Mengine yaanikwa kampuni ya Bakhresa

Mengine yaanikwa kampuni ya Bakhresa

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803

Alhamisi, Mei 02, 2013 08:12 Na Mwandishi Wetu


SIKU chache baada ya wafanyakazi wa Kampuni ya Said Salum Bakhresa, kutoa malalamiko kuhusu unyanyaswaji wanaofanyiwa , tuhuma nyingine zimezidi kuibuliwa. Tuhuma hizo zinakihusu kiwanda cha kutengeneza mikate kilichopo eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam. Wakizungumza na RAI wafanyakazi hao na wengine ambao wamedai kufukuzwa kazi kwa ajili ya kutetea maslahi yao walisema kiwanda hicho kinaendeshwa kibabe.

Walisema Meneja wa Azam Bakeries, Suleiman Mbacha, ndiye kinara wa unyanyasaji huo huku wakidai kuwa mmiliki wa kampuni hiyo (Bakheresa), hana tatizo.

“Tatizo ni kwamba Mbacha anajua kuwa hatuna uwezo wa kuonana na tajiri (mzee Bakhresa) mwenyewe ndio maana anakuwa anafanya maamuzi kama anavyotaka yeye,” alisema mfanyakazi wa zamani wa kampuni hiyo, Mustafa Said.

Kijana huyo aliyefanya kazi kiwandani hapo kwa zaidi ya miaka saba, alisema ajira yake ilikoma ghafla siku chache baada ya Bakhresa kutembelea kiwandani hapo mwaka jana.

“Alipokuja aliitisha mkutano na tulimweleza wazi kwamba mishahara na posho tunazolipwa ni ndogo sana. Mwenyewe aliliona tatizo hilo, pale pale akaagiza kuwa vibarua wapandishiwe posho kutoka Sh 4,500 kwa siku hadi Sh 6,000, na sisi tuliokuwa tukilipwa Sh 150,000 kwa mwezi akasema tulipwe Sh 200,000,” alisema Mustafa.

Mustafa alieleza kuwa baada ya agizo hilo vibarua waliongezewa posho siku hiyo hiyo isipokuwa yeye na mfanyakazi mwingine Salum Penza ambao walionekana kuwa vinara wa hoja hiyo.

Hata hivyo alisema baada ya kutokea hali hiyo walilazimika kumuona Mhasibu Yusuf Baalawi, na kuhoji sababu ya kutoongezewa mishahara, ndipo walipojibiwa kuwa meneja yaani Suleiman Mbacha amekataa kuidhinisha.

“Meneja aligoma kwa makusudi kwa kuwa eti tulikuwa na kiherehere na matokeo yake akaanza visa hadi akatufukuza kazi,” alisema.

Kwa muda wote aliofanya kazi kiwandani hapo Mustafa hakuwahi kuingiziwa fedha kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Pamoja na malalamiko hayo Mustafa alisema kampuni hiyo ilikuwa imemfungulia akaunti mbili za malipo ya NSSF, jambo ambalo linamshangaza.

RAI ilishuhudia kadi hizo za NSSF Tawi la Temeke zenye namba 37 543 326 iliyofunguliwa Agosti 2, 2006 na nyingine 38 328 313 ya Machi 30, 2007.

“Nilipofukuzwa kazi nilikwenda NSSF nikaambiwa kuwa kadi ya kwanza haitambuliki kwa hiyo haikuwa na michango yoyote isipokuwa kadi ya pili. Kwa maana hiyo miaka minne ya kwanza nilifanya kazi bure bila michango yangu kuingizwa NSSF.

Mustafa alisema kwamba ameamua kuyaweka hadharani madhila yanayowakumba wafanyakazi wa kiwanda hicho chini ya meneja huyo ili kuwasaidia wafanyakazi wanaoendelea kufanyakazi kwenye kiwanda hicho.

Alipotafutwa Mbacha ili azungumzie tuhuma hizo, alikanusha kila kitu na kudai kuwa rekodi sahihi za wafanyakazi pamoja na mambo mengine zipo kwenye Idara ya Uongozi (administration) ya kiwanda.

“Ni uzushi mtupu. Ninakushauri uende utawala na kuuliza, utapata ukweli wa mambo,” alisema Mbacha.

Wafanyakazi wengine ambao majina yao (tunayahifadhi), wamemuomba mmiliki wa kampuni hiyo kuyafanyia kazi malalamiko ya wafanyakazi ili kurejesha amani ambayo inazidi kutoweka kiwandani humo.

Wiki mbil zilizopita, wafanyakazi wa kiwanda hicho walifika kwenye ofisi za RAI kulalamikia unyanyasaji wanaotendewa na uongozi wao.

Miongoni mwa malalamiko yao ni maslahi duni na manyanyaso wanayoyapata kutoka kwa viongozi hao, huku wakiwapendelea zaidi wageni hasa kutoka Kenya na India.

Wafanyakazi hao walisema hali wanayokumbana nayo kazini kwao si ya kuridhisha na kuomba msaada kwa serikali.

