Mennonite yahimiza watu kujiunga Vicoba

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,223
1,671
Dar es Salaam. Askofu Mkuu wa Kanisa la Mennonite Tanzania, Stephen Mang’ana ametoa wito kwa Watanzania kuwekeza kwenye vikundi vya kuweka na kukopa (Vicoba), ambavyo alivitaja kama nguzo ya kuwakomboa na lindi la umaskini.
Akizindua Umoja wa Vicoba (Uvinya) Kanisa Mennonite Kitunda, Kata ya Nyantira, Askofu Mang’ana alisema Vicoba ni gari linaloweza kuwatoa Watanzania kwenye lindi la umskini.
“Ili tufike hatua hii, inapasa jamii kutumia nguvu kuanzisha Vicoba vingi zaidi. Waumini wa Mennonite mnapaswa kuwa mstari wa mbele kwa jambo hili,” alisema Askofu Mang’ana.
Askofu Mang’ana alisema Vicoba vitasaidia waumini wa Mennonite kuongeza kipata chao kwa kulipia ada za watoto, kugharimia matibabu ya familia na mahitaji mengine.
“Maisha ya muumini wa Mennonite yataboreka, ustawi wa kanisa utaboreka na hata uchumi wa taifa utaimarika na kuongezeka maradufu,” alisema Askofu Mang’ana.
Alipongeza wanachama wa Vicoba wa Nyantira kwa tabia ya uaminifu kwenye marejesho ya mikopo kwa umoja wao wa Uvinya na kwamba, uadilifu ndiyo msingi utakaodaidia vikundi kuwa endelevu na kuongeza pato la wanachama.
Awali, Katibu Mkuu wa Uvinya, Jackson Mbasa alisema mafanikio makubwa yamefikiwa na umoja huo tangu ulipoanzishwa miaka mitano iliyopita na kwamba, Vicoba 342 chini ya umoja huo, vimekopa Sh424,064,120. Alisema hali ya urejesha mikopo ni mzuri.

Katika uchangiaji huo, mfanyabiashara Chacha Kigula alijitolea kusomesha watoto wote yatima wanoatunzwa na Kanisa la Mennonite, eneo la Nyantira, kwa kuwalipia ada, sare na vifaa vya shule kutoka shule ya msingi hadi elimu ya juu.

CHANZO: MWANANCHI
 
Back
Top Bottom