asakuta same
JF-Expert Member
- Mar 1, 2011
- 14,829
- 5,040
Kumekuwa na tabia ya watu au kikundi cha watu kwa malengo wanayofahamu wenyewe kutenga meseji za uzushi kuwatisha watu na kuzisambaza kwenye mitandao ya simu.... kwamfano walianza na meseji ya kuwazimisha simu watu usiku wa saa sita (tarehe nimesahau) kuwa kutatokea migongano ya kimionzi ,kama mwezi mmoja uliopita tena wakawatumia tena watu namba wakidai ni ya freemansoon na leo nimepokea meseji kwenye simu inasema "ukitumiwa pesa na mtu usiyemjua kwenye mpesa, tigo pesa, aun airtel money au mtandao wowote usiitoe. kuna mtu katumiwa 100,000 na mtu asiyemjua kukosa utulivu kaenda kutoa baada ya kutoa kapata sms (Asante kwa kujiunga na freemansoon). kwa upendo wako watumie wote unaowajua. si uongo bali ni habari ya ukweli"
huu uzushi unaleta sintofahamu kwa jamii na zaidi kwa watu wasioweza kuchambua kipi ni kweli na kipi ni uzushi ,kawaida mimi huwajibu huo ni uongo mkubwa sana.
sasa najiuliza ,wanaotunga huu uzushi/uongo ni kina nani?
wanafaidika na nini?
ni nini malengo yao?
hawaoni wanaleta usumbufu usiokuwa wa lazima?
karibuni wadau na nyie mchangie ........
Japo sikubaliani na uzushi huo lakini hili suala la kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemfahamu ukakimbilia kutoa ni tamaa kama siyo wizi. Wengine wanakosea namba bila wao kujua ukikimbilia kutoa ni kama vile umetapeli.
Some people are simply lunatics...huwezi wabadilisha!!!
Mimi napingana na uzushi huo lakini vile vile napingana na tabia ya simu yako kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemjua ukakimbilia kuichukua.tatizo ni kwanini uanzishe uongo na kusisitiza watu wausambaze mkuu?
Mimi napingana na uzushi huo lakini vile vile napingana na tabia ya simu yako kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemjua ukakimbilia kuichukua.
Mimi napingana na uzushi huo lakini vile vile napingana na tabia ya simu yako kupokea pesa kutoka kwa mtu usiyemjua ukakimbilia kuichukua.
Je unapotuma pesa huwa haionjeshi kuwa inakwenda kwa nani kabla haujathibitisha? Au ikishakwenda huwa haitumi sms kuwa fedha zimetumwa kwa so and so? Au ukituma pesa haupigi kwa unaemtumia ku check if its received. Labda kama unamtumia hawara haraka haraka na upo na wife unashidwa kuhakikisha namba.
Kama unajua umekosea namba si unatakiwa haraka kumpigia ukiemtumia kumuomba msamaha kisha kufanya proces ya kuzirudisha?
kaka mkubwa amini hizi ni mbinu za makampuni ya simu, kunajamaa yangu aliwahi niambia kuwa kuna kuwepo na watu kadhaa wenye uwezo wa kutunga msg zenye mvuto kisha zina sambazwa kwa wateja japo watano tu. na msg itakayo soma zaidi kwenye sistim basi mtunzi anapewa kitita chake. kwa kawada msg 1 ni sawa na tsh 40 mpaka 60
embu tupige hesabu kwa kutengenza mzunguko wa japo laki moja tunaweza kupata sh'ngapi.???
inabore sana eti. unaweza kuzima simu ukakosa deal za maana. i hate that so much. tatizo ni kuwaaminisha watu ishu zizizokuwa na ev
idence
kaka mkubwa amini hizi ni mbinu za makampuni ya simu, kunajamaa yangu aliwahi niambia kuwa kuna kuwepo na watu kadhaa wenye uwezo wa kutunga msg zenye mvuto kisha zina sambazwa kwa wateja japo watano tu. na msg itakayo soma zaidi kwenye sistim basi mtunzi anapewa kitita chake. kwa kawada msg 1 ni sawa na tsh 40 mpaka 60
embu tupige hesabu kwa kutengenza mzunguko wa japo laki moja tunaweza kupata shngapi.???
hilo hata mimi nililisikia ,ila najaribu kuangalia inaingiza faida vipi kwenye makampuni ya simu mkuu?
kwenye vocha mkuu hapo vocha hutembea sana hasa ukute zile msg za ki-imani wanasema tuma msg hii kwa watu kumi na usipo fanya hivyo yatakupata kama yalivyompata ....... nk ..nk
hapo hapo kwenye mia tano,kama hauna hiyo mia tano katika simu huoni inaweza kukusukuma kwenda kununua vocha ili ufoadi hiyo msg.???siku hizi mia tano inatosha kukupa meseji zaidi ya mia mitandao yote
Msg kama hizo zinaweza kuanza kwa utani tu.
Zamani kidogo kuna mtu aliwahi anzisha rumor,
just to see how long it takes for it to come back to her.
Alianzisha message ya kuita maandamano, usiku saa mbili
kesho yake asubuhi akapokea msg kualikwa maandamano
Messages zingine zinaanzishwa kwa propaganda tu,
kama zile za kuchochea udini au uchochezi wa vyama
Zingine ni ujinga tu, ndio kama hiyo.