesabiana mna lalama eeh.
 
Wewe unataka Liwe na kipengele cha dini Kama wanavyotaka wenzetu Waislamu ?
 

sijaiona msg hii,,,hata masjid kwetu hatujasikia,,,,,wala kuambiwa kuhusu that sms,,,kila kitu huwa tunaambizana msikitini kwetu....NI UZUSH TU,UTAJUAJE KAMA IMETUNGWA NA WAISLAM,,,,,????
 
Waislamu ni watu wa ajabu sana, Ok sensa imehesabu waislamu ni 87% what next? Barabara zitakuwa ni ten ways au mafuta yatashuka bei?
vyema unge comment kwa heshima bila ya kujumlisha waislam, hao waliotoa tamko hilo je wana ridhaa ya waislam wote? jitahidi kuwa na tafakuri zaidi kabla ya ku post madudu na kashfa kwa jamii nzima badala ya walengwa. ingekuwa wana ridhaa ya waislam wote wala kusingekuwa na mjadala kwa kuwa hata mh rais ni mwislam na angeiamuru tu hiyo tume ya sensa kuingiza hicho kipengele. pls kuwa makini zaidi
 
Wewe unataka Liwe na kipengele cha dini Kama wanavyotaka wenzetu Waislamu ?

mgumu kuelewa wewe????
Yeye anasema kugomea sensa ni sawa,,,maana haina tija hata kwa mtanzania wa kawaida,,,kwani sensa iliyopita alipoteza muda na hakuhesabiwa,,,,sensa hii ina tija kwa ccm(kwa mujibu wa maelezo take),so kugomea sensa hata yeye atagomea
 


Unaongea utumbo wa kondoo. Nchi hii haina dini na wala haindeshwi kidini ila watu wote wanazo imani za dini tofauti. ALshabab we
 
Ingekuwa nafuu kila mwenye akili angezingatia hili. SENSA si jambo lililoanzishwa kwa hisia. SENSA ni mkakati maalum wa kufanikisha kupata takwimu sahihi za watu kwa makusudi fulani.

SENSA YA WATU NA MAKAZI 2012 ina madhumuni yake ambayo kwayo bajeti imetengwa na mikakati imeandaliwa ili malengo yafikiwe.

Inapotokea leo watu wanakuja na madai ambayo wao wenyewe wanashindwa kuyaelezea yana maslahi yepi kwa kweli huu ni utoto. Ikiwa madhumuni ya sensa yameainishwa tangu awali, je madhumuni ya hili ongezeko la takwimu kwa misingi ya dini ni yapi?

Naona malumbano tu yasiyo na msingi lkn hamna aliye na hoja nzito ya kunishawishi nione umuhimu wa dini kuwa kipengele kwenye sensa zaidi ya ubishi tu wa kitoto wa kusema kwani kuna ubaya gani kikiwepo.

Labda niulize swali: Kwa kuwa kuwahesabu watu waliosimama kituo cha daladala hakuna ubaya, hiyo ni sababu tosha ya serikali kuwahesabu na kuweka kumbukumbu hata kama haina shida nazo kwa kuwa tu sio vibaya?

Tuacheni ujinga jamani. Hizi imani zenu zinanipa mashaka kama nia huwa ni zenu au mmetumwa. Tuna mambo mengi yenye kututatiza kama jamii ambayo yangehitaji nguvu yetu ya pamoja kuyakabili lkn baadhi yetu tupo bize na mambo yasiyo na tija kwa hisia za uduni na matakwa wa matajiri fulani wanaotutuma.

Najua litasemeka vibaya lkn ni ukweli. Vuguvugu zinazohusisha dini ya Kiislamu sidhani kama zina mantiki, hata kule Zanzibar (Juzi nilimuuliza Zomba mara kadhaa akawa anakwepa swali langu na kuleta kejeli na visingizio visivyo na maana). Nani anawatuma hawa viongozi wa BAADHI YA WAISLAMU na anawatuma kwa malengo yapi na kwa faida ya nani?

Zanzibar imetiwa msukosuko kwa kisingizio cha KUTAKA UHURU WA ZANZIBAR, lkn nikauliza swali; Ikiwa shida ni UHURU wa Zanzibar, mbona harakati zinafanyikia misikitini na kwenye majukwaa ya dini ilhali jambo hilo ni la kisiasa? Je Wazanzibari ambao si Waislamu watashirikije kwenye harakati za kuikomboa zanzibar yao ikiwa majukwaa hayo hayo yanayoitwa ya Ukombozi wa Zanzibar yanatumika kuwatukana?

Siku Pemba ikianza kudai UHURU wake kutoka UNGUJA, harakati zitafanyikia misikitini au Pemba? Zitawahusisha waislamu au Wapemba?