Mmoja wa wazee waliofanya kazi kiwandani hapo kwa zaidi ya miaka 15 alisema pamoja na makubaliano ya mshahara wa Sh 150,000 walioafikiana na uongozi, huambulia Sh 80,000 tu kwa mwezi bila kuambiwa makato yake yanapelekwa wapi.

Mbali ya wafanyakazi hao malalamiko hayo pia yametolewa na madereva wanaosambaza mikate maeneo mbalimbali jiji hilo.

Wakati Watanzania hao wakikumbwa na dhahama hizo, uongozi wa kiwanda hicho unadaiwa kuwaajiri raia wa kutoka Kenya na India na kuwapa mishahara minono, nyumba za kuishi na marupurupu kadhaa.

 

Exploitation... CCM big wigs authorize that by OUT OF YOUR FACE MWL. NYERERE - AZIMIO LA ZANZIBAR!!!
 
Watanzania wanaoneana! Na kuna vidampa ambao hata tajiri akisema tufanyeje kuboresha hali wenyewe wanasema zinawatosha hizo hizo. Mlalamikaji amesema tajiri hana shida. Hizi ngozi zetu!

Ndugu mlalamikaji, unapaswa kwenda kulalamika labour department. Haki yako utapata.
Watanzania wanaonewa kwenye nchi yao .. Hakuna haki.. Hakuna pa kukimbilia .. Hadi tembo nao hawana pa kukimbili labda waende kenya

.
 
Yaani inasikisha sana,na kweli inawezekana Mmiliki hajui yote haya!awe anastukiza na kuomba kuongea na wafanyakazi pekee pasipo uongozi wao,asikilize mambo yote!atapata ukweli wote!watanzania roho mbaya sana wakipewa vyeo mbuzi!hovyo sana!
 
Ndiyo maana bongo karibia kila mtu mwizi halafu ufisadi ni sifa!

80,000 kwa mwezi hapo Dar mtu anaishi vipi?Tena amefanya hapo kwa miaka 15?Ama labda kuna other benefits?
 
Coming in from the cold
We and dem
Them Belly fully

zote za Bob Marley ziwape matumaini.....

Bado tunanjia ndefu sana Tanzania....
 
Thirs is gonna tarnish the image of the company...
 
tatizo wabongo tunabaniana, hatupendani, sasa we kampuni c yako na mwenye hela yake ameshasema watu waongezewe sasa we kusign hutaki
 
Bakhresa fukuza meneja huyo anakuharibia sifa yako
 
lamsingi ni kupiga tu hapo hamna jingine....ndo maana kila kukicha makampuni yanalizwa mamilioni.....
 
Watanzania wanaoneana! Na kuna vidampa ambao hata tajiri akisema tufanyeje kuboresha hali wenyewe wanasema zinawatosha hizo hizo. Mlalamikaji amesema tajiri hana shida. Hizi ngozi zetu!

Ndugu mlalamikaji, unapaswa kwenda kulalamika labour department. Haki yako utapata.

.

Huko labour ndio kuna walarushwa kibao, labda labour ya hapo ulipo.
 
Hivi karibuni nilichangia mada inayohusu wimbi la Wahindi nchini. Kampuni za Bakhresa zinachangia kwa kiasi kikubwa tatizo hili. Hapa nakosa mwelekeo. Hawa watu wanaingia nchini kupitia mipaka yetu au matundu yaliokosa ulinzi yameongezeka? "Victim" mmoja wa kiwanda cha Cola cha Bakhresa anadai kwamba watoto wa kike wanaajiriwa kiwandani hapo na qualification ya muhimu ni uwezo wa kuwastarehesha Wahindi hao. Na muajiri hapa pia ni Mhindi(?) au mTZ mwenzetu? Kazi kwelikweli.
 
Talking blues...na
Concrete jungle
Nazo zinaliwaza sana kwenye shida kama hizi.

Coming in from the cold
We and dem
Them Belly fully

zote za Bob Marley ziwape matumaini.....

Bado tunanjia ndefu sana Tanzania....
 
Bakhresa mfukuze huyo meneja atakuharibia sifa yako hapa inchini.
 
Suleiman Mbacha: Je huyu ni Mtanzania? Maana wa TZ kwa kujipendekeza hatujambo.
 
Watanzania wanaonewa kwenye nchi yao .. Hakuna haki.. Hakuna pa kukimbilia .. Hadi tembo nao hawana pa kukimbili labda waende kenya

Watanzania hawana nchi, Kagasheki amekwisha sema NCHI YOTE NI MALI YA RAIS kwa mujibu wa Katiba na CCM! Kama CCM ndo wanasema hivyo, wewe bado una ota una nchi! Watanzania ni sawa na wapangaji kwenye nyumba ya JK! Tutaonewa sana, Tutanyanyaswa sana, Tutanyonywa sana na Tutapuuzwa sana kama tukiendelea kutawaliwa na CCM!
 
Back
Top Bottom