mengine ehe lakini mengine kineheee!!!!

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
hivi kweli haya yanaweza kutokea ndani ya nchi yetu?

hivi watanzania kudhalilishwa na kugeuzwa panya wa maabara ndani ya nchi yao ndani ya hospitali tunazoziheshimu tena bila ya haya mchana ni uungwana huu?

jee serikali imepanga kuwachukulia hatua gani hawa waliohusika na haya?

au ndio limeisha ?


Wajaribiwa dawa ya UKIMWI kinyume na maadili
Habari Zinazoshabihiana


Na Joseph Lugendo

MBUNGE wa Karatu, Dkt. Wilbroad Slaa (CHADEMA), amesema Watanzania 64 walifanyiwa majaribio ya utafiti wa dawa ya UKIMWI aina ya Virodene Po 58, katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, Dar es Salaam na kwenye zahanati iliyokuwa inamilikiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi mstaafu, Bw. Omar Mahita kinyume na maadili.

Dkt. Slaa jana bungeni aliitaka Serikali kutaja chombo ambacho kilitoa kibali cha majaribio ya aina hiyo kwa Watanzania, wakati dawa hiyo ilikuwa imepigwa marufuku Afrika Kusini ilikotengenezwa.

Aidha, Mbunge huyo pia aliitaka Serikali kueleza hatua ambazo zimechukuliwa dhidi ya Watanzania wakiwamo wanajeshi walioingiza dawa hizo na kufafanua kama waliofanyiwa majaribio hayo walilipwa
fidia.

Akijibu hoja hizo, Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Aisha Kigoda, alikiri kufanyika kwa majaribio hayo na kufafanua kwamba yalifanyika kinyume na taratibu za utafiti.

Dkt. Kigoda alisema ombi la kibali cha kufanya utafiti huo liliwasilishwa katika Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Julai 2000 na baada ya tathmini ya taasisi hiyo, ombi hilo likakataliwa.

Alisema kukataliwa kwa ombi hilo kulisababishwa na matokeo ya tathmini hiyo yaliyoonesha kuwa utafiti huo ulikuwa na upungufu wa kisayansi na kimaadili.

Kwa mujibu wa Dkt. Kigoda, baada ya kukataliwa kwa ombi hilo, wanasayansi hao waliamua kuingiza dawa hizo bila kibali cha Serikali na kufanya utafiti katika Hospitali ya Lugalo na wakati huo huo kuanza kuziuza dawa hizo kiholela.

Dkt. Kigoda alisema Agosti, 2001 Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilipata habari ya kufanyika kwa vitendo hivyo na kuamua kutoa agizo la kusitisha utafiti, kuwafukuza watafiti wahalifu, kuzuia uingizwaji wa dawa hizo na kuzirejesha dawa zilikotoka.

Hata hivyo, Dkt. Kigoda hakufafanua zaidi juu ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya Watanzania wakiwamo wanajeshi ambao walihusika kuingiza dawa hizo na kufanya utafiti huo, lakini akashauri Watanzania waliohusishwa katika utafiti huo, kufuata taratibu za sheria iwapo watataka kulipwa
fidia.


majira
 
....Kwa mujibu wa Dkt. Kigoda, baada ya kukataliwa kwa ombi hilo, wanasayansi hao waliamua kuingiza dawa hizo bila kibali cha Serikali na kufanya utafiti katika Hospitali ya Lugalo na wakati huo huo kuanza kuziuza dawa hizo kiholela.

Dkt. Kigoda alisema Agosti, 2001 Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ilipata habari ya kufanyika kwa vitendo hivyo na kuamua kutoa agizo la kusitisha utafiti, kuwafukuza watafiti wahalifu, kuzuia uingizwaji wa dawa hizo na kuzirejesha dawa zilikotoka.

Hapa ndo unagundua ni jinsi gani hawa jamaa wanaweka maisha yetu at stake!! Ivi kweli m2 anaingiza dawa na hata kuziuza kupitia Hospitali ya Jeshi (Lugalo) bila serikali kuwa na taarifa? au huu ni usanii wa Kirichmond??
Hapa pia inatakiwa wahusika wote wawajibishwe kuanzia aliyekuwa mkuu wa majeshi, mganga mkuu wa hiyo hospitali, FDA na wengine wote...
Na kama walifukuzwa ni nani atalipa hizo fidia??

Aisha Kigoda tafadhali tunaomba utoe utaratibu wa kudai fidia na pia jinsi gani mtawasaidia hawa waliofanyiwa majaribio iwapo hizi dawa zitawaletea madhara...

Hapa ni mpaka kieleweke...
 
hivi kweli haya yanaweza kutokea ndani ya nchi yetu?

hivi watanzania kudhalilishwa na kugeuzwa panya wa maabara ndani ya nchi yao ndani ya hospitali tunazoziheshimu tena bila ya haya mchana ni uungwana huu?

jee serikali imepanga kuwachukulia hatua gani hawa waliohusika na haya?

au ndio limeisha ?

Mimi naamini kabisa hawa jamaa walio fanya hiyo research watakuwa walipata baraka zote kutoka serikalini na kwenye mamlaka husika.
kukanusha hata vile vyenye ukweli ni jadi ya viongozi wetu. Naamini kama mtu ataamua kulifatilia kwa makini atakutana na vibali vya huo utafiti.
 
Hii si ndio hospital teule ya viongozi wetu ( japokuwa wanaenda kutibiwa mafua london)

Ikiwa haya yanaweza kufanyika ktk Hospitali ya jeshi yenye hadhi ya kutibu viongozi wetu wa juu nini kitazuia madudu yasifanyike ktk hospitali ya kindwetwe kule Rufiji?
 
Uongozi wa nchi unapotumbukia katika ufisadi kila jambo linawezekana.
Wanaweza hata kuwauza mama wazazi wao.
 
Back
Top Bottom