Hapa utagundua kuwa kuna namna nyuma ya kila movement inayohusishwa na Uislamu wa Tanzania. Kuna watu wana agenda zao na sasa wanatafuta support ya watu na walipoona rahisi kufanikisha hili ni ktk dini ya Uislamu.

Nashangaa tofauti hii kati ya watu na tamaduni zao. Wapo wanaokasirika endapo wanafanywa wajinga na kutumika ku-serve purpose za kisiasa za watu wengine at the same time wapo wanaoona fahari kutumika kwa mtindo huo huo hata wakawa tayari kujitia msukosukoni na maisha yao kuharibika kwa jambo ambalo mkiulizwa mmoja mmoja, majibu wengi watakosa.
 
Ye yote anayemsingizia Mungu ndiye atapata malipo halali akhera!
 
muislam mwenye akili timam hawezi kutii meseji hyo iloyotolewa na watu wenye mawazo mgando na fikra finyu la kuleta mpasuko wa kidini nchini mwetu tuwakatae na mawazo hasi na yakupotosha.
 
muislam mwenye akili timam hawezi kutii meseji hyo iloyotolewa na watu wenye mawazo mgando na fikra finyu la kuleta mpasuko wa kidini nchini mwetu tuwakatae na mawazo hasi na yakupotosha.
Nasikia wameshaanza kufanya sensa Yao
 

Kwa hiyo ungependa na sisi ifike wakati fulani tuwe na Kashmir yetu kama ilivyo India? Acheni ushabiki wa mambo yasiyo na tija mtawaachiaa watoto wenu balaa siku zijazo.Kuingiza vipengele vya dini na kabila kuna chance ya mgawanyiko kutokea kutokana na tofauti za dini/kabila lakini kuondoa vipengele hivyo hakuna madhara yeyote katika nyanja yeyote!! it's as easy as ABC,tafakari!!
 

Kaka nimekusoma na nimekuelewa vyema, mimi binafsi nimekubaliana na ushauri wako kwa serikali, japo kwa upande wa viongozi wa kiislam umewaonea kwa kudhani kuwa wamewahi sana kutumia nguvu kitu ambacho si kweli, sema tatizo la media zetu huegemea upande mmoja katika kutoa taarifa zilizopo katika jamii, waislam walitoa mapendekezo yao na wakafata taratibu sitahiki na serikali ikapanga kikao cha kukutana na viongozi wa dini zote matokeo yake serikali hiyo hiyo ikawapiga chenga viongozi wa kiislam na ikafanya mkutano na viongozi wa kikristo pekee, viongozi wa kiislam walipohoji wasira akawajibu kwa dharau sana kuwa eti tuliwaita na nyie hamkuja, pamoja na hayo yote viongozi wetu hawakukata tamaa waliwasiliana na serikali kukawa na kikao kingine kilichofanyika dodoma na ndio wawakilishi wa serikali hawakutumia busara katika kujibu hoja zilizowasilishwa mbele yao.

Ama sehemu niliyo bold ni kwamba uko sahihi kabisa kuwa wakristo wako fiti ktk mipango na hii usiione kama mshangao sana bali jua huo ni unyonyaji ambao ulipangwa na baadhi ya waumini wa kikristo waliokuwa na nafasi za juu serikalini za kuwawekea pekee wakristo MoU ambapo kila mwaka serikali inalazimika kuchota billions of money kuwapa wao wajiendeleze hali ya kuwa jamii nyingine inaachwa nyuma, hiyo ndiyo sababu kubwa. Pia kuhusu wakristo kufanya sensa ni sahihi inawezekana ila tatizo lilipo ni kwamba kwanini wanapo weka takwimu zao huweka pia na za waislam? ivi unaweza kuniambia lini waliwahesabu waislam? Mwisho napenda kusema kuwa uvunjifu wa amani unaweza kutengenezwa na serikali kwa kuachilia upande mmoja ukafanya vile wapendavyo na serikali ikafata na kuacha upande mwingine wa jamii ukinung'unika kwa kutokutendewa haki, suala la wakristo kutoa takwimu za watanzania kwa mujibu wa dini zao na serikali isitoe tamko juu ya hilo hakika ni kukosea. Kuna takwimu ambazo huwa ni image na Nation si sahihi kila mtu ajifanyie sensa kwani utakosa report iliyo sahihi.
 

Mkuu Pasco naanimi akili unayo, naomba uitumie. Si kila ambacho si kibaya kufanywa basi kina maana. Eti kwa kuwa kucheka si vibaya basi sasa tukae chini na kucheka mchana kutwa kama wehu, kisa; KUCHEKA SI VIBAYA!

