Mental Toughness

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
735
1,464
MENTAL TOUGHNESS SECRETS OF THE WORLD CLASS by Steve Siebold


CHAMPIONS EMBRACE RELATIVITY
MABINGWA WANAAMINI KWENYE KUTEGEMEANA KWA VITU

Waliofanikiwa wanafahamu kuwa mitazamo yote inategemeana na mazoea na imani ya mhusika. Na hii ndio sababu Waliofanikiwa wanapenda kuwa karibu na wale wanaofikiri na kutafakari makubwa kuliko wao. Imani na matarajio huwa yanaambukiza na Waliofanikiwa hujua jinsi ya kuzitumia fursa hizo - Steve Siebold

Wengi tunaweka thamani ya vitu kutegemeana na mtazamo yetu binafsi kuhusu vitu hivyo.
Waliofanikiwa wao wanajua jinsi ya kupambanua fikra zao. Wakijua vitu vinategemeana. Unaposema kitu ni kikubwa au kidogo, wanakuuliza unalinganisha na nini?

Waliofanikiwa wao wanapenda kuweka kiwango cha juu katika utendaji bila kuwa na mtu wa kuwasimamia. Wanaweka viwango vya juu kabisa ukilinganisha na walivyo wao. Na wakishaweka viwango hivyo wanapata nguvu ya kufanikisha chochote wanachotaka.

Kutafakari kwa kina kunaondoa hofu na kunainua hatua za matarajio.

Usidharau hii siri maana ina uwezo wa kubadili mtazamo wako kwenye kila eneo la maisha yako.

Hatua ya kuchukua hapa:
Hebu wasikilize watu walio karibu nawe na uone ni jinsi gani wanapima vitu kulingana na mitazamo yao binafsi.

Wakipima kitu na kukitambulisha kuwa ni kikubwa au kidogo waulize wana kilinganasha na nini?

Jaribu na uone matokeo utakayopata.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom