Mengi ni mfano wa kuigwa au wa kuogopwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mengi ni mfano wa kuigwa au wa kuogopwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bravo777, Jul 26, 2012.

 1. B

  Bravo777 Member

  #1
  Jul 26, 2012
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Juzi nilimshangaa mbunge mmoja alipokuwa akichangia hotuba ya Wizara ya Habari na kudai eti Mengi ni 'mfano wa kuigwa' katika kushughulikia maslahi ya wafanyakazi. Ukweli ni kwamba waandishi wa habari ndani ya IPP Media wanateseka sana kwa kucheleweshewa au kutolipwa kabisa mishahara kiasi cha wengi wao kuacha kazi na kukimbilia vyombo vingine. Nawajua waandishi kadhaa ambao wameondoka IPP huku wakiwa bado wanadai malimbikizo ya mishahara na stahili nyingine ya siku nyingi, miezi kadhaa. Anawatumia waandishi kujiendeleza yeye mwenyewe kibiashara, halafu anawatosa kiaina, wengi wao bila hata kuwalipa stahili yao! Mfano wa kuigwa? Hiyo ni kichekesho.

  Huyu hawezi kuwa mfano wa kuigwa, bali wa kuogopwa sana. Nasubiri wapambe wake waingie humu kumtetea ili niweke mambo yote hadharani, tena kwa SERIES.
   
Loading...