Kufanya SENSA ya wanyama kulikuwa na lengo na bilashaka hata ukiwa punguani huwezi kuomba au kumuamuru (kama wanavyofanya hawa wenzetu) aliyekuja na SENSA yake ya wanyama aongeze kipengele kwenye dodoso cha kuorodhesha ni wanyama wangapi wameng'oka meno.

Sensa ya WATU na MAKAZI imekuja ikiwa na msingi na malengo yake. Yanatambulika na yanajieleza. Mfanya SENSA (serikali) amelenga kupata takwimu zitakazomwezesha kufanya A, B na C, sasa leo unapokuja na suala la alterations kukiwa kumebakia miezi michache kabla ya sensa na sababu ikawa ni SI VIBAYA kuhesabu dini hii ni akili kweli?

Mnaonaje nyie wenye kutaka dini zenu zihesabiwe mngesubiri sensa nyingine ya wanyama, halafu mumuombe huyo mwenye sensa awahesabu watu wa dini yenu?
Naendelea kuuliza. kuna ubaya gani kujua?

Na mimi naendelea kuuliza, kila ambacho si kibaya kifanywe hata kama hakina malengo?
 
Last edited by a moderator:

kuna jambo!!
mkitaka kujua waislamu wako wangapi, kila mtaa una msikiti. Mhesabiane ninyi huko. Wengine hatutaki, serikali yenyewe waislam, kuanzia huyo no1, 2, nk. Sasa mnashindwa nini, acheni muone vitambulisho vya kitaifa mtapataje. Hatutaki BOKOHARAM hapa.
 

Mkuu Mr.Mak, kuna mambo ambayo ukitaka maisha yako yawe ya amani basi usiruhusu hisia zikaingia huko. Umekiri kuwa Wakristo wako FIT kimipango, lkn hapo hapo unaingiza hisia mbovu kuwa ni matokeo ya ukandamizaji dhidi ya Waislamu unaofanywa na Wakristo kupitia serikali. Haya ndio makosa yenu ya kuongozwa na hisia na kuukimbia ukweli.

Angalia mfano uliotoa; MoU. Mara ngapi mmeelezwa MoU iliandikwa kwa sababu gani? Hata Rais aliwaambia kwenye baraza la Iddi Dodoma, lkn kwa kuwa kuna ambacho mmedhamiria kuamini na mmelishana chuki kiasi mmepofuka kamwe hamtokuja kuelewa mnajikwaa wapi.

MoU haikujenga uimara wa Wakristo, bali uimara wa kimipango wa Wakristo ulipelekea Serikali kufikia sehemu ikaanza kutegemea huduma zinazotolewa na Taasisi za Kijamii za Kikristo. Unaposema serikali inatoa fedha kwa Wakristo na kuiacha nyuma dini nyingine, huu ni upotofu. Hebu niambie jinsi MoU iliyoandikwa 1992 ilivyoweza kuweka JIWE la MSINGI wa ujenzi wa Hospitali za BUGANDO, KCMC, TEULE (Muheza), NDANDA na msururu wa shule ambazo serikali ilizitaifisha kutoka kwa Kanisa.

Unawezaje kusema MoU iliyoandikwa 1992 imejenga miundombinu ya tangu mkoloni? Tumia busara na akili yako vyema mkuu, MoU ni katika kuwapunguzia gharama wananchi wanaotumia facilities hizo. Ndio maana hizi Hospitali na Zahanati zenye kupokea ruzuku gharama zake ni sawa na hospitali za serikali. Na huo ndio msingi wa MoU na sio kuanzisha. Rais aliwaeleza, hata nyinyi mkianzisha huduma za jamii mtapewa ruzuku. Sasa badala ya kuingia kazini mko bize kulalamika na kutaka mfanyiwe kila kitu. Mwarabu aliyewaletea dini, hakuwa na utaratibu wa kuwajibika na nyinyi mnaurithi.

Mkuu, zile hospitali ni za kanisa. Zinapewa ruzuku kwa sharti kwamba uratibu na uendeshwaji wake utafanywa na serikali kwa manufaa ya wananchi. Kama hujaitembea Tanzania ukaishia Buguruni ulikozaliwa ni rahisi kuropoka chochote unachojisikia lkn kama ungeijua Tanzania kama wanaoishi vijijini ungekuwa na busara zaidi kuhusu MoU.
 
Last edited by a moderator:
Kuna mtu nilimuuliza kuhusu hicho kitu lakini sikupata majibu. Ni lini na kiongozi yupi wa Kanisa alitoa hizo takwimu? Tungependa kuziona hapa au kama hamnazo mtoe maelezo ya kueleweka.
 
... Msg haichochei kitu isipokuwa ni taarifa ya kiimani inayowahusu waislam, ...
Aisee, kurani bwana, kumbe inakataza kuhesabiwa!! Mbona sensa nyingine walihesabiwa?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…